Kamis, 18 Desember 2008

Tenga amgaragaza Malinzi


Na Jumanne Khasim
Daily News; Monday,December 15, 2008 @12:20

Habari nyingine
  • Malkia wa Afrika Mashariki kupatikana leo
  • Flamingo yapigwa jeki
  • Mbilinyi bingwa wa Fiddle
  • Redio, runinga zatakiwa kuacha kuwanyonya wasanii
  • Mbio za wazi kufanyika Dar
  • Wasanii waingiza 16.5m/-
  • Zambia yaalikwa Chalenji
  • 70 kuchuana katika gofu leo
  • Laibon FC bingwa Longido
  • Filamu, tamthiliya zinapotosha maadili
  • Rais wa Shirikisho la Soka Leodegar Tenga ametetea nafasi yake kwa kumbwaga mpinzani wake Jamal Malinzi katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana Dar es Salaam.


    Katika uchaguzi huo uliofanyika jana kwenye ukumbi wa NSSF waterfront, Tenga alitangazwa mshindi kwa kupata kura 68 dhidi ya kura 39 za Malinzi ambaye alirejeshwa kuwania nafasi hiyo baada ya kushinda rufaa kutokana na kuenguliwa na kamati ya uchaguzi.

    Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa Tenga alisema " nawashukuru wajumbe kwa kunipa nafasi nyingine ya kumalizia kazi niliyoianza.'Pia alimuhakikishia Mwakilishi wa wa Shirikisho la Soka la Taifa (FIFA) kwenye uchaguzi huo Ashford Mamelodi kuwa kipindi cha miaka mnne ijayo kitakuwa cha kuendeleza maendeleo yaliyokwishafikiwa.

    Nate Malinzi pamoja na kukubali kushindwa alimuomba Tenga kutokuweka kisasi kwa wale ambao hawakumpigia kura jambo ambalo Tenga alimhakikishia halitakuwapo.Aidha Malinzi aliahidi kumkabidhi ilani yake ya uchaguzi ambayo itakuwa changamoto katika utendaji wake wa kazi.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Henry Tandau alimtangaza athumani Nyamlani kuwa mshindi wa nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, baada ya kujikusanyia kura 65 kati ya kura 107 zilizopigwa na kura mbili kuharibika. Mwalusako alipata kura 39 na Ali Mwanakatwe aliambulia kura moja.

    Katika nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais wa TFF ambaye anawakilisha klabu za Ligi Kuu, nafasi hiyo ilikwenda kwa mgombea Ramadhan Nassib aliyemwangusha mpinzani wake wa karibu Damas Ndumbalo aliyepata kura 45.

    Nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji imechukuliwa na wallace Karia ambaye ni mpinzani wake Abduk Sauko aliyepata kura 26 huku kura moja ikiharibika. Wajumbe wengine wa kamati ya utendaji kupitia kanda 11 za soka ni kama ifuatavyo: Amri Roshan ametetea nafasi yake katika kanda ya Kagera na Shinyanga kwa kumshinda Mbasha Masha kwa kura 88 kwa 19.

    kanda ya pili inayojumuisha mikoa ya Mara na Mwanza Samuel Nyalla ambayye alikuwa mgombea pekeealipata kura 73, kura 33 za hapana wakati kura tatu ziliharibika na kwa upande wa kanda ya Manyara na Arusha, Khafani Mgonja aliibuka kidedea kwa kupata kura 60 dhidi ya 45 za mpinzani wake Charles Mugodo, kura mbili ziliharibika kwenye uchanguzi huo.

    kanda ya Kigoma na Tabora, Msafiri Mgoyi alimbwaga Ismail rage kwa kura 75 dhidi ya 32. Akizungumza na alimbwaga Ismail Rage kwa kura 75 dhidi ya 32. Akizungumza na gazeti hili, Rage alisema kuwa: “ Nilikuwa naumwa na jana (juzi) jioni ndipo niliporuhusiwa kutoka hospitali lakini leo (jana) nimeweza kwenda kutumia haki yangu kupiga kura na kurejea nyumbani kupumzika.”

    Kwa upande wa kanda ya Mbeya na Rukwa Theophil Sikazwe alirejea kwa kupata kura 70 dhidi ya 36 za John Mwangakala na kanda ya Iringa na Ruvuma Eliud Mvella amekuwa mshindi kwa kupata kura 52 na kumbwaga Joseph Mapunda aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo akiwa amepata kura 50 huku John Kiteve akipata kura tano. Katika kanda ya Lindi na Mtwara Shaibu Nampunde alitetea nafasi yake kwa kupata kura 52 na Murtaz Mangungu kura 31, Juma Muruwa kura 19 na Vincent Majili kura tano.

    Kanda ya Dodoma na Singida Hussein Mwamba aliibuka mshindi kwa kunyakua kura 46 na kuwabwaga Mulami Ng’hambi aliyepata kura 43 na Nassor Kipenzi aliyeambulia kura 18 wakati Kanda ya Pwani na Morogoro ilichukuliwa na Athumani Kambi na kumbwaga Hassan Hassanol kwa kupata kura 57 dhidi ya 50.

    Wakati kanda ya Kilimanjaro na Tanga Khalid Mohamed alishinda kwa kupata kura 44 na kumwangusha Titus Bandawe aliyepata kura 27 huku Charles Mchau kura 25 na Benedict Macha kura 10.

    Kanda ya Dar es Salaam, Muhsin Balbhou aliishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 41 na kuwashinda wapinzani wake Omari Abdulkadir aliyepata kura 37 na Lameck Nyambaya aliyepata kura 29. Viongozi waliochaguliwa jana watakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka miaka minne na kuongoza kwa jahazi la soka ya Tanzania ambalo limeanza kwenda katika njia sahihi.

    Tidak ada komentar:

    Posting Komentar