Chombo kinachohusika na uchaguzi nchini Iran , baraza la wadhamini, limekiri kuwapo na hitilafu katika uchaguzi wa rais ambao umemrejesha rais Mahmoud Ahmadinejad madarakani.
Msemaji wa baraza hilo ameiambia televisheni ya taifa ya Iran kuwa kura kadha zilizopigwa katika majimbo 50 zimepindukia idadi ya watu wenye haki ya kupiga kura.
Wagombea watatu waliokuwa wakigombea kiti hicho pamoja na Ahmadinejad wanalalamika kuwa hadi majimbo 170 kutoka jumla ya majimbo 366 ya uchaguzi yamekumbwa na hitilafu hizo.
Wakati huo huo , kiongozi wa upinzani nchini Iran, Mir Kossein Musavi, amewataka wanaomuunga mkono kuendelea na maandamano dhidi ya madai ya udanganyifu.
Mousavi amewaambia wanaomuunga mkono kuwa wanapaswa kupuuzia marufuku dhidi ya maandamano, lakini wanapaswa kuonyesha uvumilivu baada ya maafisa kuwakamata zaidi ya waandamanaji 450 mwishoni mwa juma.
Mapambano katika mitaa ya Tehran imesababisha watu kumi kuuwawa na zaidi ya wengine 100 kujeruhiwa siku ya Jumamosi. Serikali ya Iran inalaumu ghasia hizo kuwa zinaungwa mkono na mataifa ya magharibi.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar