RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI NA DMITRY MEDVEDEV WA RUSSIA
Akihutubia baraza kuu la umoja wa mataifa, rais wa Urusi Dmitri Medvedev ameueleza uamuzi wa Marekani wa kutoendelea na mradi wake wa ngao dhidi ya makombora katika bara la Ulaya kuwa ni hatua muhimu kuelekea katika mwelekeo sahihi.
Akizungumzia mzozo wa mwaka jana wa kivita kati ya Urusi na Georgia, Medvedev ameshauri kupatikana mkataba mpya wa usalama katika bara la Ulaya ili kutatua mizozo kama hiyo.
Leo Alhamis, rais Barack Obama anatarajiwa kuwa mwenyekiti wa mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa, ikiwa ni mara ya kwanza kwa rais wa Marekani kufanya hivyo tangu kuundwa kwa baraza hilo mwaka 1946.
Kikao hicho cha leo kitalenga katika kupunguza silaha za kinuklia. Azimio lililotayarishwa na Marekani linatarajiwa kuyatolea wito mataifa kuondoa kabisa hazina zao za silaha za kinuklia kwa kutia saini na kuidhinisha mkataba unaozuwia kuenea kwa silaha hizo pamoja na mkataba unaozuwia majaribio ya silaha za kinuklia. Mkataba wa pili bado haujaidhinishwa na Marekani pamoja na mataifa mengine manane yaliyo na teknolojia ya kinuklia, ikiwa ni pamoja na India na Pakistan.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar