Rabu, 04 Februari 2009

YANGA NOMA. ILIMPA MTU BAO 8. KIPA AKAA CHINI...

Kipa wa Etoile d'Or Mirontsy ya Comoro alipoamua kukaa chini baada ya Yanga kupachika bao la nane katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa kwenye uwanja wa Taifa wikiendi iliyopita. Yanga ilishinda 8-1 huku mshambuliaji wake Mkenya, Boniface Ambani akipachika mabao manne peke yake.

WAKATI mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na matumaini makubwa kushinda mechi ya leo dhidi ya Etoile d�Or ya Comoro, wapinzani wao wametamba ngoma itakuwa nzito.

Kocha Mkuu wa Yanga, Dusan Kondic raia wa Serbia ameonyesha kupunguza kasi ya mazoezi ya nguvu hali inayoonyesha ameridhika na fiziki ya kikosi chake na badala yake amelalia zaidi katika masuala ya kiufundi.

Lakini Kocha Mkuu wa Etoile d�Or, Nasurdine Maanrouf alianza na mazoezi makali baada ya kutua nchini na jana alipanga wachezaji wake wafanye mazoezi ya taribu kabla ya kupumzika leo asubuhi wakisubiri �mtanange� huo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Kondic amesema kwa ufupi, "Siwezi kudharau mechi kama wengi wanavyosema, nataka kushinda. Tukipata ushindi mzuri, tutajihakikishia kusonga mbele mapema, maana yake tutaanza kuangalia zaidi raundi inayofuata,"alisema.

Lakini Maanrouf amesema, "Naijua Yanga ingawa kwa kuisikia, umaarufu wake kwa Comoro pale ulikuja baada ya kuitoa AJSM, ambayo ni moja ya timu bora kule kwetu. Tumekuja tukiwa na tahadhari zote."

Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo jana walikuwa wakilanda katika mitaa ya Kariakoo huku wakishangaa mitaa na majengo marefu na baadhi ya mashabiki wakiwakejeli na kuwaonyeshea vidole vya mabao matano. Wakati huo wapinzani wao Yanga wakiwa wamepumzika kwenye kambi yao katika hoteli ya Lamada.


Mshambuliaji tegemeo wa Yanga, Boniface Ambani akipasha msuli tayari kuingia uwanjani kufanya vitu vyake. Yanga ambayo ndio timu pekee Afrika Mashariki yenye kipa mzungu inaanza kampeni zake za Ligi ya Mabingwa leo Jumamosi kwa kuivaa Etoile d�Or ya Comoro Jijini Dar es Salaam,


Naye mshambuliaji nyota wa Yanga, Boniface Ambani alisema yuko katika hali nzuri zaidi, "Nilikuwa nahofia kupiga mashuti, lakini mechi ya ligi iliyopita niliachia shuti na kuona sijajitonesha. Mechi ya Wacomoro nitacheza kwa raha na kujiamini zaidi.

Wakati Ambani anasisitiza kutaka kupachika mabao, mabeki, Shadrack Nsajigwa, Nadir Haroub �Canavaro� na kiungo Athuman Idd �Chuji� wamesisitiza kutaka kupata ushindi mnono.

Uchunguzi wa Mwanaspoti unaonyesha Yanga ina kila sababu ya kuibuka na ushindi mnono ingawa Wacomoro hao watacheza kwa kujihami muda mwingi ili kuzuia kurejea kwao na mvua ya mabao kwa kuwa wameonyesha uoga wa wazi wazi wa kukutana na Jangwani.

Timu hiyo ni changa katika michuano ya kimataifa kwani mara nyingi zimekuwa zikishiriki timu za AJSM, iliyobamizwa mabao 5-1 na Yanga, nyingine ni Etoile de Sud na Coin Nord.

Katika mazoezi yao, wameonyesha zaidi kucheza mchezo wa kujihami zaidi huku wakijifunza kushambulia kwa kushitukiza na kufunga kwa mipira ya krosi.

Iwapo Yanga itavuka, katika hatua hiyo itakutana na mabingwa watetezi wa Afrika, Al Ahly inayoongozwa na kiungo mahiri na mchezaji bora wa mwaka 2008 wa BBC, Mohammed Aboutrika.

Timu 42 zinashiriki katika hatua hiyo ya Ligi ya Mabingwa wakiwamo mabingwa wa Zanzibar, Miembeni, ambao wamefunga safari kwenda kuivaa Mwonomotapa ya Zimbabwe.

Huenda Kondic akapanga kikosi chake kama ifuatavyo: Kaseja au Obren, Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, George Owino Haroub Cannavaro, Geofrey Bonny, Mrisho Ngassa, Athuman Idd, Boniface Ambani, Ben Mwalala na Shamte Ally.

Wakati Yanga ni leo, kesho Jumapili kwenye uwanja huo huo ni zamu ya Prisons ya Mbeya, ambayo inaikaribisha Khalij Sert ya Libya katika mechi ya Shirikisho.

Wachezaji wamemueleza mwandishi wetu, Michael Momburi kwamba wanachotaka ni kuibuka na ushindi kesho na kuliwakilisha vema taifa.

"Hakuna kukata tamaa hili ni soka na ndio maana tunajiandaa, kila kitu kipo sawa kufanya vibaya kwenye mechi za ligi haimaanishi kwamba hata kimataifa itakuwa hivyo,"alisema mshambuliaji Oswald Morris.

"Mpira ndivyo ulivyo, tutajitahidi kurekebisha makosa hao Walibya hatuwajui lakini tutapambana nao uwanjani na tunaamini matokeo yatakuwa mazuri, tutashangaza."

Kocha wa timu hiyo, James Nestory alisema kwamba kikosi chake kimejipanga vizuri na hawana mchecheto wowote na wageni.

Prisons imekuwa na mwenendo usioridhisha tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara lakini wachezaji wake wamesema hiyo haijalishi katika mchezo wa kesho wala haina nafasi.

Imepoteza mechi tatu kwa timu za Dar es Salaam, yaani Yanga, Simba na Villa Squad, ambayo mzunguko wa kwanza ilionekana 'wagawa pointi'.

Kikosi cha Mundu ndio wawakilishi wa Zanzibar katika michuano hiyo na inakutana na wenyeji wake, Red Arrows ya Zambia.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar