Taarifa kutoka mji mkuu Tehran zinasema polisi wa kupambana na fujo wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wa upinzani wa mgombea aliyeshindwa katika uchaguzi wa juni 12,Mirhousein Mousavi. Kiasi cha waandamanaji 1000 wanasemekana wamesanyika katika uwanja wa Haft-e Tir ,ulioko katikati ya mji mkuu Tehran.
Maandamano hayo yanafanyika licha ya jeshi la mapinduzi linalomuunga mkono rais Mahmoud Ahmedinejad kutoa kitisho cha kuwatia adamu watakaoendelea na maamndamano hayo ya upinzani.Jeshi hilo limetoa taarifa likiwataja waandamanaji hao kama ni watu wanaozusha ghasia na wenye njama ya uhaini dhidi ya nchi hiyo jambo ambalo jeshi hilo limesema litakuwa tayari pamoja na polisi,vikosi vya usalama,ulinzi pamoja na jeshi la Basij kukabiliana nalo kwa hali zote.
Kiongozi wa upinzani Mir Hossein Moussavi hapo jana usiku aliwaambia wafuasi wake waendelee na maandamani lakini wajizuie kufanya ghasia.Hata hivyo taarifa ya Mousavi imedai kwamba kuna wafuasi wengine wasiokuwa kutoka kambi yake ambao wanajiingiza katika maandamano ya ghasia na ambayo serikali inadai yanafanywa na watu waliotumwa na nchi za magharibi kuzusha hali ya mtafaruku nchini Iran.
Wafuasi wa Mousavi hii leo wamerifu kwamba wanataka kuwasha taa za magari katika miji ya nchi hiyo kati ya saa 5 na saa 12 jioni ili kuonyesha imani yao kwa wahanga wa maandamano ya jumamosi,aidha imerifiwa katika tovuti ya Mosavi kwamba waandamanaji hao pia watabeba mishumaa ya rangi nyeusi iliyofungwa kitambaa cha kijani kuwakumbuka wahanga hao,hii ikiwa ni alama ya Mousavi ya kuonyesha harakati za mageuzi.
Hata hivyo kwa upande mwingine msemaji wa baraza kuu linalohusika na masuala ya uchaguzi Abbas Ali Kadkhodaeai amesema kwamba dosari za uchaguzi zilizozungumziwa na wagombea watatu walioshindwa katika uchaguzi Mir Hossein Mosuavi,Mehdi Kurroubi na Mohsen Rezaei hazijakubaliwa na baraza kuu.Shirika la habari la Iran IRNA ambalo linamuunga mkono rais Mahmoud AhmedNejad limezishutumu baadhi ya nchi za magharibi na vyombo vya habari vya kiarabu kwa kuyatafsiri vibaya matamshi ya msemaji wa baraza hilo.Bildunterschrift:
Kwa upande mwingine nchi za kiarabu zimevunja ukimya wake juu ya mzozop huo wa Iran umoja wa falme za kiarabu Emarati imejitokeza kumuunga mkono rais wa Iran.Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Sheikh Abdullah bin Zayed al Nahayan amekubaliana na madai ya Iran kwamba nchi za magharibi zinaingilia mzozo wa ndani wa Iran na kwamba hatua hiyo haikubaliki.
Akizungumza kuhusu msimamo wa Umoja wa Ulaya juu ya mzozo huo wa Iran waziri wa mambo ya nje wa Uswisi ambayo imechukua uwenyekiti wa umoja huo,Carl Bildt amesema serikali ya Tehran lazima ikomeshe matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji.Nchi za Magharibi kama vile Italia zimeshasema kwamba ziko tayari kwasaidia waandamanaji wa upinzani.Italia inasema kwamba itafungua ubalozi wake mjini Tehran kuwapokea waandamanaji waliojeruhiwa katika ghasia hizo ikishirikiana na nchi nyingine za Umoja wa Ulaya.Harakati hizo za Italia zinafuatiwa na hatua ya Uswisi ya kuataka kuangalia ikiwa nchi za Umoja huo wa Ulaya zinaweza kuandaa mpanago wa kufungua ofisi zao za kibalozi kwa ajili ya waandamanaji hao wa upinazni nchini Iran.Kansela Angela Merkel wa Ujerumani pia ametoa matamshi makali dhidi ya utawala wa Iran ambapo ametaka waliokamatwa waachiwe huru.
Leo serikali ya Ujerumani imemualika balozi wa Iran nchini humo kujieleza baada ya Tehran kuzishutumu nchi za magharibi kwamba zinaingilia kati masuala ya ndani ya jamhuri hiyo ya kiislamu.Viongozi wa Iran wamezikosoa zaidi nchi za Marekani na Uingereza pamoja na vyombo vya ahabari vya kigenia ambavyo tayari yamezuiwa kuripoti matukio ya ndani ya Iran.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar