Mjumbe maalum wa Marekani George Mitchell akutana na Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Marekani na Israel zinajibidisha kutatua tofauti kati yao kuhusu makaazi ya walowezi katika ardhi ya Palestina.
Mjumbe maalum wa Marekani Mashariki ya Kati, George Mitchell alifanya mazungumzo yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu, na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, huku bado tofauti zikwepo, baina ya washirika hao wawili kuhusu makaazi ya walowezi wa kiyahudi huko West Bank. Na nchini Iraq, Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates alifanya ziara ambayo haikutarajiwa kwa mara ya kwanza tangu vikosi vya Marekani kuondoka katika miji ya Iraq.
Mkutano kati ya Netanyahu na Mitchell ulifanyika faraghani katika afisi ya Waziri huyo mkuu mjini Jerusalem.
Ilikuwa dhahiri katika mazungumzo yao, Viongozi hao wawili walikuwa wanajaribu kuziba nyufa zilizojitokeza katika uhusiano kati ya Marekani na Israel kuhusiana na hatua ya Israel kuendelea na ujenzi wa makaazi ya kiyahudi huko Jerusalem Mashariki. Utawala wa rais Obama haujaficha, hadharani na faraghani umesisitita kwa juhudi zozote za amani kufaulu ni lazima Israel isitishe ujenzi wa makaazi hayo. Ndio ujumbe Mitchell alifika nao kutoka mjini Washington.
Israel hata hivyo ina msimamo tofauti......inataka kuendeleza baadhi ya ujenzi ili kuwapa makaazi Wayahudi wanaoishi Jerusalem Mashariki na huko West Bank.
Bildunterschrift:
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas akutana na George Mitchell.
Jana katika mkutano wake na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas huko Ramallah- Mitchell alikiri kuwepo kwa tofauti kati ya Marekani na Israel, na kwamba utawala wa Rais Barack Obama bado haujapata ufumbuzi wa swala la kuishurutisha Israel isimamishe kabisa ujenzi wa makaazi katika ardhi inazozikalia za Palestina. ''' Msimamo wa kisiasa wa Marekani haujabadilika- Israel lazima isitishe ujenzo wote kama hatua ya kwanza ya kupatikana kwa amani ya kudumu katika eneo hilo.'' alisema Mitchell.
Alipokutana na Rais wa Israel Shimon Peres, Mitchell alimhakikishia Peres kwamba tofauti zao kuhusiana na swala la ujenzi watajadiliana kama marafiki na washirika wakuu, na kwamba swala hili halitaathiri uhusiano wa muda mrefu kati ya Marekani na Israel.
Mitchell pia aliwatolea wito mataifa mengine ya Kiarabu kuanzisha juhudi za kuanzisha upya uhusiano na Israel. Mpatanishi mkuu wa Palestina Saeb Erakat ambaye pia alikutana na Mitchell aliishtumu Israel kwa kutumia upanuzi wa makaazi katika ardhi ya Palestina kama kisingizio cha kukwamisha juhudi za upatanishi na kupatikana kwa dola la Kipalestina.
Tukiingia nchini Iraq- Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates alifanya ziara ambayo haikutarijiwa nchini Iraq. Gates alifika Iraq baaada ya ziara fupi nchini Israel na Jordan katika mfulilizo wa ujumbe mzito wa Marekani kufufua juhudi za amani Mashariki ya Kati.
Robert Gates afanya ziara ya kwanza Iraq, tangu vikosi vya Marekani kuondoka katika miji mikuu, Juni 30.
Nchini Israel Gates alisema Iran yenye nyuklia Iran ni tihsio kubwa kwa usalama wa eneo zima la Mashariki ya Kati.
Ziara ya Gates Iraq- ndiyo ziara ya pili ya afisa mkuu wa Marekani tangu vikosi vya Marekani kuondoka kutoka miji mikuu ya Iraq, tarehe 30 mwezi Juni. Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden alisherehekea siku ya uhuru wa Marekani, Julai 4 nchini Iraq. Ziara hii ya Gates pia inakuja wiki moja baada ya Waziri mkuu wa Iraq Nuri-al- Maliki kukutana na Rais Obama mjini Washington, Marekani.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar