Mugabe apongeza mkutano na EU | |||||||
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema mazungumzo baina ya maafisa waandamizi wa serikali yake na viongozi wa nagazi ya juu wa Umoja wa Ulaya yamefanikiwa sana. Baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika mjini Harare, kwa mara nyingine Bwana Mugabe alitaka vikwazo vya kimataifa vilivyowekewa nchi yake mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2002 viondolewe. Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nao kwa upande wake ulipongeza mkutano huo, lakini ukasema bado wakati muafaka wa kuondoa vikwazo haujafika na ukalalamika juu ya mwendo wa pole kuelekea mageuzi. Ujumbe huo wa Umoja wa Ulaya pia umepanga kukutana na waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai. Kabla ya kukutana na wajumbe hao wa Umoja wa Ulaya, Rais Mugabe alisema, anawakaribisha wajumbe hao kwa mikono miwili huku akiwa na matumaini mazungumzo yao yatazaa matunda. Lakini Bwana Mugabe pia alisema hawezi kubebeshwa lawama kutokana na mambo yaliyokwenda mrama Zimbabwe na kuzitupia lawama serikali ya mataifa ya Magharibi na vikwazo vya kimataifa, ambavyo alisema havina budi kuondolewa mara moja. Bwana Mugabe mwenye umri wa miaka 85 alisema kwa sasa hana mipango ya kuondoka madarakani kwa maelezo kuwa "najiona bado kijana". Ujumbe wa Umoja wa Ulaya ulioongozwa na Kamishna wa maendeleo Karel De Gucht, umeeleza kuridhishwa na mazungumzo hayo. Lakini kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Andrew Harding, akiwa mjini Harare, ujumbe huo wa Ulaya ulisisitiza hakukuwa na makubaliano yoyote lakini ni mazungumzo tu. |
Minggu, 13 September 2009
Enzi mpya kati ya Umoja wa Ulaya na Zimbabwe
Langganan:
Posting Komentar (Atom)
Tidak ada komentar:
Posting Komentar