Mahakama  ya   umoja  wa  mataifa  inayowahukumu wale  waliopanga  mauaji  ya  kimbari  nchini Rwanda mwaka  1994 imemhukumu  kwenda  jela miaka  30  waziri  wa  zamani  wa  mambo  ya  ndani anayeshutumiwa  kuwadanganya  maelfu  ya  watu kujificha  mlimani  kabla  ya  kuuwawa.
Mahakama  hiyo  ya  kimataifa  ya  uhalifu  wa  kivita, yenye  makao  yake  nchini  Tanzania,  imesema callixte  Kalimanzira, mshirika  wa  karibu   wa  rais na  waziri  mkuu  wakati  wa  mauaji, alipatikana  na hatia  ya  mauaji  ya  kimbari  na  kula  njama  ya kufanya  mauaji.
Wanamgambo  wa  Kihutu  waliwauwa  Watutsi walio  wachache  wapatao  800,000  pamoja  na Wahutu  waliochukua  msimamo  wa  kati  katika siku  100  za  mauaji  ambayo  yaliishtusha  Afrika  na dunia  kwa  jumla.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar