Urusi yatoa pendekezo la kuandaa mkutano wa kutafuta amani Mashariki ya Kati.
Pendekezo la Urusi la kutaka kuwa mwandalizi wa mkutano wa kutafuta kupatikana kwa amani katika eneo la mashariki ya kati limepata uungwaji mkono wa kimataifa na huenda na sasa mkutano huo huenda ukaandaliwa ifikiapo mwishoni mwa mwaka huu.
Urusi ambayo ni mwanachama wa pande zinazohusika na kupatikana kwa amani katika mashariki ya kati zikiwemo marekani , umoja wa mataifa na umoja wa Ulaya, kwa muda wa miaka minne sasa zimekuwa zikishinikiza kuandakliuwa kwa mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya mashariki ya kati.
"Ninaamini mkutano huu utafanyika, na pia ninaamini kuwa utafanyika mwaka huu hata kama utakuwa mwezi mei, Juni au Oktaba" , alisema mpatanishi mkuu wa umoja wa ulaya Marc Otte.
Marekani na Israel zinaonekana kulionea haya pendekezo hilo la Urusi ambalo hata hivyo limekaribishwa na Palestina. Uhusiano mzuri kati ya urusi na palestina umeanza tangu wakati wa utawala wa kisovieti.
Kinyume na nchi za magharibi, urusi imekuwa na uhusiano na kundi la Hamas suala ambalo limezua maswali la ni nani atahudhuria mkutano huo ikiwa utaandaliwa nchini Urusi.
Israel mara nyingi inapinga mikutano ya kimataifa kutokana na hofu kuwa mkutano kama huo ni kama kuungana miongoni mwa nchi za kiarabu dhidi yake.
Lakini Urusi pia ina uhusiano mwema na Israeli na haitaki kuuuweka uhusiano huo kwenye hatari , pia haitaki kuiweka Israel katika hali mbaya, lakini ingetaka mkutano huo ufanyike.
Wiki iliyopita urusi ilimpongeza rais wa marekani Barack Obama baada ya kuwaalika viongozi kutoka Palestina na Israel kwenda katika Ikulu, mwaliko amabo unaonekana kuwa mwanzo wa mpango wa kutafuta amani katika mashahariki ya kati.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Mfalme wa Jordan Abdullah wa pili pamoja na mfalme wa saudi Arabia Abdullah bin Abdul Aziz nao wameishinikiza marekani kushikiri vilivyo kwenye mpango huo wa kutafuta amani katika mashariki ya kati kulingana na shirika moja la habari la Saudi Arabia.
Mfalme wa Joran Abdullah wa pili alikutawa na mwenzake wa Saudi Arabia baada ya kurejea kutoka nchini marekanji alikofanya mkutano na rais wa marekani Barack Obama katika ikulu ambapo wote wawili walijadiliana masuala ya kimataifa likiwemo la mpango wa amani katika mashariki ya kati.
Katika mahojiano yaliyopeperushwa baada ya mkutano kwenye ikulu ,mfalme Abdullah wa pili aliitaka marekani kutangaza msimamo wake kabla waziri mkuu wa Israeli ,Benjan Netanyahu hajazuru marekani mwezi ujao.
Kati ya yale yanayohitajika kutimizwa kwenywe mpango huu ni pamoja na kusalimishwa kwa ardhi yote ya nchi za kiarabu iliyotekwa na Israel mwaka 1967 pamoja na ardhi ya palestina palestina ili Israeli iweze kutambuliwa na nchi za kiarabu kama taifa .
Hata hivyo waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahbu amekataa kukubali pendekezo la kuitambua Israel kama taifa na anatarajiwa kutangaza sera zake kabla ya kufanya ziara nchini Marekani.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar