Rabu, 16 September 2009

New Brand for USD 250. Price negotiable.

Warning: IT IS NOT THE APPLE IPHONE PRODUCT


descriptions:

Style

Smartphone

Status

UNLOCKED

Languages

English / French / Italian / Arabic / Russian / Viatnamese / Portugues / Spanish / German

Screen

3.5'' screen / 16 million color QVGA / PX : 320*240

Bluetooth

Enabled

Data Transfer bluetooth

Radio

FM radio

Memory

2GB TF for free (INCLUDED IN PHONE) MAX SUPPORT 16GB

Camera

1.3 MP camera for Picture & Video capability, Tested put out biggest size is 640*480

Bandwidth

Quad-band (850/900/1800/1900Mhz)

SIM card Slot

Dual Active SIM (Two active lines operates)

Ring tones

64 chord ring tone / Stereo Loud speaker

Telephone Directories

Music

MP3

Movie

MP4, 3PG (watch movie upto 8hrs)

Messages &
Multimedia Messaging

200 SMS / MMS

Game

Built in games (5 built-in common games)

Functions

Hands free / Voice recorder / self-designed ringtones / photo editor / calculator / otepad / health management / calendar / To do list / Alarm / World Clock / Spot watch

Communication

WAP / GPRS / JAVA

Scheduled Power On/Off

Starting and shutting images as your wish / auto power off

Alarm Clock

MP3 alarm clock / MP3 alarm clock

Keyboard

Touch screen / Handwriting Stylus

WEB

GPRS / WAP

Em@il

POP3 and IMAP

Conversions

Unit conversion / Currency conversion

Warrant

6 months with the company. (3 days check and free shipping to and fro the company USA for maintenance)

Extra features

shake control. forward, rewind music by shaking the phone. also next picture or backward by shaking the phone.

Operating System

Applications

slide to unlock

> Works

Worldwide


> Parameters :

Interface

USB

Stand-by time

7 to 10 days

Talk time

3 to 4 hrs

Dim (l x w x d)

115 x 61 x 11.5 mm

Weight

100 g


> In the Box :

1 x

Celphone full Touch screen smartphone

2 x

Lithium batteries (2 X 1800 mAh)

1 x

Wall charger

1 x

2GB TF memory card

1 x

Earphones

1 x

USB cable

1 x

User manual


1 x

Car charger (1st Gift)







Minggu, 13 September 2009

Enzi mpya kati ya Umoja wa Ulaya na Zimbabwe

Mugabe apongeza mkutano na EU

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe
Rais Robert Mugabe alaumu vikwazo kwa kuidhoofisha nchi yake
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema
mazungumzo baina ya maafisa waandamizi wa
serikali yake na viongozi wa nagazi ya juu wa Umoja
wa Ulaya yamefanikiwa sana.

Baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika mjini

Harare, kwa mara nyingine Bwana Mugabe alitaka

vikwazo vya kimataifa vilivyowekewa nchi yake mara

baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2002 viondolewe.

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nao kwa upande wake

ulipongeza mkutano huo, lakini ukasema bado wakati muafaka wa

kuondoa vikwazo haujafika na ukalalamika juu ya mwendo wa pole kuelekea mageuzi.

Ujumbe huo wa Umoja wa Ulaya pia umepanga kukutana na waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai.

Kabla ya kukutana na wajumbe hao wa Umoja wa Ulaya, Rais Mugabe alisema, anawakaribisha wajumbe hao kwa mikono miwili huku akiwa na matumaini mazungumzo yao yatazaa matunda.

Lakini Bwana Mugabe pia alisema hawezi kubebeshwa lawama kutokana na mambo yaliyokwenda mrama Zimbabwe na kuzitupia lawama serikali ya mataifa ya Magharibi na vikwazo vya kimataifa, ambavyo alisema havina budi kuondolewa mara moja.

Bwana Mugabe mwenye umri wa miaka 85 alisema kwa sasa hana mipango ya kuondoka madarakani kwa maelezo kuwa "najiona bado kijana".

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya ulioongozwa na Kamishna wa maendeleo Karel De Gucht, umeeleza kuridhishwa na mazungumzo hayo.

Lakini kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Andrew Harding, akiwa mjini Harare, ujumbe huo wa Ulaya ulisisitiza hakukuwa na makubaliano yoyote lakini ni mazungumzo tu.

Senin, 07 September 2009

Mmiliki wa Chelsea Abramovich aelekea kileleni Kilimanjaro


MMILIKI wa klabu ya soka ya Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu ya England, Roman Abramovich amefanikiwa kupanda Mlima Kilimanjaro na kesho anatarajiwa kufika kileleni.

Wakizungumza na Mwananchi baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya African Environment ambao ndio wanamsaidia tajiri huyo kupanda mlima huo, mteja wao leo anatarajia kufika eneo la barafu umbali wa mita 4,800 toka usawa wa bahari.

Mwongozaji wa kampuni hiyo aliiambia Mwananchi jana kuwa walikuwa katika eneo la Karanga umbalo lipo umbali wa mita 4,200 toka usawa wa bahari.

"Ni kwamba anapanda vizuri na amekuwa na juhudi kubwa na tuna imani atafika kileleni wa kuweka historia,"alisema mwongozaji huyo.

Hata hivyo, alisema katika mazungumzo yake anaonekana kufurahia kupanda mlima huo na kama akishawishiwa vizuri anaweza kuileta hapa nchini Chelsea ili kupanda mlima huo.

"Anafurahia sana kupanda mlima na alikuwa hajui kama anafahamika katikaTanzania, ameshangaa na hata kuona kuna mashabiki wa klabu,"alisema mwongozaji huyo.

Hata hivyo, katika upandaji mlima huo imekuwa ni vigumu billionea huyo kujichanganya na wasaidizi wake 115 ambao wanamsaidia yeye na wenzake watano kupanda mlima huo.

Tajiri huyo alianza kupanda mlima huo Septemba 3 kwa kupelekwa na helikopta maalum baada ya kutembelea viwanja vya farasi vilivyopo katika eneo la maji ya Chai, wilayani Arumeru

Amekuwa akisindikizwa na kikosi cha askari wa kampuni binafsi ya Warrior Security, walinzi wake na maafisa wa kampuni ya uwakala wa utalii ya African Environment.

Ziara hiyo imekuwa yenye ulinzi mkali huku walinzi wakiwaizuia picha kupigwa, Abromovich anapanda mlima huo akipitia njia ya Lemosho iliyopo eneo la West Kilimanjaro.

Bilionea huyo anatarajiwa kushuka mlima huo, Septemba 10 kupitia geti la Mwika ambapo anatarajiwa kupokelewa na kupewa cheti cha kupanda mlima huo ambapo tayari kuna taarifa mamia ya watu wakiwemo viongozi wa serikali, michezo na viongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) watakuwepo.

mazoezi ya kijeshi ya nchi za Africa Mashariki


Rais Jakaya Kikwete akiipeperusha bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuashiria kuzindua rasmi mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya nchi za jumuiya hiyo Monduli, mkoani Arusha jana. (Picha na Freddy Maro).

Minggu, 06 September 2009

Gadaffi azitaka nchi za Africa kuzifunga Balozi za Israel..

Lieberman afanya ziara barani Afrika.

Waziri wamambo ya nje wa Israel Avigdor Lieberman atoa mwito kwa Afrika, isaidie katika mashariki ya kati.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Avigdor Lieberman anatarajiwa kuwasili nchini Kenya leo jioni kuendelea na ziara ya nchi tano barani Afrika.

Waziri huyo alienza ziara hiyo nchini Ethiopia amelitaka bara la Afrika lisaidie katika juhudi za kuutatua mgogoro wa mashariki ya kati.

Waziri Lieberman amesema kutokana na uhusiano wake na nchi za kiarabu, Afrika inaweza kutoa mchango muhimu katika mashariki ya kati.

Waziri Lieberman amesema Israel inaitarajia Afrika isaidie katika kuleta mtazamo wa ukadirifu na kuleta maridhiano katika mashariki ya kati. Ameeleza kuwa ,kutokana na uhusiano wa nchi za Afrika na nchi za Kiarabu iwe katika medani ya Umoja wa nchi za kiarabu au Umoja wa nchi za Kiislamu-IOC,Afrika inaweza kuwa na ushawishi muhimu.

Waziri Lieberman ametoa mwito huo muda mfupi tu baada ya kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi- mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika kuzitaka nchi za Afrika zizifunge balozi za Israel .

Gaddafi aliwaambia viongozi wa nchi za Afrika kwenye mkutano wao wa kilele mjini Tripoli kwamba Israel inachochea migogoro barani Afrika na kwa hiyo balozi zake zifungwe.

Hatahivyo waziri wa Israel amesema harakati na maamuzi ya za nchi za Afrika yanapaswa kuonyesha mtazamo wa kujenga.

Amezitaka nchi za Afrika ziache kuwa na mtazamo wa kuegemea upande mmoja katika maamuzi yao.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Israel anafanya ziara barani Afrika kwa lengo la kuendeleza uhusiano wa kibiashara sambamba na kutafuta kuungwa mkono kidiplomasia katika bara ambapo pana mtazamo thabiti wa kuziunga mkono nchi za kiarabu.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel bwana Lieberman leo anatarajiwa kuwasilisi nchini Kenya .

Katika ziara yake barani Afrika waziri huyo pia atazitembelea,Ghana, Nigeria na Uganda.

Rabu, 02 September 2009

Salamu toka kwa mdau...


Napenda kuchukua nafasi hii katika chombo chetu hiki cha kupashana habari kwa kuwapongeza waislamu wote wanaosoma katika chuo cha urafiki Lumumba kwa kumalizi siku kumi za kwanza za mfungo na mungu awajalie na awape nguvu,moyo na uwezo wakumalizia siku zilizo bakia. kila la kheri. Shabani H. Biboze kny. Waislamu wote RUDN

Selasa, 01 September 2009

Haya ni maeneo ya Miami huko Florida....usipime...



Nyani wahamishwa Ikulu kwa kumkojolea Rais

IKULU ya Zambia imeagiza kuhamishwa kwa nyani wapatao 200 kutoka kwenye viunga vya eneo hilo, baada ya mmoja wao kumkojelea Rais Rupia Banda.

Tukio hilo lilitokea mapema mwezi Juni, wakati Rais Banda akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na Wanadipolmasia, eneo la nje ya Ikulu.

Kwa mujibu wa wa gazeti la The Post (The Post Newspaper) la Zambia, baada ya tukio hilo Rais Banda alisikika kwa lugha yao ya Nyanja akisema kwa mstuko, : "Ahaa...kanitundila (yaani kanikojolea)," hali iliyofanya watu wote waliokuwepo kwenye mkutano huo kuangalia juu ya mti kuona nyani huyo aliyefanya kitendo cha utovu wa nidhamu.

Gazeti hilo lilifafanua kwamba, Rais Banda baadaye alimwagiza Mtaalamu wa Taasisi ya Wanyama kwenye Bustani hiyo ya Ikulu Munda Wanga, kuwaondoa nyani hao.

Katika zoezi hilo la hamisha hamisha wanyama hao, gazeti hilo lilisema zilitumika jumla ya dola za Marekani 50,000 sawa na zaidi ya Sh 70 milioni za Tanzania.

“…Rais alitaka baadhi ya nyani hao kupelekwa maeneo mengine kutoka makazi ya watu na kurejeshwa porini,"alifafanua Meneja Masoko Fred Hengeveld, kutoka Taasisi ya Wanyama ya Munda.

Gazeti la The Post lilifanua kwamba, katika zoezi hilo jumla ya nyani wapatao 61 walikamatwa na kuondolewa viunga vya Ikulu hiyo.

Tukio hilo la kusisimua ambalo lilitokea Juni 24 wakati Rais Banda akizungumza na waandishi na wana diplomasia hao huku kima hao wakiwa juu ya mti, limeshangaza wananchi wengi wa Zambia kwani ni la kwanza kuwahi kutokea maeneo ya Ikulu tangu marais mbalimbali waliopita kuitisha mikutano kwenye viunga hivyo.

Baadhi ya wanasiasa wa upinzani wamekuwa kete hiyo ya kima kama hatua ya kumdhihaki kiongozi huyo mkuu wa nchi kutokana na kitendo hicho cha 'kutundilwa' na nyani.

Rais Banda aliingia madarakani mapema mwaka huu baada ya kifo cha Rais Levy Mwanawasa, ambaye alifariki kutokana na ugonjwa wa Kiharusi nchini Ufaransa.

Hali ni mbaya CHADEMA


HALI ya kisiasa ndani ya Chadema imezidi kuchafuka baada ya uchaguzi wa Baraza la Vijana Taifa (Bavicha) kuahirishwa kwa miezi sita, huku mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo (jina tunalo) akitishia kumchoma kisu mwanachama anayeaminika kuwa kambi ya naibu katibu mkuu, Zitto Kabwe.

Wakati hatma ya uchaguzi huo ikiwa bado njia panda, mizengwe imezidi kutikisa uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake baada ya mmoja wa wagombea anayeaminika kuwa upande wa Zitto kunusuruka kung'olewa.

Joto zaidi linaloonyesha hali tete ndani ya Chadema, lilipandishwa na hatua iliyotangazwa jana mchana na katibu mkuu, Dk Wilbrod Slaa ya kuahirisha uchaguzi huo hatua ambayo ilipingwa na Zitto na msemaji wa chama hicho David Kafulila ambao wanataka kutangazwa kwanza kwa matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika juzi na kuitishwa kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CC), ambacho inasemekana kinafanyika leo.

Wagombea waliokuwa wakiwania nafasi ya uenyekiti wa Bavicha ni John Heche, Dadi Igogo na David Kafulila ambaye licha ya kuwa ofisa habari wa chama hicho, anatarajiwa kuwania ubunge Jimbo la Kigoma Kusini mwaka 2010.

Akitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi huo jana, Dk Willibrod Slaa alisema uchaguzi huo utafanyika ndani ya miezi sita ijayo.

“Mimi kama katibu nimeshauriana na kamati ya wazee ya chama nikiongozwa na Mzee (Edwin) Mtei, Bob Makani na Balozi (Christopher) Ngaiza tumeubatilisha uchaguzi huo, hivyo utafanyika ndani ya miezi sita ijayo,” alisema Slaa.

“Tumeamua hivi kwa sababu kwanza kufanya uchaguzi ni gharama, tunatumia karibia Sh50 milioni ambazo zinaweza kujenga zahanati moja. Jamani hapa tutawaeleza nini Watanzania.

“Wajumbe walidai kuwa uchaguzi ulijaa rushwa, lakini niliwambia waandike malalamiko kwa maandishi na ujumbe mfupi na wamenipatia nitayafanyia kazi na yatatolewa maamuzi na vyombo husika.”

Lakini Zitto alipinga uamuzi huo akisema katibu mkuu hana mamlaka ya kutoa tangazo hilo na kwamba nanlaka hayo ni Kamati Kuu (CC).

"Lakini pia, chombo pekee chenye uwezo wa kufanya uamuzi huo ni Kamati Kuu, sasa inakuaje chombo kingine kichukue uamuzi tena bila matokeo kutangazwa wala mgombea kukata rufaa," alisema Zitto.

Alifafanua kuwa uamuzi huo umetokana na baadhi ya watu kukataa matokeo hayo baada ya kuweka mbele maslahi binafsi badala ya maslahi ya chama kwa kuwa jambo la msingi katika suala hilo ni matokeo hayo kutangazwa kwanza kabla ya kuahirisha uchaguzi.

"Jambo la kwanza ni kutangaza matokeo na baadaye kama kuna mgombea alikuwa akipinga, anaweza kukata rufaa, lakini matokeo hayajatangazwa wala hakuna aliyekata rufaa," alifafanua Zitto.

Kutokana na utashi wa katiba, Zitto alisema tayari amemwomba katibu mkuu kuitisha mkutano wa CC kujadili suala hilo.

"Nimemwomba Dk Slaa aitishe kikao cha Kamati Kuu tujadili hii hali maana kama viongozi hatutakuwa na busara na chama kitavurugika," alionya.

Alipoulizwa nini mustakabali wa Chadema kutokana na matukio hayo ya vurugu yanayotikisa chama, alijibu: "Viongozi tusipotumia busara chama kitavurugika, lakini tukitumia busara na kuweka maslahi ya chama mbele, tutaweza kutatua haya mambo kwa urahisi."

Zitto alihoji: "Kwanini wazee wasitumie busara kama walizotumia kuniomba mimi nijitoe kwa kutaka wagombea wengine wajitoe au wakubali matokeo kwa kumwachia Kafulila?

"Tukiwa na busara; tukiheshimu demokrasia, tutaweza kuvuka salama. Naamini hilo tu ndiyo suluhisho la kukivusha chama salama."

Naye Kafulila alipinga uamuzi wa kuahirisha uchaguzi kabla ya kutangaza matokeo akisema anataka kutangazwa kwanza kwa matokeo ambayo anaamini, yalimpa ushindi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kafulila alisema haoni sababu ya kutotangazwa kwa matokeo hayo ambayo anaamini alishinda licha ya kutokubalika na sehemu kubwa ya wajumbe wa sekretarieti na wabunge wa viti maalum.

"Ukiangalia hata hayo mambo ya karatasi kuongezeka, utaona labda ulikuwa ni mpango maalumu wa kumwangusha mtu fulani, lakini imeshindikana," aliongeza.

"Kwa kifupi, sikubaliani na uamuzi huo ninachotaka kwanza matokeo yatangazwe na pia baraza halina mamlaka hayo. Hiyo ni kazi ya Kamati Kuu."

Habari zinadai kuwa tangu John Mnyika kuondoka kwenye wadhifa wa uenyekiti wa vijana wa Chadema, kumekuwa na mkakati wa kumdhibiti Kafulila unaofanywa na baadhi ya vigogo wa Chadema kutokana na mgombea huyo kuonekana mwiba kwao.

Kafulila anasemekana kuwa ni mtu anayepinga waziwazi mambo yanayoendeshwa kinyume na taratibu na amekuwa hahofii viongozi wa juu yake kueleza msimamo wake.

Wakati hayo yakiendelea, vurugu zaidi zimezidi kutikisa chama hicho na jana zilifikia katika hatua ya mgombea mmoja wa nafasi ya uenyekiti wa vijana kutaka kumchoma kisu mwanachama ambaye alikuwa akimtetea Zitto Kabwe asitukanwe na mgombea huyo.

Kabla ya kufikia hatua ya kutishiana visu, mgombea huyo alikuwa akibishana na baadhi ya wafuasi wa Kafulila kwenye ofisi za makao makuu ya Chadema zilizo Kinondoni jijini Dar es salaam.

Wakati Mwananchi inafika kwenye ofisi hizo majira ya saa 7:00, vurugu zilikuwa zimeshapoa tangu saa 5:00, lakini wanachama walikuwa wamekaa kwenye vikundi wakijadili matukio mbalimbali ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mgombea huyo na mwanachama mmoja anayedaiwa kuwa anamuunga mkono Kafulila, walirushiana ngumi kwanza na baadaye ndipo mgombea huyo alipotoa kisu na kumtishia.

Mashuhuda hao walidai kwamba mara baada ya mgombea huyo kutoa kisu, wanachama wengine waliokuwa karibu waliingilia kati na kumtoa eneo hilo.

Mwanachama anayedaiwa kutishiwa kisu aliiambia Mwananchi kuwa alikuwa akimsihi mgombea huyo kuacha kumsema vibaya Zitto kwa kuwa malalamiko yote ya uchaguzi wa juzi yako ngazi za juu za chama hicho.

Mwanachama huyo alifafanua kwamba baada ya kumwambia mgombea huyo maneno hayo, alipandisha ghadhabu zaidi na kuanza kutukana.

“Sasa mimi nilivyoona anamtukana Zitto, nilimwambia aache lakini hakusikia; alikuwa anasema Zitto wako na Kafulila walishirikiana kumwibia kura. Kutokana na kuendelea kuongea ovyo, tulishikana na alivyoona muziki ni mnene alinitolea kisu na kutaka kunichoma,” alidai.

Katika hatua nyingine, Dk Slaa juzi alilazimika kurudi katika ukumbi wa uchaguzi wa Bavicha mnamo saa 6:20 usiku ili kutuliza ghasia zilizoibuliwa na wajumbe mara baada ya kupata habari kuwa kura 20 ziliongezeka katika nafasi ya mwenyekiti.

Wajumbe hao ambao walionekana kuwa upande wa mgombea wa nafasi hiyo, John Heche ambaye ni diwani wa Tarime Mjini, walipinga matokeo kabla hayajatangazwa hali iliyomlazimu msimamizi wa uchaguzi huo, Charles Mwera, ambaye pia ni mbunge wa Tarime, kutoyatangaza.

Dk Slaa, ambaye aliondoka kwenye ukumbi huo juzi saa 7:00 mchana, alirejea kwa mara ya pili saa 6:20 usiku, vurugu zikiendelea baada ya Heche kumpiga ngumi mbili ofisa wa kurugenzi ya uchaguzi ya Chadema, Ali Chitandana na kumlazimu kufanya kazi kubwa kuzituliza.

“Jamani wajumbe nawaomba muwe watulivu kila kitu kilichotokea nimepewa taarifa na Mnyika, kwa hiyo kama kuna mtu ana malalamiko ayaandike na kuyawasilisha makao makuu ya chama kesho (jana) asubuhi ili niyafanyie kazi,” alisema Dk Slaa.

Katika hatua nyingine, wajumbe hao walimweleza wazi Dk Slaa kuwa hawajalipwa fedha zao za posho hali iliyomlazimu katibu huyo mkuu kumwagiza Mtunza Fedha kuwalipa wajumbe hao kutoka mikoa mbalimbali nchini usiku huohuo.

“Wewe Mtunza Fedha walipe wajumbe posho zao; jamani nimeshamwagiza atawalipa wote ila wale ambao wameshakata tiketi kwa ajili ya kusafiri watarudishiwa fedha zao kesho (jana) kwa sababu hamuwezi kuondoka kwa kuwa uchaguzi huu unaweza kurudiwa, lakini yote yatajulikana mara baada ya viongozi kukutana,” alisema Dk Slaa.

“Kwa kweli, nimesikitika sana hiki kitendo kilichotokea leo ni aibu kwa chama. Hapa wapinzani na magazeti yatapata pa kusemea.

Hiki chama ni cha demokrasia; nahitaji kujua kila kitu kilichotokea ili vifanyiwe maamuzi na yeyote atakayebainika kuhusika kwa namna moja au nyingine atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa katiba ya chama.”

Habari hii imeandikwa na Ramadhan Semtawa, Fidelis Butahe, Musa Mkama na Fred Azzah

Jumat, 28 Agustus 2009

huku ndo kunogewa na mziki au?

AFANDA SELE

Michael Jackson 'aliuawa', afisa aeleza


Afisa mchunguzi wa vifo huko Los Angeles nchini Marekani ametangaza rasmi kuwa kifo cha Michael Jackson kilisababishwa na mtu mwingine, Jackson alifariki mwishoni mwa mwezi Juni.

Alieleza kuwa kifo chake kilisababishwa na kupewa dawa ya ganzi aina ya propofol, na nyingine ya kutuliza maumivu aina ya lorazepam.

Chembe chembe za dawa nyingine aina nne tofauti pia zilikutwa katika mwili wa mwanamuziki huyo.

Mwandishi wa BBC aliyeko Los Angeles anasema hitimisho hilo linaongeza uwezekano wa kufunguliwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya madaktari waliokuwa wakimpatia Michael Jackson madawa hayo.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizotolewa hivi karibuni na ofisa huyo mchunguzi wa vifo, daktari binafsi Conrad Murray, aliyekuwa akimtibu Bw Jackson, aliwaeleza polisi alimpatia mwanamuziki huyo dawa aina ya propofol kumsaidia apate usingizi. Dr Murray amekana madai ya uhalifu.

Mazishi ya mwanamuziki huyo yamepangwa kufanyika Septemba 3 katika eneo la Forest Lawn Memorial Park huko Glendale, kitongoji cha Los Angeles, katika shughuli itakayokuwa ya faragha.

Mazishi hayo awali yalipangwa kufanyika tarehe 29 Agosti - siku ambayo angekuwa hai angetimiza umri wa miaka 51.

CCM ana kwa ana na maaskofu Katoliki

Atarajiwa kupoza mtafaruku wa Waraka

Kanisa lasita kumwalika kuwa mgeni rasmi wa hafla

WAKATI mjadala kuhusu waraka uliotolewa na Kanisa Katoliki ukipamba moto, Rais Jakaya Kikwete, leo Jumatano, anatarajiwa kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Mwanza Mhashamu Anthony Petro Mayala (69) atakapokutana uso kwa uso na Maaskofu wote wa Kanisa hilo ambao ndio waliobariki waraka huo.

KINGUNGE Ngombale Mwiru amekuwa mwepesi kuzungumzia waraka wa Kanisa Katoliki kuhusu jinsi ya kuchagua viongozi katika uchaguzi ujao kila mara alipotakiwa kufanya hivyo, na wakati mwingine aliita waandishi wa habari ili atoe msimamo wake, lakini jana alimudu kusema maneno mawili tu; "no comment".

Mbali na Kingunge, katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ambaye Halmashauri Kuu ya chama chake ilipendekeza kuwa viongozi wa dini wakutane na viongozi wa kisiasa kabla ya kutoa nyaraka zake, alitoa kauli kama ya Kingunge, hali kadhalika Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Sera, Uratibu na Bunge) Philip Marmo.

Mwananchi ilikuwa imetaka maoni yao kuhusu tamko la Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kuwa kanisa halitapokea maagizo wala maelekezo wakati wa kuandika nyaraka zake.

Waraka huo ambao umesambazwa na kuuzwa nchi nzima, unaelekeza waumini wa kanisa hilo kuchagua viongozi waadilifu, wapenda amani na wenye kujali zaidi maslahi ya wananchi.

Lakini baadhi ya watu, wakiongozwa na Kingunge wamekuwa

wakiupinga kwa madai kuwa unaweza kuwa hatari kwa amani.

Akiongoza ibada ya mazishi ya Askofu Anthony Mayalla juzi, Kardinali Pengo alieleza bayana kuwa si jukumu la viongozi wa kidini kupokea maagizo na maelekezo ya na wanasiasa wakati wa kutekeleza majukumu yake kwa sababu kufanya hivyo ni kukiuka misingi na maelekezo ya kanisa.

Kardinali Pengo alikwenda mbali zaidi alipotoa maneno yaliyoonekana kumlenga moja kwa moja Kingunge aliposema "wakomunisti siku zote wako mbali na Mungu, afadhali hata ya mapebari wanaamini kuwa Mungu yupo".

Kingunge anajulikana kama mmoja wa waumini wakubwa wa siasa za Kikomunisti na hula kiapo kwa kunyoosha mkono juu tofauti na wanasiasa wengine ambao hushika vitabu vitakatifu vya dini zao wakati wanapoapa.

Mwananchi ilipowasiliana na Kingunge jana kupata maoni yake kuhusu msimamo wa Pengo, alikiri kuwa hana hoja tena katika suala hilo.

"No comment (sina la kusema)," alijibu Kingunge na kukata simu. Kingune amekuwa akisisitiza kuwa waraka huo wa Kanisa Katoliki haufai na kulitaka kanisa liufute.

Na hata kanisa lilipomtaka aeleze ubaya wa waraka huo, aliendelea kusema haufai na kusababisha alaumiwe na viongozi wengi wa dini pamoja na wadau wengine wa masuala ya dini na demokrasia.

Kauli kama ya Kingunge ilitolewa na katibu mkuu wa CCM, Makamba."Sina lolote la kusema katika hilo. Wewe niulize ya CCM.

Kuna kura za maoni za kuwachagua wagombea wa serikali za mitaa," alisema Makamba, ambaye chama chake kiliratibu mkutano na waandishi wa habari ambao Kingunge aliutumia kusisitiza msimamo wake dhidi ya waraka wa Katoliki.

Baadaye Makamba alipozungumza tena na gazeti dada la Mwananchi The Citezen alisema: ÒNdugu yangu kila mtu amemsikia baba askofu, sasa unataka mimi niseme nini? Mimi sibishani naye hata kidogo na siwezi kusema abadilishe msimamo.

''Kimsingi, Mwadhama Pengo ni kiongozi mkubwa sana katika Kanisa Katoliki, siwezi kubishana naye hata kidogo.''

Hoja za kupinga na hata kuunga mkono waraka wa Kanisa Katoliki, zilianzia Bungeni Julai Mwaka huu.

Mjadala huo pia ulijadiliwa kwa hisia tofauti na wanasiasa, wasomi, viongozi wa dini na hata wananchi wa kawaida.

Mzee Kingunge, ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na kada anayeheshimika sana ndani ya CCM baada ya kufanya kazi kwa karibu na marais wa awamu zote nne, alionekana kutoa hoja nzito zaidi na hasa alipobeba msimamo wa chama hicho kutaka waraka huo uondolewe.

Kama hiyo haitoshi, CCM kupitia Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec), hivi karibuni, ilitoa azimio la kuwataka viongozi wa dini kukaa na viongozi wa dini ili kushauriana katika suala zima la utoaji wa waraka, ikiwa ni njia ya kuepuka kuvunja mshikamano wa kitaifa.

Lakini juzi, Kardinali Pengo alisema Kanisa Katoliki litaendelea kutoa nyaraka zake bila kuomba baraka kwa serikali na hata chama kwa sababu huo ni wajibu waokatika kufanya kazi ya Mungu.

"Waacheni maaskofu wafanye kazi zao na wasifundishwe kazi kwa maana kuandika waraka ni mamlaka kutoka kwa Mungu na si kwa uwezo wao.

Vyama visilazimishe kwamba ni lazima vitoe ushauri," alisema Pengo katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na Rais Jakaya Kikwete, mawaziri, wabunge na marais wastaafu.

Kardinalo Pengo pia alikemea wale ambao wanaonekana kuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ufisadi wakati hata ingekuwa wao ndio walio katika nafasi hizo, wangefanya vitendo hivyo vya wizi wa lami za umma.

Kuhusu kauli hiyo ya Kardinali Pengo dhidi ya vinara wa vita dhidi ya ufisadi, mmoja wa wabunge walio mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ufisadi, Aloyce Kimaro (Vunjo-CCM) alisema binafsi hana uhakika juu ya suala hilo lakini anajifahamu kuwa moyo wake ni safi.

Lakini alimwelezea Kardinali Pengo kama mmoja wa watu mahiri na wanaohitajika sana katika kuendeleza vita itakayowezesha kuwaangamiza mafisadi ili mali za Watanzania zibaki salama.