Rais wa Somalia , ambaye madaraka yake yako hatarini akiwa katika jumba la rais mjini Mogadishu, ametangaza leo hali ya hatari katika juhudi za kupambana na mashambulizi makali ya wiki sita ya wapiganaji.
Tangazo hilo la rais Sharif Sheikh Ahmed limekuja huku kukiweko majadiliano juu ya kuchukuliwa hatua mpya ya kuingilia kati kuyaondoa makundi ya wapiganaji wa Kiislamu, miezi sita tu baada ya majeshi ya Ethiopia kufikisha mwisho hatua yao iliyodumu miaka miwili ya kuingilia kati.
Wiki sita baada ya kuzuka mapigano makali ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 300, udhibiti wa serikali hiyo katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu, Mogadishu, unapungua. Akizungumzia kuhusu hali nchini Somalia makamu wa rais wa Kenya Kalonzo Musyoka amesema.
Umoja wa Afrika umeeleza tena leo wasi wasi wake na kuidhinisha wito wa hapo kabla uliotolewa na Somalia wa kuomba usaidizi wa kijeshi kutoka nje.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Umoja wa Afrika, Jean Ping, amesema katika taarifa kuwa serikali ya Somalia ina haki ya kuomba msaada kutoka kwa mataifa wanachama wa Umoja wa Afrika pamoja na jumuiya ya kimataifa, kwa jumla.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar