Tampilkan postingan dengan label HABARI ZA MICHEZO. Tampilkan semua postingan
Tampilkan postingan dengan label HABARI ZA MICHEZO. Tampilkan semua postingan

Sabtu, 30 Mei 2009

What happened to Mau U?

Barcelona bingwa mpya barani Ulaya

Mabingwa wapya wa soka barani Ulaya
Barcelona mabingwa wa soka Ulaya
Jaribio la Manchester United kuweka historia ya kuwa klabu ya kwanza kutetea ubingwa wake wa Ulaya, lilikwama baada ya kuchapwa katika uwanja wa Stadio Olimpico, Rome.

Matumaini ya kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson kurudia kile alichofanya dhidi ya Chelsea mwaka jana yaliyeyuka walipofungwa na Barcelona mabao 2-0 huku mshambuliaji wa Argentinas Lionel Messi akisumbua ngome ya Manchester United.

United ilianza pambano hilo kwa kishindo kikubwa, huku dalili zikionekana za kutetea ubingwa wao, huku Cristiano Ronaldo akiisumbua ngome ya Barcelona na kuwafanya Barcelona kubabaika.

Lakini mara tu baada ya Samuel Eto'o kufunga bao la kwanza katika dakika ya 10 kipindi cha kwanza, kwa kumponyoka Nemanja Vidic, hali ya mchezo ikabadilika na Barcelona wakawa wanamiliki mchezo na kufuta matumaini ya Manchester United kuongeza kikombe kingine zaidi ya kile cha Ligi Kuu ya England.

Barcelona walionekana kumiliki kila idara na hasa sehemu ya katikati ambapo Andres Iniesta na Xavi wakitawa.

Ilikuwa ni Barcelona tena walioweza kupachika bao la pili kupitia kwa Lionel Messi kwa kichwa baada ya kuwekewa mpira wa juu na Xavi, katika dakika ya 25 ya kipindi cha pili.

Kwa ushindi huo sasa Barcelona wamejiongezea kikombe cha tatu msimu huu baada ya kushinda ligi ya Uhispania- La Liga pamoja na kombe la Hispania.

Mohammed Dewji amkana Juma Kaseja

Mohammed Dewji amkana Juma Kaseja
Kocha mpya wa African Lyon Eduardo Filipe Almeida(katikati) akitambulishwa kwa waandishi wa habari na Mkurugenzi wa timu Mohamed Dewji(kulia) katika halfa fupi jijini jana.
Na Mwandishi Wetu

AFRICAN LYON imemtambulisha kocha wake mpya Mreno Eduardo Filipe Almeida ambaye atainoa timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara huku ikisema imejitoa katika suala la kumtaka Juma Kaseja.

Akimtambulisha kocha huyo kwa waandishi wa habari jana katika ofisi zake jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu, Mohamed Dewji alisema kocha huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kufundisha klabu hiyo.

Alisema Mreno huyo alishawahi kufundisha kikosi cha vijana wa umri chini ya miaka 13 na 16 katika timu kongwe za Ureno za Benfica na Porto kabla ya kupata mkataba Hongkong. Katika hatua nyingine Dewji amekanusha madai kuwa timu hiyo imemsajili kipa wa Yanga, Juma Kaseja.

Dewji alikiri kufanya mazunguzmzo na kipa huyo lakini hawaafikiana naye kwa madai kuwa dau alilotaka lilikuwa ni kubwa mno.

Dewji alisema kuwa timu yake inahitaji kipa kijana zaidi ambaye wanaweza kumtumia zaidi ya misimu mitatu ya ligi na hivyo umri wa Kaseja pia umekuwa ni kikwazo cha wao kumhihitaji.

" Tunao vijana wengi wa umri mdogo ambao walicheza vizuri wakati wa mechi za kutafuta kupanda daraja. Tulihitaji wachezaji wachahe wenye uzoefu ili kuwapa changamoto vijana wetu wachanga na ndiyo maana tukamfuata Kaseja," alisema Dewji.

Hata hivyo Dewji hakuwa tayari kueleza Kaseji alihitaji kiasi gani ili asajiliwe na klabu hiyo ya African Lyon yenye makazi yake Mbagala wilayani Temeke.

Katika hatua nyinine Dewji alisema kuwa ujenzi wa uwanja wa kisasa katika eneo la Mbagala tayari umeshaanza katika hatua za awali na utakuwa na nyasi za bandia.

Kocha mkuu wa Simba Phiri kuhamia Yanga?

Phiri: Mimi Yanga? Acheni masihala

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amesema anaendelea kusaka wachezaji kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake, lakini ameshangazwa na habari kuwa atajiunga na Yanga na ameziita habari hizo kuwa ni masihala makubwa.

"Yanga! Kwa nini? Kwani kocha wao (Dusan Kondic) ameondoka? Nani kasema? Kila mtu anaweza kusema lake ila mimi nina mkataba na Simba na wala sijazungumza na Yanga.

Nakuhakikishia naelekeza nguvu zangu Simba na kila kitu ninafanya kwa ajili ya Simba kwa kipindi hiki,� alisema Phiri jana Ijumaa alipozungumza na Mwanaspoti kwa simu kutoka Zambia.

Phiri raia wa Zambia alisema hawezi kufanya kitu ambacho kitachanganya mipango yake; "Waambie niko Simba na hata huku ninafanya kazi za Simba," alisisitiza kocha huyo mpole.
Wakati Phiri akisema hivyo, Kocha Mkuu wa Yanga, Dusan Kondic aliiambia Mwanaspoti jana Ijumaa kuwa kama viongozi wa Yanga watakuwa wameamua hivyo, atamkaribisha Phiri.

"Suala hili wanaweza kulizungumzia viongozi, lakini ni kitu kibaya sana ambacho mtu anaweza kujitangazia tu. Mimi nipo Yanga, naendelea na kazi za Yanga kwa ajili ya msimu ujao tena kwa umakini mkubwa. Lakini kama yatatokea mabadiliko mimi ni kocha. Kukaa katika klabu kwa siku kadhaa na kuondoka si kitu kigeni," alisema raia huyo wa Serbia.
Kwa upande wa uongozi wa Yanga, Katibu Mkuu wa klabu hiyo kongwe nchini, Lucas Kisasa alisema hawana mpango wowote na Phiri.

"Tunafikiria vitu vingine kabisa, suala la kocha ni kwamba Dusan Kondic ndiye kocha mkuu wa Yanga. Naomba watendeeni haki wasomaji wenu kwa kuwaandikia habari za kweli. Kwa kifupi hatuna mpango huo," alisema Kisasa.
Mwanaspoti ilipiga mguu hadi kwa Mfadhili wa Yanga, Yusuf Manji ambaye pia alisisitiza kuwa hizo taarifa ni mpya kwake na anazisikia kwa mara ya kwanza.

"Tayari tuna Kondic ambaye ndiye kocha bora Tanzania, amefanya karibu kila kitu na Yanga wanajivunia. Timu imechukua ubingwa ikiwa na mechi mkononi, tumetoa mfungaji bora, tuna wachezaji wanatakiwa Ulaya na kwingine kama China. Hatuna mpango wa kutaka kocha mwingine,' alisema Manji.

Lakini kwa upande wa Simba kupitia mwenyekiti wake wa usajili, Kassim Dewji wamesisitiza kwamba Phiri ana mkataba na klabu hiyo na hakuna mpango wowote wa kumwachia aende Jangwani.

Taarifa ya baadhi ya vyombo vya habari jana zilisema kuwa kocha huyo anataka kujiunga na Yanga jambo ambalo lilizua mjadala sehemu mbalimbali nchini.

Kaseja, Sunguti watemwa Yanga


SIKU saba kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa mwaka mmoja, Kocha wa Yanga, Dusan Kondic amemtema rasmi kipa wake, Juma Kaseja.

Kaseja, aliyesajiliwa na Yanga kwa kitita cha dola 30,000 (Sh milioni 36) msimu uliopita ni miongoni mwa majina matano ambayo Kondic ameyapeleka kwa uongozi kuwa waachwe.

Pamoja na Kaseja, Yanga imewatema washambuliaji wake wawili, Gaudence Mwaikimba na mkongwe, Maurice Sunguti aliyeibuka mfungaji bora na kinara wa mabao misimu miwili iliyopita.

Kondic pia amewatema wachezaji wawili watoro sugu, Laurent Kabanda ambaye alikwenda kwao Congo na Credo Mwaipopo aliyetoka kwenda Sweden kabla ya kurejea miezi kadhaa iliyopita.

Habari za uhakika kutoka Yanga zinasema kuwa kikao cha juzi Alhamisi cha uongozi, kocha Kondic na mfadhili, Yusuf Manji umepitisha uamuzi huo na majina hayo matabo yatatangazwa wakati wowote kuwa wameachwa.

Habari hizo zenye uhakika ni kuwa Yanga imemuacha Kaseja baada ya Kondic raia wa Serbia kumuweka katika orodha ya wachezaji asiowahitaji tena kwa ajili ya msimu ujao na hasa baada ya kupata habari kuwa kipa wake wa Serbia, Obren Curkovic anarejea.

Kondic amefanya hivyo ikiwa ni siku chache baada ya kuiambia Mwanaspoti kuwa kipa namba moja wa Simba, Ally Mustapha 'Barthez' ni bora kuliko Kaseja.

Katika kikao hicho, Mserbia huyo aliueleza uongozi huo kwamba pamoja na ubora wa Kaseja katika mambo mengine lakini kasoro ya umbo na hasa ufupi ndio kimefanya asitake kuendelea naye.

Kondic alisema hakuwahi kumtaka Kaseja na hata msimu uliopita alitua Jangwani kutokana na siasa za Yanga na Simba, lakini halikuwa chaguo lake.

Tayari kocha huyo ameanza mipango ya kuhakikisha wanasajili kipa mwingine hapa nchini lakini ikiwa ni baada ya kurejea kwa kipa Mserbia, Obren Curkovic ambaye aliondoka nchini kwa hofu ya vitisho na kwenda kwao Serbia, baadaye Austria kufanya majaribio ambako anaelezwa ameshindwa.

Kwa upande wa Mwaikimba na Sunguti, Kondic alikieleza kikao hicho kwamba wameshindwa kuonyesha mchango wowote hata pale alipowapa nafasi ya kufanya hivyo, lakini Sunguti ikiwa ni kutokana na umri kumtupa mkono.

Kondic amekieleza kikao hicho kwamba, kitu muhimu kwa Yanga ni kufanya usajili wa wachezaji wachache tu huku akisisitiza kuwa Nurdin Bakari 'Kibajaji', Ben Mwalala na Mike Baraza hawatakwenda popote kwani anawahitaji kwa msimu ujao.

Kondic amewaweka mabeki Yusuf Hamis na Abuu Mtiro na Mkenya, George Owino katika orodha ya wachezaji watakaouzwa kwa kuwa bado wana mkataba na jeshi hilo la Jangwani.

Wengine ambao Kondic amewaweka katika orodha ya kuuzwa nje ya nchi ni Nadir Haroub 'Cannavaro' (Vancouver-Canada), Shadrack Nsajigwa (Ufaransa) na Boniface Ambani (China).

Akizungumza na Mwanaspoti jana Ijumaa, Katibu Mkuu wa Yanga, Lucas Kisasa alikiri kuwa na kikao hicho na kusema kilihusu mambo ya Yanga na si kwa ajili ya taarifa kwenye vyombo vya habari.

"Kweli tumekutana, lakini ilihusu mambo ya Yanga na tusingependa yazungumziwe hadharani. Tukiwa tayari tutawaita na kuwaeleza," alisema Kisasa.

Lakini kwa upande wa Kondic alisisitiza kwamba, usajili mpya hautakuwa na mabadiliko makubwa kama wengi wanavyofikiri.

"Kweli tulikutana, lakini ni mambo yetu ya ndani ukiwamo usajili. Tumejadili mengi ukiwamo usajili, kweli kuna ambao wataachwa, wengine watauzwa na wengine tunawasiliana nao kwa ajili ya usajili.

Ila hatutakuwa na mabadiliko makubwa kwa kuwa tuna wachezaji wa kutosha na kumbuka kuna Joseph Shokokoti na John Njoroge ambao wako Tusker kwa mkopo. Pia tuna chipukizi wetu ambao tuliwapandisha mwaka jana. Hivyo ni sehemu chache tutaongeza.

Mwanaspoti ilimsaka mfadhili Mkuu wa Yanga, Yusuf Manji ambaye alimsajili Kaseja mwaka jana na kuweka rekodi ya usajili kwa wachezaji wandani ikiwa ni pamoja na kumpa mshahara wa Sh milioni moja ambaye alisema suala hilo ameachiwa Kondic.

"Tunaweza kusajili mchezaji yeyote kama anaweza kuisaidia Yanga hata kama itakuwa Sh milioni 50, lakini kocha ndiye anatuelekeza wapi twende kwenye hili. Hivyo kama kumbakiza au kumuacha mchezaji ni suala la kocha," alisema Manji.

Akizungumza jana kuhusu hilo, Kaseja alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kirefu kwa kuwa ameelekeza nguvu zake kwenye mechi ya leo Jumamosi ya fainali ya Kombe la Taifa.

"Mkataba haujaisha nitakuwa nimeachwa vipi, hapo sielewi lakini naomba mnipe muda kwa kuwa nikiamua kuzungumza nitakuwa na mengi tu. Ila naelekeza nguvu zangu katika mechi ya kesho (leo Jumamosi) ya Taifa Cup baada ya hapo naweza kuzungumza vizuri," alisema Kaseja ambaye ndiye kipa bora namba moja nchini.

Minggu, 10 Mei 2009

Mechi za Simba na Yanga kuna nini ndani yake?

Kaduguda atoboa siri kubwa
Haruna Moshi 'Boban' wa Simba ambae imedaiwa yupo kwenye orodha mpya ya kocha wa Yanga, Dusan Kondic ingawa duru za ndani ya Simba zinadai kuwa ni ngumu mno mchezaji huyo kung'oka Msimbazi na kwenda Yanga kutokana na wadhamini na washauri wake wakubwa.
Na Michael Momburi


MWINA Kaduguda amedai kuwa hakuna kiongozi yoyote wa timu hizo ambae anapenda kusikia mechi ya watani ya jadi.

Katibu huyo mkuu wa kuchaguliwa wa Simba, alisema jijini Dar es Salaam kuwa licha ya kwamba viongozi hutamba hadharani lakini moyoni huumia sana.

"Mechi inayokutanisha Simba na Yanga hakuna kiongozi yoyote wa hizo timu anayeipanda, ni mechi ngumu sana na yenye mambo mazito," alidokeza Kaduguda.

"Kwanza gharama ni nyingi mno tofauti na watu wa kawaida wanavyofikiria, halafu kwa viongozi hatutulii, mpaka mkeo nyumbani anakuwa hana raha.

"Kwa mfano mimi muda wangu wa kulala kwa wiki ambayo tunafanya maandalizi ya hiyo mechi siwezi kulala chini ya saa 6 usiku.

"Hata nikilala lazima utasikia kiongozi fulani kakuamsha muda fulani kuashiria kwamba kuna mambo yakufanya au hata wazee, yaani ni mechi ngumu sana ambayo hakuna kiongozi wa timu yoyote kati ya hizo mbili anayeipenda."

Mshambuliaji wa Yanga, Boniface Ambani alitamka hivikaribuni kwamba anashangazwa jinsi viongozi wa Yanga walivyokuwa wakijiandaa na mechi dhidi ya Simba tofauti na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Jumat, 27 Maret 2009

Yanga yatwaa ubingwa na mechi 5 mkononi

WAKATI kipute cha Ligi Kuu Tanzania Bara kikiwa inaelekea ukingoni huku kila timu ikiwa imebakiza mechi tano, tayari Yanga imeshatwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo, Prisons ya Mbeya imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta baada ya kuichapa Kagera Sugar 2-1.

Katika mchezo huo ambao jana ulihailishwa kutokana na mvua nyingi iliyonyesha jijini Mbeya na kusababisha uwanja wa Sokoine kujaa maji, ulishudia wenyeji Prisons ikipata bao la mapema katika dakika ya 7 lililofungwa na Yona Ndabila aliyeunganisha vema pasi ya Osward Morris.

Kagera Sugar wenye hamu ya kubwa ya kuchukua nafasi ya pili walijirekebisha katika kipindi cha pili na kupata bao la kusawazisha mwanzoni kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Shija Hassan baada ya kuchezewa vibaya kwenye eneo la hatari.
Maafande hao wa magereza waliandika bao la ushindi kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 64 iliyofungwa na Ismail Suma kwa ushindi huo sasa Prisons imefikisha pointi 25 ikiwa nyuma kwa pointi mbili kwa Simba.

Simba ina kazi ya ziada kuhakikisha inashinda mechi zake zilizosalia ili kubaki nafasi ya pili huku ikiiombea dua baya Kagera Sugar.

Mabingwa wa Tanzania Bara, ambao wamekuwa wakitumia staili yao ya 4-4-2 wameendelea kuwawashia indiketa wapinzani wao Simba ambao waliukosa ubingwa huo msimu uliopita na kushikiria nafasi ya tatu huku nafasi ya pili ambayo ilichukuliwa na Tanzania Prisons ya Mbeya.

Wakati Yanga wakishekelea kutangaza ubingwa mapema, timu za Polisi Dodoma, Villa Squad na Moro United zinapumulia kwenye mashine kutokana na timu hizo kuwa kwenye hatari ya kushuka daraja.

Katika msimamo wa ligi, Polisi Dodoma inashika mkia baada ya kucheza mechi 17 na imeshinda moja, imetoka sare mara tisa na imepoteza saba na ina pointi 12.

Villa Squad wamecheza mechi 16 wameshinda nne, wamedroo mbili na kupoteza 10 wana pointi 14 wakati Moro United ina pointi 15 ikiwa imepishana pointi moja na Polisi Morogoro, ambayo ina pointi 16.

Mechi zote zinaifanya ligi kuwa ngumu kutokana na timu zote kupambana kufa na kupona kuhakikisha zinabaki kwenye Ligi Kuu na timu za Simba, Mtibwa na Kagera wakiwania zikiwania nafasi ya kusaka Kombe la Shirikisho.

Tayari timu za Majimaji, Manyema na African Lyon zimepanda daraja na timu tatu zitashuka daraja ligi kuu.

Wafungaji waongoza kwa ufungaji msimu huu ni Boniface Ambani wa Yanga mwenye mabao (14) akifuatiewa na Hessen Bunu (JKT Ruvu) (10), Said Dilunga wa Toto Africa (8), Musa Mgosi wa Simba (7).

Rabu, 25 Maret 2009

Yanga inatisha, yatwaa ubingwa kabla ya ligi kuisha licha ya TFF kuwanyang'anya point 2....

Na Tedy Mwarabu

Mabigwa wa soka Tanzania bara 2008/9 Yanga wakipongezana. Wamefanikiwa kutangaza ubingwa kabla ligi haijaisha.

BAO la mwaka la kipa Juma Kaseja lilitosha kuweka historia mpya kwa kuipa Yanga ubingwa wa 22 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza huku Azam ikiichapa 6-2 Villa Squad jijini Dar es Salaam.

Yanga iliyokuwa ikihitaji pointi tatu ili kutangazwa mabingwa kwa msimu wa 2008/'09, iliandika bao lake la kwanza katika dakika ya 21 lililofungwa na Kaseja aliyetumia vizuri udhaifu wa mwenzake, Abdallah Msafiri wa Toto Africa na kuachia mkwaju ambao ulidunda na kutinga nyavuni.

Awali, Kaseja alidaka na kupiga mpira mrefu wa juu uliokwenda moja kwa moja wavuni, dakika tisa baadaye Hussein Sued aliisawazishia Toto Afrika kabla ya Mike Baraza kufunga bao la pili na ushindi kwa mabingwa hao.

Katika mchezo huo ulioshuhudia timu hizo zikikosa penalti kila moja, mshambuliaji MkenyaMike Baraza wa Yanga alikosa penalti dakika ya 18 kipindi cha kwanza , naye Said Dilunga alipoteza nafasi ya pekee ya kuisawazishia Toto wakati mkwaju wake wa penalti ulipoishia mkononi mwa Kaseja, dakika ya 62.

Naye Sweetbert Lukonge anaripoti kutoka Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuwa jahazi la Villa Squad limezidi kuzama baada ya kukubali kipigo cha mabao 6-2 kutoka kwa Azam FC.

Mshambuliaji Nsa Job ndiye aliyekuwa mwiba mkali kwa ngome ya Villa kwa kupachika mabao matano peke yake na kuzawadiwa mpira akimwachia mchezaji wa kimataifa wa Uganda, Danny Wagaluka akihitimisha karamu hiyo ya mabao kwa bao la sita.

Katika mchezo huo uliokuwa na raha ya aina yake, ulishuhudia mabao manne yakifungwa ndani ya dakika nane za mchezo huo, Azam ilipata mabao kupitia kwa Nsa Job, dakika ya 16 na 25 wakati Villa walisawazisha kupitia kwao, Juhudi Samwel 19 na Lewede Dayton (24),kipindi cha kwanza na kufanya matokeo kuwa 2-2 hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kilikuwa kibaya zaidi kwa Villa baada ya Nsa Job kufunga bao la tatu, nne na sita katika dakika ya 51,74 na 88, huku Mganda Wagaluka akipachika bao la tano (85).

Katika kile kilichoonekana kama kuchanganyikiwa na kipigo, mchezaji wa Villa , Launt Bagia alikosa penalti mwisho mwa mchezo, dakika ya 90 iliyopanguliwa na kipa wa Azam, Vladimir Niyonkuru.

Kutoka Mbeya, Brandy Nelson anaripoti kuwa mvua kubwa iliyokuwa inanyesha mjini humo ilisababisha mwamuzi Dominick Nyamsana kutoka Dodoma kuusimamisha mchezo huo katika dakika ya 28.

Mchezo huo baina ya Prisons na Kagera Sugar ulikuwa ukichezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa huku zikiwa zimefungana bao 1-1.

Akizungumzia kuahirishwa kwa mechi hiyo mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoani Mbeya, Festo Nkemwa alisema mvua kubwa iliyojaza maji uwanjani ndiyo sababu ya kuahirishwa kwake.

Nkemwa alisema mvua hiyo ilisababisha wachezaji wa timu hizo kuanguka na kuweza kuhatarisha afya zao.

Naye mwamuzi Nyamsana alisema hadi uamuzi huo ulifikiwa kutokana na hali ya uwanja kutofaa tena kwa mchezo huo.

Mabao hayo, Prisons yalifungwa na Shaban Mtupa dakika ya nne, Haruna Hassan wa Kagera akasawazisha, dakika ya 18.

Senin, 09 Maret 2009

Leo ni Leo uwanja wa Taifa

Vancouver kuwavaa Yanga leo

champion
Vancouver kuwavaa  Yanga leo
Na Julius Kihampa

MABINGWA wa Ligi Daraja la Kwanza ya Marekani ya Kaskazini, Vancouver Whitecaps FC, leo wanashuka katika Uwanja Mkuu wa Taifa jijini Dar es Salaam kukipiga na mabingwa wa hapa, Yanga kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki...

wAFUNGWA SASA KURUHUSIWA KUFANYA MAPENZI GEREZANI

utaruhusu wanandoa kujamiiana itakapowezekana
Gloria Tesha
Daily News; Sunday,March 08, 2009 @18:39
Habari nyingine
  • Kilosa yaanzisha matumizi ya vyandarua
  • Mafisadi wabanwa kuwania ubunge
  • Magereza:Tutaruhusu wanandoa kujamiiana itakapowezekana
  • Lori lapamia basi, watano wafa
  • Viongozi wenye majungu Mbeya waonywa
  • Shahada ya Ubaharia sasa kutolewa nchini
  • Shelys yaipa dawa Ocean Road
  • Taharuki yazuka vituo vya LUKU
  • Wanafunzi washinda rufaa Bodi ya Mikopo
  • Wafanyakazi TSN wasaidia yatima
  • Magereza inafanyia kazi mapendekezo ya wataalamu iliowatuma nje, ya kuangalia uwezekano wa wafungwa kupata haki ya ndoa zao wakati wanatumikia vifungo vyao.

    Hayo yalielezwa na Kamishna Mkuu wa Magereza, Augustino Nanyaro wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwavisha nishani askari 44 wa Magereza mwishoni mwa wiki Dar es Salaam.

    Alisema upitiaji wa mapendekezo hayo unachukua muda na hata utekelezaji wake utategemea mambo mengi, yakiwamo ya uwezo wa kiuchumi. Kama utaratibu huo utaanza kutumika, wafungwa watakaokuwa na vigezo stahili vikiwamo vyeti vya ndoa, watapaswa kutumia maeneo yenye mazingira tofauti na gerezani lakini si nje ya gereza.

    “Wazo lipo lakini uwezo wa kutekeleza ni kitu kingine, tumeyaona haya kwa wenzetu katika kutembea kwetu na tumedhani ni jambo zuri kufanyika hapa nchini, kufungwa si kwamba hustahili mambo yote,” alisema Kamishna Mkuu wa Magereza, Augustino Nanyaro.

    Alisema hata hivyo utekelezaji huo hautahusu kila mfungwa, bali ni wale watakaokidhi vigezo ikiwamo nidhamu na heshima ya hali ya juu itakayoruhusu kukaa na familia yake (mke au mume) na kujamiiana. Alisema hata hivyo, utekelezaji wake utachukua muda mrefu kulingana na hali ya uchumi itakavyoruhusu.

    Nanyaro alisema mpango huo utakuwa na faida kwa vizazi vijavyo baada ya mambo ya msingi kama kupunguza msongamano yatakapopatiwa ufumbuzi wa kudumu. Kuhusu msongamano magerezani, alisema ziara ya Rais Jakaya Kikwete ya kutembelea magereza aliyoifanya zaidi ya mwaka mmoja uliopita imeanza kuzaa matunda, kwani msongamano umepungua na kasi ya kusikiliza kesi mahakamani imeongezeka tofauti na awali.

    “Ushirikiano wa mahakama, polisi na magereza umeongezeka baada ya ziara ya rais na maboresho yamefanyika na yanaendelea kufanyika magerezani, tumejenga mabweni mawili ya wafungwa gereza la Ukonga na ukarabati wa mabweni unaendelea huko Tanga, Mbarali, Lilongwe na maeneo mengine,” alisema Kamishna huyo.

    Aidha kuhusu idadi ya wafungwa waliohukumiwa kunyongwa na namna wanavyochangia msongamano magerezani kutokana na kukaa muda mrefu gerezani bila hukumu yao kutekelezwa, alisema wafungwa hao hawazidi 400 na idadi hiyo haichangii kwa namna yoyote msongamano.

    Kuhusu mazingira na namna Magereza ilivyojipanga kutumia nishati mbadala na gesi asilia kuepusha uharibifu wa mazingira kutokana na matumizi ya kuni, alikiri kuwa wanachangia uharibifu wa mazingira na kwamba miradi mbalimbali ya gesi mbadala na asilia inafanyika katika magereza.

    Alisema maofisa kadhaa wa magereza walipelekwa Rwanda kupata utaalamu wa kutengeneza nishati kutokana na kinyesi katika gereza kuu la nchi hiyo na sasa majaribio yanafanyika katika gereza la Ukonga na yatakamilika Mei mwaka huu. “Walipata mafunzo kwa gereza la wafungwa 11,000 ambalo wanatumia nishati itokanayo na kinyesi cha mahabusu.

    Ukonga mradi wa majaribio unafanyika kupitia mtaalamu yule yule wa Rwanda na itakapokamilika na kuonyesha mafanikio, tutaitumia kwa magereza yote 12 makuu,” alisema. Aliyataja magereza mengine yenye miradi ya gesi na nishati mbadala kuwa ni Ruanda, Mbeya wanakotumia mkaa wa mawe, Keko, Dar es Salaam wanakotumia gesi asilia ya Songo Songo kwa majaribio na Chuo cha Magereza Ukonga.

    Katika hatua nyingine, Nanyaro alisema mchakato wa kupanda miti kwa kushirikiana na wafadhili, wizara mbalimbali, mashirika ya nje na ndani ya nchi unaendelea katika maeneo mbalimbali ambapo tayari miti zaidi ya milioni tatu imepandwa. Maeneo hayo ni pamoja na Bariadi mkoani Shinyanga ambapo zaidi ya ekari 1,200 zimehusika.

    mAXIMO KOCHA WA TIMU YA TAIFA ADAIWA KUUA WACHEZAJI WOTE WA YANGA

    Kondic: Maximo umeua wachezaji wangu wote
    Kocha wa Yanga Kondic Dusan(Kulia) akiwa na msaidizi wake, Spaso Solokovisk. Kondic ambae timu yake inacheza na Al- Ahly wikiendi ijayo katika mechi ya Ligi ya Mabingwa amelalamika kwamba wachezaji wake wote zaidi ya saba waliokuwa kwenye timu ya Taifa ni wagonjwa na hajui la kufanya.
    Na Michael Momburi

    KOCHA wa Yanga, Kondic Dusan amesema hana raha kwani wachezaji wote waliokuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars wapo katika hali mbaya.

    Ingawa hakumtaja Kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo, Kondic amekuwa akilalamika mara kwa mara wachezaji wake wengi kuitwa kwenye kikosi cha Stars na kuingilia ratiba ya klabu hiyo.

    Yanga inajiandaa na mechi ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya Misri ambayo wenyeji wametangaza rasmi kwamba itachezwa jijini Cairo Jumapili ya wikiendi ijayo.

    Kondic aliiambia Mwanaspoti mazoezini kwenye Uwanja wa Uhuru Alhamisi usiku, kwamba, hali ya wachezaji wote waliokuwemo kwenye kikosi cha Stars si nzuri na inamuweka katika wakati mgumu.

    Wachezaji wa Yanga waliokuwa na kikosi cha Stars kwenye fainali za CHAN ni Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, Kigi Makassi, Godfrey Bonny, Nadir Haroub 'Cannavaro', Athuman Idd, Amir Maftah, Mrisho Ngassa, Jerry Tegete na Abdi Kassim.

    "Sina raha kabisa, usinione ninavyozungumza na wewe. Niko kwenye wakati mgumu sana wachezaji wangu tegemeo waliokuwa safarini wamerudi lakini wote ni matatizo," alisema Kondic kwa hasira kocha huyo wa Serbia.

    "Kila mmoja ni mgonjwa hakuna mzima hata mmoja, halafu angalia nina siku ngapi kabla ya kuingia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly tena ugenini.

    "Ngassa na Cannavaro hawapo mazoezini matatizo ni hayo hayo kwamba hawako vizuri na wana majeraha madogo madogo ndio maana nimewaruhusu wapumzike.

    "Hao wengine umewaona hapo wamekuja na wanafanya mazoezi lakini kila mmoja ana tatizo; mara msuli unauma, mara goti! Hakuna hata mmoja ambaye yuko kamili, yaani hapa inabidi kufanya kazi ya ziada sana na kutegemea ripoti ya daktari.

    "Vinginevyo hali itakuwa ngumu sana halafu muda tulionao ni mfupi mno. Sina raha kabisa, najaribu kufanya kazi kadri inavyowezekana niangalie hali za hawa wachezaji zitakuwaje katika siku zilizobaki,"alisisitiza Kondic ambaye alisema mambo mengine yanakwenda vizuri mazoezini.

    Katika hatua nyingine, Kondic alisema kwamba kiungo wake, Athuman Idd 'Chuji' amemwambia kwamba hana tofauti zozote na kocha Marcio Maximo kama inavyoripotiwa.

    "Nimezungumza naye kaniambia kwamba hana matatizo yoyote na Maximo wala Taifa Stars na mimi nadhani kama kungekuwa na tatizo Maximo angeshaniambia lakini huyo kocha hajanieleza au kunipigia simu,"alisisitiza Kondic kwa kifupi na kusisitiza kwamba labda abanwe mwenyewe Idd anaweza kusema zaidi.

    Lakini hata hivyo mchezaji huyo ambaye amejitoa kwenye timu ya Taifa amekuwa mgumu kutoa tamko.

    Katika mazoezi ya juzi jioni ambayo wachezaji Ngassa na Cannavaro ndio pekee waliokosekana, mabingwa hao watetezi walikuwa wakichezea mipira uwanjani kwa zaidi ya saa mbili na baadaye wakatumia dakika chache kunyoosha viungo kabla ya kupanda gari na kuelekea kambini kwenye Hoteli ya Tamal iliyoko karibu na Mwenge karibu na ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar es Salaam.

    Timu hiyo imetimuliwa kwenye Hoteli ya Lamada baada ya kushindwa kulipa fedha wanazodaiwa.

    Rabu, 04 Februari 2009

    YANGA NOMA. ILIMPA MTU BAO 8. KIPA AKAA CHINI...

    Kipa wa Etoile d'Or Mirontsy ya Comoro alipoamua kukaa chini baada ya Yanga kupachika bao la nane katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa kwenye uwanja wa Taifa wikiendi iliyopita. Yanga ilishinda 8-1 huku mshambuliaji wake Mkenya, Boniface Ambani akipachika mabao manne peke yake.

    WAKATI mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na matumaini makubwa kushinda mechi ya leo dhidi ya Etoile d�Or ya Comoro, wapinzani wao wametamba ngoma itakuwa nzito.

    Kocha Mkuu wa Yanga, Dusan Kondic raia wa Serbia ameonyesha kupunguza kasi ya mazoezi ya nguvu hali inayoonyesha ameridhika na fiziki ya kikosi chake na badala yake amelalia zaidi katika masuala ya kiufundi.

    Lakini Kocha Mkuu wa Etoile d�Or, Nasurdine Maanrouf alianza na mazoezi makali baada ya kutua nchini na jana alipanga wachezaji wake wafanye mazoezi ya taribu kabla ya kupumzika leo asubuhi wakisubiri �mtanange� huo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


    Kondic amesema kwa ufupi, "Siwezi kudharau mechi kama wengi wanavyosema, nataka kushinda. Tukipata ushindi mzuri, tutajihakikishia kusonga mbele mapema, maana yake tutaanza kuangalia zaidi raundi inayofuata,"alisema.

    Lakini Maanrouf amesema, "Naijua Yanga ingawa kwa kuisikia, umaarufu wake kwa Comoro pale ulikuja baada ya kuitoa AJSM, ambayo ni moja ya timu bora kule kwetu. Tumekuja tukiwa na tahadhari zote."

    Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo jana walikuwa wakilanda katika mitaa ya Kariakoo huku wakishangaa mitaa na majengo marefu na baadhi ya mashabiki wakiwakejeli na kuwaonyeshea vidole vya mabao matano. Wakati huo wapinzani wao Yanga wakiwa wamepumzika kwenye kambi yao katika hoteli ya Lamada.


    Mshambuliaji tegemeo wa Yanga, Boniface Ambani akipasha msuli tayari kuingia uwanjani kufanya vitu vyake. Yanga ambayo ndio timu pekee Afrika Mashariki yenye kipa mzungu inaanza kampeni zake za Ligi ya Mabingwa leo Jumamosi kwa kuivaa Etoile d�Or ya Comoro Jijini Dar es Salaam,


    Naye mshambuliaji nyota wa Yanga, Boniface Ambani alisema yuko katika hali nzuri zaidi, "Nilikuwa nahofia kupiga mashuti, lakini mechi ya ligi iliyopita niliachia shuti na kuona sijajitonesha. Mechi ya Wacomoro nitacheza kwa raha na kujiamini zaidi.

    Wakati Ambani anasisitiza kutaka kupachika mabao, mabeki, Shadrack Nsajigwa, Nadir Haroub �Canavaro� na kiungo Athuman Idd �Chuji� wamesisitiza kutaka kupata ushindi mnono.

    Uchunguzi wa Mwanaspoti unaonyesha Yanga ina kila sababu ya kuibuka na ushindi mnono ingawa Wacomoro hao watacheza kwa kujihami muda mwingi ili kuzuia kurejea kwao na mvua ya mabao kwa kuwa wameonyesha uoga wa wazi wazi wa kukutana na Jangwani.

    Timu hiyo ni changa katika michuano ya kimataifa kwani mara nyingi zimekuwa zikishiriki timu za AJSM, iliyobamizwa mabao 5-1 na Yanga, nyingine ni Etoile de Sud na Coin Nord.

    Katika mazoezi yao, wameonyesha zaidi kucheza mchezo wa kujihami zaidi huku wakijifunza kushambulia kwa kushitukiza na kufunga kwa mipira ya krosi.

    Iwapo Yanga itavuka, katika hatua hiyo itakutana na mabingwa watetezi wa Afrika, Al Ahly inayoongozwa na kiungo mahiri na mchezaji bora wa mwaka 2008 wa BBC, Mohammed Aboutrika.

    Timu 42 zinashiriki katika hatua hiyo ya Ligi ya Mabingwa wakiwamo mabingwa wa Zanzibar, Miembeni, ambao wamefunga safari kwenda kuivaa Mwonomotapa ya Zimbabwe.

    Huenda Kondic akapanga kikosi chake kama ifuatavyo: Kaseja au Obren, Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, George Owino Haroub Cannavaro, Geofrey Bonny, Mrisho Ngassa, Athuman Idd, Boniface Ambani, Ben Mwalala na Shamte Ally.

    Wakati Yanga ni leo, kesho Jumapili kwenye uwanja huo huo ni zamu ya Prisons ya Mbeya, ambayo inaikaribisha Khalij Sert ya Libya katika mechi ya Shirikisho.

    Wachezaji wamemueleza mwandishi wetu, Michael Momburi kwamba wanachotaka ni kuibuka na ushindi kesho na kuliwakilisha vema taifa.

    "Hakuna kukata tamaa hili ni soka na ndio maana tunajiandaa, kila kitu kipo sawa kufanya vibaya kwenye mechi za ligi haimaanishi kwamba hata kimataifa itakuwa hivyo,"alisema mshambuliaji Oswald Morris.

    "Mpira ndivyo ulivyo, tutajitahidi kurekebisha makosa hao Walibya hatuwajui lakini tutapambana nao uwanjani na tunaamini matokeo yatakuwa mazuri, tutashangaza."

    Kocha wa timu hiyo, James Nestory alisema kwamba kikosi chake kimejipanga vizuri na hawana mchecheto wowote na wageni.

    Prisons imekuwa na mwenendo usioridhisha tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara lakini wachezaji wake wamesema hiyo haijalishi katika mchezo wa kesho wala haina nafasi.

    Imepoteza mechi tatu kwa timu za Dar es Salaam, yaani Yanga, Simba na Villa Squad, ambayo mzunguko wa kwanza ilionekana 'wagawa pointi'.

    Kikosi cha Mundu ndio wawakilishi wa Zanzibar katika michuano hiyo na inakutana na wenyeji wake, Red Arrows ya Zambia.

    Selasa, 03 Februari 2009

    TANZANIA KUJENGWA BARABARA KAMA HIVI..

    Maeneo ya kujenga barabara za juu Dar yatajwa Bungeni Na mwandishi wetu toka DODOM


    SERIKALI imelihakikishia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba mpango wa kujenga barabara za juu (fly over) kwenye makutano mbalimbali jijini Dar es Salaam unaendelea vizuri.

    Naibu Waziri wa Miundombinu , Hezekiel Chibulunje aliliambia bunge jana mjini hapa kuwa, maandalizi yote ya awali yamekamilika, na kwamba kinachosubiriwa ni kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

    Alisema hata agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa hivi karibuni jijini Dar es Salaam litakwenda sambamba na ujenzi wa barabara zingine ndani ya jiji.

    Alisema kazi ya awali, ikiwemo michoro tayari imekwishanza sambamba na kuwekwa kwa alama katika maeneo husika.

    Chibulunje alisema Shirika la Ushirikiano la Japani( JICA) liliisaidia Serikali kwa kufanya uchunguzi wa namna ya kutengeneza mpango wa usafiri jijini(City Transport Master Plan) na kwamba uchunguzi huo ulipendekeza baadhi ya makutano ya barabara jijini yawe na barabara za juu.

    Aliyataja makutano ya barabara yaliyopendekezwa kuwa na barabara za juu kuwa ni makutano ya Ubungo, Magomeni, Jangwani(Fire), kamata, Tazara na makutano ya Nyerere na Kawawa (Chang’ombe) ambapo alibainisha kuwa kwa sasa serikali inapitia ushauri huo.

    Kuhusu barabara za katikati ya Jiji , Naibu Waziri, alisema Serikali imetenga Sh 20 bilioni kwa ajili ya kuzijenga kwa kiwango cha lami ili kupunguza msongamano wa magari na kuwezesha kuwa na ubora unaotakiwa.

    Alizitaja barabara zinazohusika kuwa ni pamoja na barabara ya Kigogo-Jangwani-Jengo la Club ya Yanga (km.9.6), Tabata-Dampo-Kigogo, Ubungo-Maziwa-External na Old Bagamoyo (Morocco-JKT Mlalakuwa).

    Nyingine ni TPDC, Mbezi (Morogoro road-Malamba mawili-Kinyelezi-Banana, Jet mwisho,Tangi bovu-Goba, Kimara Baruti-Msewe- Changanyikeni na barabara ya Kimara –Kirungule-External (Mandela) ambazo alisema kuwa zote ziko katika hatua mbalimbali za usanifu wa kina kwa ajili ya kuanza ujenzi.

    Alikuwa akijibu swali la Charles Keenja (Ubungo CCM) aliyetaka kujua ni nini kinasababisha kero ya msongamano wa magari katika barabara ya Ubungo na nini ufumbuzi wa jambo hili na lini.

    Keenja pia alitaka kujua mipango ya Serikali kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam hususani kwenye makutano ya barabara za katikati ya Jiji.

    Hata hivyo, Naibu Waziri alitoa sababu nyingine kuwa msongamano huo unatokana na idadi kubwa ya magari ya watu binafsi hali inayotokana na kipato cha Mtanzania kukua na kuwezesha watu wengi kumiliki magari tofauti na ilivyokuwa mwanzoni mwa miaka ya 1990.

    Alisema mikakati itakayosaidia kupunguza msongamano huo ni pamoja na mabasi yaendayo kasi na upanuzi wa barabara muhimu kama vile Sam Nujoma,barabara za Kilwa na Mandela ambazo shughuri zake zinaendelea.

    Minggu, 18 Januari 2009

    YANGA YAUA.........

    YANGA ya Dar es Salaam imeendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kuifunga JKT Ruvu bao 1-0 katika mchezo mkali wa ushindani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Ushindi huo umeifanya Yanga kukaribia utetezi wa ubingwa wake pamoja na kujichimbia kileleni kwa kufikisha pointi 36.

    JKT Ruvu imepoteza mechi zote mbili kwa Yanga, kwani katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ilichapwa mabao 2-1.

    Mchezo wa jana ulikuwa wa mashambulizi ya hapa na pale, na Yanga walilifikia lango la wapinzani wao katika dakika za 15 na 30 lakini Jerry Tegete na Boniface Ambani mashuti yao hayakulenga lango.

    Kipa wa JKT, Abdallah Ngachimwa alisimama imara na kuokoa shuti la Ambani katika dakika ya 22 kabla ya Kessy Muhsin kupiga shuti la umbali wa mita 30 lililodakwa kifundi na Juma Kaseja.

    Kipindi cha pili, Yanga waliongeza kasi ya mashambulizi na katika dakika ya 67, Shamte Ally aliipatia bao kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi ya Mrisho Ngassa.

    Shamte alifunga bao hilo baada ya kuingia dakika ya 65 kuchukua nafasi ya Ambani.

    Yanga iliendelea kushambulia na katika dakika za 55 na 63 walikosa mabao mfululizo kupitia kwa Tegete kabla ya Mashaka Maliwa wa JKT naye kukosa bao akiwa na Kaseja katika dakika ya 77.

    Kocha wa Yanga, Dusan Kondic alisema timu yake imekosa umakini kutokana na wachezaji wake kutokaa pamoja muda mrefu. Hata hivyo aliwapongeza kwa ushindi.

    Akizungumzia mchezo huo, kocha wa JKT Ruvu, Charles Kilinda alisema ngome kukosa umakini ndiyo chanzo cha wao kufungwa. Hata hivyo alilalamikia maamuzi ya Kazi, kuwa hakuwa makini.

    Naye Dorice Malyaga anaripoti kuwa Mtibwa Sugar imeichapa Kagera Sugar mabao 2-1 katika mchezo wa ligi hiyo kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani.

    Mabao ya Mtibwa yaliwekwa kimiani na Rashid Gumbo katika dakika 20 na Abdallah Juma katika dakika 89 baada ya kuunganisha mpira wa kona wa Yahaya Akilimali.

    Bao pekee la Kagera lilifungwa na Paul Kabange katika dakika ya 25.

    Kamis, 18 Desember 2008

    Tenga amgaragaza Malinzi


    Na Jumanne Khasim
    Daily News; Monday,December 15, 2008 @12:20

    Habari nyingine
  • Malkia wa Afrika Mashariki kupatikana leo
  • Flamingo yapigwa jeki
  • Mbilinyi bingwa wa Fiddle
  • Redio, runinga zatakiwa kuacha kuwanyonya wasanii
  • Mbio za wazi kufanyika Dar
  • Wasanii waingiza 16.5m/-
  • Zambia yaalikwa Chalenji
  • 70 kuchuana katika gofu leo
  • Laibon FC bingwa Longido
  • Filamu, tamthiliya zinapotosha maadili
  • Rais wa Shirikisho la Soka Leodegar Tenga ametetea nafasi yake kwa kumbwaga mpinzani wake Jamal Malinzi katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana Dar es Salaam.


    Katika uchaguzi huo uliofanyika jana kwenye ukumbi wa NSSF waterfront, Tenga alitangazwa mshindi kwa kupata kura 68 dhidi ya kura 39 za Malinzi ambaye alirejeshwa kuwania nafasi hiyo baada ya kushinda rufaa kutokana na kuenguliwa na kamati ya uchaguzi.

    Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa Tenga alisema " nawashukuru wajumbe kwa kunipa nafasi nyingine ya kumalizia kazi niliyoianza.'Pia alimuhakikishia Mwakilishi wa wa Shirikisho la Soka la Taifa (FIFA) kwenye uchaguzi huo Ashford Mamelodi kuwa kipindi cha miaka mnne ijayo kitakuwa cha kuendeleza maendeleo yaliyokwishafikiwa.

    Nate Malinzi pamoja na kukubali kushindwa alimuomba Tenga kutokuweka kisasi kwa wale ambao hawakumpigia kura jambo ambalo Tenga alimhakikishia halitakuwapo.Aidha Malinzi aliahidi kumkabidhi ilani yake ya uchaguzi ambayo itakuwa changamoto katika utendaji wake wa kazi.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Henry Tandau alimtangaza athumani Nyamlani kuwa mshindi wa nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, baada ya kujikusanyia kura 65 kati ya kura 107 zilizopigwa na kura mbili kuharibika. Mwalusako alipata kura 39 na Ali Mwanakatwe aliambulia kura moja.

    Katika nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais wa TFF ambaye anawakilisha klabu za Ligi Kuu, nafasi hiyo ilikwenda kwa mgombea Ramadhan Nassib aliyemwangusha mpinzani wake wa karibu Damas Ndumbalo aliyepata kura 45.

    Nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji imechukuliwa na wallace Karia ambaye ni mpinzani wake Abduk Sauko aliyepata kura 26 huku kura moja ikiharibika. Wajumbe wengine wa kamati ya utendaji kupitia kanda 11 za soka ni kama ifuatavyo: Amri Roshan ametetea nafasi yake katika kanda ya Kagera na Shinyanga kwa kumshinda Mbasha Masha kwa kura 88 kwa 19.

    kanda ya pili inayojumuisha mikoa ya Mara na Mwanza Samuel Nyalla ambayye alikuwa mgombea pekeealipata kura 73, kura 33 za hapana wakati kura tatu ziliharibika na kwa upande wa kanda ya Manyara na Arusha, Khafani Mgonja aliibuka kidedea kwa kupata kura 60 dhidi ya 45 za mpinzani wake Charles Mugodo, kura mbili ziliharibika kwenye uchanguzi huo.

    kanda ya Kigoma na Tabora, Msafiri Mgoyi alimbwaga Ismail rage kwa kura 75 dhidi ya 32. Akizungumza na alimbwaga Ismail Rage kwa kura 75 dhidi ya 32. Akizungumza na gazeti hili, Rage alisema kuwa: “ Nilikuwa naumwa na jana (juzi) jioni ndipo niliporuhusiwa kutoka hospitali lakini leo (jana) nimeweza kwenda kutumia haki yangu kupiga kura na kurejea nyumbani kupumzika.”

    Kwa upande wa kanda ya Mbeya na Rukwa Theophil Sikazwe alirejea kwa kupata kura 70 dhidi ya 36 za John Mwangakala na kanda ya Iringa na Ruvuma Eliud Mvella amekuwa mshindi kwa kupata kura 52 na kumbwaga Joseph Mapunda aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo akiwa amepata kura 50 huku John Kiteve akipata kura tano. Katika kanda ya Lindi na Mtwara Shaibu Nampunde alitetea nafasi yake kwa kupata kura 52 na Murtaz Mangungu kura 31, Juma Muruwa kura 19 na Vincent Majili kura tano.

    Kanda ya Dodoma na Singida Hussein Mwamba aliibuka mshindi kwa kunyakua kura 46 na kuwabwaga Mulami Ng’hambi aliyepata kura 43 na Nassor Kipenzi aliyeambulia kura 18 wakati Kanda ya Pwani na Morogoro ilichukuliwa na Athumani Kambi na kumbwaga Hassan Hassanol kwa kupata kura 57 dhidi ya 50.

    Wakati kanda ya Kilimanjaro na Tanga Khalid Mohamed alishinda kwa kupata kura 44 na kumwangusha Titus Bandawe aliyepata kura 27 huku Charles Mchau kura 25 na Benedict Macha kura 10.

    Kanda ya Dar es Salaam, Muhsin Balbhou aliishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 41 na kuwashinda wapinzani wake Omari Abdulkadir aliyepata kura 37 na Lameck Nyambaya aliyepata kura 29. Viongozi waliochaguliwa jana watakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka miaka minne na kuongoza kwa jahazi la soka ya Tanzania ambalo limeanza kwenda katika njia sahihi.