Uingereza imeahidi kutoa paundi milioni tano zaidi kama msaada kwa Zimbabwe leo Jumatatu, na kusifu hatua za maendeleo zilizofikiwa na serikali mpya ya umoja wa kitaifa, lakini imehimiza mageuzi zaidi baada ya mazungumzo muhimu kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.
Akizungumza baada ya mazungumzo na waziri mkuu, Morgan Tsvangirai , ikiwa ni mazungumzo ya kwanza ya aina hiyo na kiongozi wa Zimbabwe kwa muda wa miongo miwili, waziri mkuu, Gordon Brown, ameahidi msaada zaidi, iwapo mpango wa mageuzi utapata kasi zaidi.
Fedha hizo za ziada dola milioni 8.2 zinafikisha kiasi cha paundi milioni 60, ikiwa ni msaada wa mpito kwa serikali ya Zimbabwe mwaka huu, Brown amesema , ambaye serikali yake ilikuwa inapingana na utawala wa rais Robert Mugabe kwa muda mrefu.
Lakini katika ishara nyingine ya kuchukua tahadhari, Brown amesema kuwa msaada huo wa ziada utapitia katika mashirika ya kutoa misaada badala ya kwenda katika serikali ya Zimbabwe moja kwa moja.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar