Lieberman afanya ziara barani Afrika.
Waziri wa mambo ya nje wa Israel Avigdor Lieberman anatarajiwa kuwasili nchini Kenya leo jioni kuendelea na ziara ya nchi tano barani Afrika.
Waziri huyo alienza ziara hiyo nchini Ethiopia amelitaka bara la Afrika lisaidie katika juhudi za kuutatua mgogoro wa mashariki ya kati.
Waziri Lieberman amesema kutokana na uhusiano wake na nchi za kiarabu, Afrika inaweza kutoa mchango muhimu katika mashariki ya kati.
Waziri Lieberman amesema Israel inaitarajia Afrika isaidie katika kuleta mtazamo wa ukadirifu na kuleta maridhiano katika mashariki ya kati. Ameeleza kuwa ,kutokana na uhusiano wa nchi za Afrika na nchi za Kiarabu iwe katika medani ya Umoja wa nchi za kiarabu au Umoja wa nchi za Kiislamu-IOC,Afrika inaweza kuwa na ushawishi muhimu.
Waziri Lieberman ametoa mwito huo muda mfupi tu baada ya kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi- mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika kuzitaka nchi za Afrika zizifunge balozi za Israel .
Gaddafi aliwaambia viongozi wa nchi za Afrika kwenye mkutano wao wa kilele mjini Tripoli kwamba Israel inachochea migogoro barani Afrika na kwa hiyo balozi zake zifungwe.
Hatahivyo waziri wa Israel amesema harakati na maamuzi ya za nchi za Afrika yanapaswa kuonyesha mtazamo wa kujenga.
Amezitaka nchi za Afrika ziache kuwa na mtazamo wa kuegemea upande mmoja katika maamuzi yao.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Israel anafanya ziara barani Afrika kwa lengo la kuendeleza uhusiano wa kibiashara sambamba na kutafuta kuungwa mkono kidiplomasia katika bara ambapo pana mtazamo thabiti wa kuziunga mkono nchi za kiarabu.
Waziri wa mambo ya nje wa Israel bwana Lieberman leo anatarajiwa kuwasilisi nchini Kenya .
Katika ziara yake barani Afrika waziri huyo pia atazitembelea,Ghana, Nigeria na Uganda.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar