Mapigano kati ya makabila mawili nchini Tanzania kugombea mifugo yamesababisha vifo vya watu tisa katika siku chahce zilizopita.
Mapigano kati ya kabila la Luo na Wakurya mkoani mara yamesababisha mamia ya watu kukimbia makazi yao.
Baadhi ya taarifa zinasema idadi ya watu waliokufa huenda ikawa watu arobaini.
Msemaji wa polisi amesema nyumba zimechomwa moto na ngombe kuibwa.
Waandishi wa habari wanasema wizi wa mifugo katika eneo hilo limekuwa la kawaida kwa miaka mingi, lakini mapigano sasa yanaonekana kuwa makubwa zaidi.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar