utaruhusu wanandoa kujamiiana itakapowezekana | |
Gloria Tesha Daily News; Sunday,March 08, 2009 @18:39 | |
Hayo yalielezwa na Kamishna Mkuu wa Magereza, Augustino Nanyaro wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwavisha nishani askari 44 wa Magereza mwishoni mwa wiki Dar es Salaam. Alisema upitiaji wa mapendekezo hayo unachukua muda na hata utekelezaji wake utategemea mambo mengi, yakiwamo ya uwezo wa kiuchumi. Kama utaratibu huo utaanza kutumika, wafungwa watakaokuwa na vigezo stahili vikiwamo vyeti vya ndoa, watapaswa kutumia maeneo yenye mazingira tofauti na gerezani lakini si nje ya gereza. “Wazo lipo lakini uwezo wa kutekeleza ni kitu kingine, tumeyaona haya kwa wenzetu katika kutembea kwetu na tumedhani ni jambo zuri kufanyika hapa nchini, kufungwa si kwamba hustahili mambo yote,” alisema Kamishna Mkuu wa Magereza, Augustino Nanyaro. Alisema hata hivyo utekelezaji huo hautahusu kila mfungwa, bali ni wale watakaokidhi vigezo ikiwamo nidhamu na heshima ya hali ya juu itakayoruhusu kukaa na familia yake (mke au mume) na kujamiiana. Alisema hata hivyo, utekelezaji wake utachukua muda mrefu kulingana na hali ya uchumi itakavyoruhusu. Nanyaro alisema mpango huo utakuwa na faida kwa vizazi vijavyo baada ya mambo ya msingi kama kupunguza msongamano yatakapopatiwa ufumbuzi wa kudumu. Kuhusu msongamano magerezani, alisema ziara ya Rais Jakaya Kikwete ya kutembelea magereza aliyoifanya zaidi ya mwaka mmoja uliopita imeanza kuzaa matunda, kwani msongamano umepungua na kasi ya kusikiliza kesi mahakamani imeongezeka tofauti na awali. “Ushirikiano wa mahakama, polisi na magereza umeongezeka baada ya ziara ya rais na maboresho yamefanyika na yanaendelea kufanyika magerezani, tumejenga mabweni mawili ya wafungwa gereza la Ukonga na ukarabati wa mabweni unaendelea huko Tanga, Mbarali, Lilongwe na maeneo mengine,” alisema Kamishna huyo. Aidha kuhusu idadi ya wafungwa waliohukumiwa kunyongwa na namna wanavyochangia msongamano magerezani kutokana na kukaa muda mrefu gerezani bila hukumu yao kutekelezwa, alisema wafungwa hao hawazidi 400 na idadi hiyo haichangii kwa namna yoyote msongamano. Kuhusu mazingira na namna Magereza ilivyojipanga kutumia nishati mbadala na gesi asilia kuepusha uharibifu wa mazingira kutokana na matumizi ya kuni, alikiri kuwa wanachangia uharibifu wa mazingira na kwamba miradi mbalimbali ya gesi mbadala na asilia inafanyika katika magereza. Alisema maofisa kadhaa wa magereza walipelekwa Rwanda kupata utaalamu wa kutengeneza nishati kutokana na kinyesi katika gereza kuu la nchi hiyo na sasa majaribio yanafanyika katika gereza la Ukonga na yatakamilika Mei mwaka huu. “Walipata mafunzo kwa gereza la wafungwa 11,000 ambalo wanatumia nishati itokanayo na kinyesi cha mahabusu. Ukonga mradi wa majaribio unafanyika kupitia mtaalamu yule yule wa Rwanda na itakapokamilika na kuonyesha mafanikio, tutaitumia kwa magereza yote 12 makuu,” alisema. Aliyataja magereza mengine yenye miradi ya gesi na nishati mbadala kuwa ni Ruanda, Mbeya wanakotumia mkaa wa mawe, Keko, Dar es Salaam wanakotumia gesi asilia ya Songo Songo kwa majaribio na Chuo cha Magereza Ukonga. Katika hatua nyingine, Nanyaro alisema mchakato wa kupanda miti kwa kushirikiana na wafadhili, wizara mbalimbali, mashirika ya nje na ndani ya nchi unaendelea katika maeneo mbalimbali ambapo tayari miti zaidi ya milioni tatu imepandwa. Maeneo hayo ni pamoja na Bariadi mkoani Shinyanga ambapo zaidi ya ekari 1,200 zimehusika. |
Senin, 09 Maret 2009
wAFUNGWA SASA KURUHUSIWA KUFANYA MAPENZI GEREZANI
Langganan:
Posting Komentar (Atom)
Tidak ada komentar:
Posting Komentar