Ushindi huo umeifanya Yanga kukaribia utetezi wa ubingwa wake pamoja na kujichimbia kileleni kwa kufikisha pointi 36.
JKT Ruvu imepoteza mechi zote mbili kwa Yanga, kwani katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ilichapwa mabao 2-1.
Mchezo wa jana ulikuwa wa mashambulizi ya hapa na pale, na Yanga walilifikia lango la wapinzani wao katika dakika za 15 na 30 lakini Jerry Tegete na Boniface Ambani mashuti yao hayakulenga lango.
Kipa wa JKT, Abdallah Ngachimwa alisimama imara na kuokoa shuti la Ambani katika dakika ya 22 kabla ya Kessy Muhsin kupiga shuti la umbali wa mita 30 lililodakwa kifundi na Juma Kaseja.
Kipindi cha pili, Yanga waliongeza kasi ya mashambulizi na katika dakika ya 67, Shamte Ally aliipatia bao kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi ya Mrisho Ngassa.
Shamte alifunga bao hilo baada ya kuingia dakika ya 65 kuchukua nafasi ya Ambani.
Yanga iliendelea kushambulia na katika dakika za 55 na 63 walikosa mabao mfululizo kupitia kwa Tegete kabla ya Mashaka Maliwa wa JKT naye kukosa bao akiwa na Kaseja katika dakika ya 77.
Kocha wa Yanga, Dusan Kondic alisema timu yake imekosa umakini kutokana na wachezaji wake kutokaa pamoja muda mrefu. Hata hivyo aliwapongeza kwa ushindi.
Akizungumzia mchezo huo, kocha wa JKT Ruvu, Charles Kilinda alisema ngome kukosa umakini ndiyo chanzo cha wao kufungwa. Hata hivyo alilalamikia maamuzi ya Kazi, kuwa hakuwa makini.
Naye Dorice Malyaga anaripoti kuwa Mtibwa Sugar imeichapa Kagera Sugar mabao 2-1 katika mchezo wa ligi hiyo kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani.
Mabao ya Mtibwa yaliwekwa kimiani na Rashid Gumbo katika dakika 20 na Abdallah Juma katika dakika 89 baada ya kuunganisha mpira wa kona wa Yahaya Akilimali.
Bao pekee la Kagera lilifungwa na Paul Kabange katika dakika ya 25.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar