Jumat, 27 Maret 2009

Mwandishi wetu wa kutumainiwa ametuletea hii

ZIJUE IQ ZA WATU MBALIMBALI MASHUHURI

Na Tedy Mwarabu

Barack Obama 110
George Bush 91
Bill Clinton 182
Jimmy Carter 175
John Kennedy 174
Richard Nickson 155
Franklin Ruswelt 147
Ronald Regan 105
Gerald Ford 121
Lindon Johnson 126
Sharon Stoun 154

0-60 very low
60-90 low
90-110 normal
110-130 high
130-200 very high

Na Tedy Mwarabu wa THE THOMCOM

Yanga yatwaa ubingwa na mechi 5 mkononi

WAKATI kipute cha Ligi Kuu Tanzania Bara kikiwa inaelekea ukingoni huku kila timu ikiwa imebakiza mechi tano, tayari Yanga imeshatwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo, Prisons ya Mbeya imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta baada ya kuichapa Kagera Sugar 2-1.

Katika mchezo huo ambao jana ulihailishwa kutokana na mvua nyingi iliyonyesha jijini Mbeya na kusababisha uwanja wa Sokoine kujaa maji, ulishudia wenyeji Prisons ikipata bao la mapema katika dakika ya 7 lililofungwa na Yona Ndabila aliyeunganisha vema pasi ya Osward Morris.

Kagera Sugar wenye hamu ya kubwa ya kuchukua nafasi ya pili walijirekebisha katika kipindi cha pili na kupata bao la kusawazisha mwanzoni kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Shija Hassan baada ya kuchezewa vibaya kwenye eneo la hatari.
Maafande hao wa magereza waliandika bao la ushindi kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 64 iliyofungwa na Ismail Suma kwa ushindi huo sasa Prisons imefikisha pointi 25 ikiwa nyuma kwa pointi mbili kwa Simba.

Simba ina kazi ya ziada kuhakikisha inashinda mechi zake zilizosalia ili kubaki nafasi ya pili huku ikiiombea dua baya Kagera Sugar.

Mabingwa wa Tanzania Bara, ambao wamekuwa wakitumia staili yao ya 4-4-2 wameendelea kuwawashia indiketa wapinzani wao Simba ambao waliukosa ubingwa huo msimu uliopita na kushikiria nafasi ya tatu huku nafasi ya pili ambayo ilichukuliwa na Tanzania Prisons ya Mbeya.

Wakati Yanga wakishekelea kutangaza ubingwa mapema, timu za Polisi Dodoma, Villa Squad na Moro United zinapumulia kwenye mashine kutokana na timu hizo kuwa kwenye hatari ya kushuka daraja.

Katika msimamo wa ligi, Polisi Dodoma inashika mkia baada ya kucheza mechi 17 na imeshinda moja, imetoka sare mara tisa na imepoteza saba na ina pointi 12.

Villa Squad wamecheza mechi 16 wameshinda nne, wamedroo mbili na kupoteza 10 wana pointi 14 wakati Moro United ina pointi 15 ikiwa imepishana pointi moja na Polisi Morogoro, ambayo ina pointi 16.

Mechi zote zinaifanya ligi kuwa ngumu kutokana na timu zote kupambana kufa na kupona kuhakikisha zinabaki kwenye Ligi Kuu na timu za Simba, Mtibwa na Kagera wakiwania zikiwania nafasi ya kusaka Kombe la Shirikisho.

Tayari timu za Majimaji, Manyema na African Lyon zimepanda daraja na timu tatu zitashuka daraja ligi kuu.

Wafungaji waongoza kwa ufungaji msimu huu ni Boniface Ambani wa Yanga mwenye mabao (14) akifuatiewa na Hessen Bunu (JKT Ruvu) (10), Said Dilunga wa Toto Africa (8), Musa Mgosi wa Simba (7).

Kamis, 26 Maret 2009

KIINGILIO, KIINGILIO, KIINGILIO

THE HUSTLERS ENTERTAINMENT wanawatangazia wapenzi wote wa miondoko ya POP kuwa mchango wa kiingilio umeanza kutolewa. mchango wako unaweza kupelekwa kwa wafuatao.

Block 1. FATUMA
Block 2. SHAA
Block 5. MUDI na HUSEIN NGENJE
Block 6. ZEFANIA NA KAPONTA
Block 7. JESSE na MICHAEL MBASHA
Block 8. KAZUNDE na SHOLLA
Block 9. KINANA na ATHUMANI (FIDO)
Block 10. MAPIGANO, ZEDEKIA na LUSANDA
Block 11. JAMILA

Rabu, 25 Maret 2009

Yanga inatisha, yatwaa ubingwa kabla ya ligi kuisha licha ya TFF kuwanyang'anya point 2....

Na Tedy Mwarabu

Mabigwa wa soka Tanzania bara 2008/9 Yanga wakipongezana. Wamefanikiwa kutangaza ubingwa kabla ligi haijaisha.

BAO la mwaka la kipa Juma Kaseja lilitosha kuweka historia mpya kwa kuipa Yanga ubingwa wa 22 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza huku Azam ikiichapa 6-2 Villa Squad jijini Dar es Salaam.

Yanga iliyokuwa ikihitaji pointi tatu ili kutangazwa mabingwa kwa msimu wa 2008/'09, iliandika bao lake la kwanza katika dakika ya 21 lililofungwa na Kaseja aliyetumia vizuri udhaifu wa mwenzake, Abdallah Msafiri wa Toto Africa na kuachia mkwaju ambao ulidunda na kutinga nyavuni.

Awali, Kaseja alidaka na kupiga mpira mrefu wa juu uliokwenda moja kwa moja wavuni, dakika tisa baadaye Hussein Sued aliisawazishia Toto Afrika kabla ya Mike Baraza kufunga bao la pili na ushindi kwa mabingwa hao.

Katika mchezo huo ulioshuhudia timu hizo zikikosa penalti kila moja, mshambuliaji MkenyaMike Baraza wa Yanga alikosa penalti dakika ya 18 kipindi cha kwanza , naye Said Dilunga alipoteza nafasi ya pekee ya kuisawazishia Toto wakati mkwaju wake wa penalti ulipoishia mkononi mwa Kaseja, dakika ya 62.

Naye Sweetbert Lukonge anaripoti kutoka Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuwa jahazi la Villa Squad limezidi kuzama baada ya kukubali kipigo cha mabao 6-2 kutoka kwa Azam FC.

Mshambuliaji Nsa Job ndiye aliyekuwa mwiba mkali kwa ngome ya Villa kwa kupachika mabao matano peke yake na kuzawadiwa mpira akimwachia mchezaji wa kimataifa wa Uganda, Danny Wagaluka akihitimisha karamu hiyo ya mabao kwa bao la sita.

Katika mchezo huo uliokuwa na raha ya aina yake, ulishuhudia mabao manne yakifungwa ndani ya dakika nane za mchezo huo, Azam ilipata mabao kupitia kwa Nsa Job, dakika ya 16 na 25 wakati Villa walisawazisha kupitia kwao, Juhudi Samwel 19 na Lewede Dayton (24),kipindi cha kwanza na kufanya matokeo kuwa 2-2 hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kilikuwa kibaya zaidi kwa Villa baada ya Nsa Job kufunga bao la tatu, nne na sita katika dakika ya 51,74 na 88, huku Mganda Wagaluka akipachika bao la tano (85).

Katika kile kilichoonekana kama kuchanganyikiwa na kipigo, mchezaji wa Villa , Launt Bagia alikosa penalti mwisho mwa mchezo, dakika ya 90 iliyopanguliwa na kipa wa Azam, Vladimir Niyonkuru.

Kutoka Mbeya, Brandy Nelson anaripoti kuwa mvua kubwa iliyokuwa inanyesha mjini humo ilisababisha mwamuzi Dominick Nyamsana kutoka Dodoma kuusimamisha mchezo huo katika dakika ya 28.

Mchezo huo baina ya Prisons na Kagera Sugar ulikuwa ukichezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa huku zikiwa zimefungana bao 1-1.

Akizungumzia kuahirishwa kwa mechi hiyo mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoani Mbeya, Festo Nkemwa alisema mvua kubwa iliyojaza maji uwanjani ndiyo sababu ya kuahirishwa kwake.

Nkemwa alisema mvua hiyo ilisababisha wachezaji wa timu hizo kuanguka na kuweza kuhatarisha afya zao.

Naye mwamuzi Nyamsana alisema hadi uamuzi huo ulifikiwa kutokana na hali ya uwanja kutofaa tena kwa mchezo huo.

Mabao hayo, Prisons yalifungwa na Shaban Mtupa dakika ya nne, Haruna Hassan wa Kagera akasawazisha, dakika ya 18.

Licha ya kutakiwa kukamatwa na mahakama ya kimataifa pindi atakaposafiri.....

Rais wa Sudan afika Misri

Na Tedy Mwarabu

Rais wa Sudan Omar al-Bashir
Kiongozi wa Sudan anashtakiwa kwa makosa ya kihalifu chini ya mazingira ya kivita nchini Sudan
Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, amewasili nchini Misri.

Hii ni safari yake ya pili tangu waranti ya mahakama ya kimataifa ya ICC ya kutaka akamatwe kutolewa.

Nchi ya Misri haimo katika orodha ya mataifa ambayo yametia saini mkataba wa ICC.

Mataifa wanachama yanawajibika kumnasa yeyote yule ambaye hati ya kumkamata imetolewa dhidi yake, wanapoingia katika ardhi ya nchi hiyo.

Bw Bashir, ambaye alifanya ziara fupi siku ya Jumatatu nchini Eritrea, anatazamiwa kufanya mashauri na Rais Hosni Mubaraka wa Misri.

Kiongozi huyo wa Sudan anashtakiwa kwa makosa ya kihalifu katika mazingira ya kivita katika eneo la Darfur.

Bado haijafahamika wazi ikiwa rais Bashir ataendelea na mipango yake ya kuhudhuria mkutano wa mataifa ya Kiarabu utakaofanyika Doha, Qatar, kati ya tarehe 29-30 mwezi Machi.

Mamlaka ya juu zaidi ya kidini nchini Sudan, ambayo ni kamati ya wasomi wa Kiislamu, wiki hii ilimshauri asisafiri, kutokana na vitisho kutoka kwa maadui.

China yatuumiwa na PENTAGON kuwa inazalisha silaha nyingi mno....

WASHINGTON – China is increasing its military power more rapidly and developing new "disruptive technologies" that are shifting the military balance in its region and possibly beyond, a new Pentagon report said.

And Beijing continues to develop weapons that threaten Taiwan, even though tensions between the two have been reduced significantly, according to the report scheduled for release later Wednesday.

The latest in a series of annual assessments for Congress of China's military power, the report says the U.S. "welcomes the rise of a stable, peaceful and prosperous China and encourages China to participate responsibly" in world affairs.

"However, much uncertainty surrounds China's future course, particularly regarding how its expanding military power might be used," said a summary of the report obtained by The Associated Press.

The report comes in the wake of heightened tensions between the U.S. and China this month, after Chinese vessels harassed a U.S. Navy surveillance ship in international waters in the South China Sea.

During a meetings with China officials after the incident, Secretary of State Hillary Rodham Clinton said both sides have agreed on the need to reduce tensions and avoid a repeat of the confrontation.

The new report notes that the People's Liberation Army is undergoing a comprehensive transformation from a mass army designed for long wars of attrition on its territory to one that can fight and win short, high-intensity conflicts along its periphery against high-tech adversaries.

"The pace and scope of China's military transformation have increased in recent years, fueled by acquisition of advanced foreign weapons, continued high rates of investment" in technologies and far-reaching doctrinal reforms in the armed forces, the report said.

"China's ability to sustain military power at a distance remains limited, but its armed forces continue to develop and field disruptive military technologies ... that are changing regional military balances and that have implications beyond the Asia-Pacific region," it said. It said that included technologies for nuclear, space and cyber warfare.

The report noted China's buildup of short-range missiles opposite Taiwan. Taiwan and China split amid civil war in 1949 and Beijing says it is intent on eventual unification, by persuasion if possible but by force if considered necessary.

"In the near-term, China's armed forces are rapidly developing coercive capabilities for the purpose of deterring Taiwan's pursuit of ... independence," the report said, adding China's military might could be used to pressure Taiwan toward a settlement on Beijing's terms "while simultaneously attempting to deter, delay or deny any possible U.S. support for the island in case of conflict."

Since taking office 10 months ago, Taiwanese President Ma Ying-jeou has moved aggressively to reverse his predecessor's pro-independence polices, sanctioning a rapid expansion in trade relations with the mainland, and raising the prospect of a formal peace treaty between the sides.

China's Premier Wen Jiabao said early this month that Beijing is ready to hold talks with Taiwan on political and military issues in the pursuit of ending hostility between the longtime rivals. But Taiwan's defense minister later noted publicly that China has made repeated threats to attack Taiwan if it moves to make its de facto independence permanent and that Taiwan remains concerned about the estimated 1,300 missiles Beijing has readied against the island.

Wednesday's report also noted that China has used its military muscle for good, such as peacekeeping and disaster relief.

Senin, 23 Maret 2009

HOTELI HIZI ZA TANZANIA ZIMETEKETEA KWA MOTO...


Hotel za kitalii za Paradise Holiday Resort na Oceanic Bay and Resort zilizo katika ufukwe wa Bahari ya Hindi wilayani hapa, zimeteketea kwa moto. Moto huo ulioteketeza hoteli zote mbili kwa muda wa saa moja leo, ulianzia jikoni katika Hoteli ya Paradise na kushika mtungi wa gesi na kusambaa kwa kasi kutokana na hoteli hiyo kuezekwa kwa makuti na kuwapo upepo mkali.

Moto ulikuwa ukiwaka kwa juu usawa wa meta 30. Baada ya kuona Hoteli ya Paradise inawaka, wafanyakazi wa hoteli jirani ya Oceanic Bay walikwenda kutoa msaada na wakati wakiendelea kusaidia, ghafla moto ulishika katika hoteli yao na wao kushindwa kurejea kuokoa mali.

Kutokana na moto huo kushika kasi, wageni waliokuwapo walihaha kujiokoa na baadhi yao kufanikiwa kuondoka na mizigo yao. Hata hivyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha.

Katika Hoteli ya Paradise ambayo ni maarufu kwa mikutano, iliyopo umbali wa takriban kilometa 60 kutoka Dar es Salaam, sehemu ambayo haijaungua ni ya chakula na vibanda vichache ufukweni, wakati Hoteli ya Oceanic sehemu iliyosalia ni baa peke yake.

Katika tukio hilo lililotokea saa 4.30 asubuhi, magari matatu yaliyokuwa katika Hoteli ya Paradise yaliungua, moja aina ya Nissan Patrol namba T382 ASR liliteketea lote na mengine yaliyoungua ni la Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mbeya aina ya Toyota GX namba STK 3240 na Toyota Land Cruiser namba T 182 ATX lililokuwa likitumiwa na Dk. Donath Mrawira.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo aliyekuwa eneo la tukio, Serenge Mrengo, alisema, “moto umeshika kasi sana kwa sababu ya kuezekwa kwa makuti na upepo mkali, hii ni changamoto kwetu kubadili mtindo wa kuezekea makuti”.

Akielezea jinsi walivyouona moto huo, mkufunzi kutoka Canada aliyekuwa akitoa mafunzo kwa mameneja wa mikoa 21 wa Tanzania bara wa Tanroads, Dk. Donath Mramira, alisema “baada ya kutoka mapumziko ya chai kwenye saa 4.30 asubuhi tukiwa ndani, ghafla umeme ulikatika na tuliamua kuendelea na mafunzo, lakini dada mmoja alifungua mlango tupate hewa ndipo tukaona watu wanalia.

“Tulidhani kuna mtu amekufa, lakini kufuatilia vizuri tukaona hoteli inaungua moto, mimi niliokoa laptop yangu na projekta tu na hili gari lililoungua ni la rafiki yangu aliyeniazima nilitumie nikiwa hapa nchini”. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Hoteli ya Paradise ambaye pia ndiye mmiliki wake, Abdullahi Nur Guled, alisema hoteli hiyo imekatiwa bima na thamani yake ni zaidi ya dola milioni 10 za Marekani (sawa na zaidi ya Sh bilioni 13).

“Wasiwasi wangu ni wafanyakazi ambao wako 180 watakosa kazi na serikali itakosa mapato, achilia mbali wale wanaoajiriwa kwa kutuletea vitu hotelini,” alisema. Naye Meneja Uendeshaji wa Paradise, Shukri Ali, alisema hoteli hiyo iliyoanza kutoa huduma mwaka 1997 ilikuwa na uwezo wa kupata faida ya dola 60,000 hadi 80,000 kwa siku kutokana na huduma zake.

Meneja huyo aliyedai hawajafanikiwa kuokoa kitu, alisema hoteli hiyo ina vyumba 82 na wakati tukio linatokea, ilikuwa na wageni 89 waliopanga na watu 70 waliokuwa wakihudhuria mikutano minne tofauti, ukiwamo huo wa Tanroads.

Mkuu wa Wilaya alisema magari ya zimamoto yalitoka Dar es Salaam na wilayani Kibaha na kuongeza: “Sisi Bagamoyo hatuna gari la kuzimia moto, mwaka juzi Halmashauri ililipa zaidi ya Sh milioni 400 lakini hadi leo gari halijafika”.

Magari yaliyoonekana kutoa huduma za kuzima moto huo ni ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam namba STK 1066 na SM 5778. Kwa upande wa Meneja Mkuu wa Hoteli ya Oceanic Bay, Rahul Nayar, alisema hoteli yake ilikuwa imeajiri wafanyakazi 200 na kutokubali kuzungumzia lolote kwa madai mmiliki yuko Dubai.

“Siwezi kuzungumzia hasara, mwenye hoteli yuko Dubai ndiye anayefahamu kila kitu,” alisema. Thamani halisi ya uharibifu haikuweza kupatikana mara moja, kwani hakukuwa na mtu aliyekuwa tayari kuzungumzia hilo leo. Uezekaji makuti umekuwa ukichochea kasi ya moto kama ilivyotokea Septemba 22 mwaka juzi, ambapo Hoteli ya Sea Cliff ya Dar es Salaam ikiwa na vyumba 92 nayo iliungua moto kwa staili kama hii.

Minggu, 22 Maret 2009

BAADA YA KUAPISHWA MAPEMA LEO...RAIS WA MADAGASCAR AHUTUBIA TAIFA

Taadhari kwa wanafunzi wote waliojaza fomu za mikopo online

Wanafunzi wote waliojaza fomu ya HESLB namba slf3 ukurasa wa 5/2 online wanashauriwa waangalie tena kwa makini zaidi namba ya account waliyojaza online kwa sababu taarifa za kiufundi zinaonesha kwamba namba hiyo ikiandikwa online, wakati wa kuinakili (printing) HUBADILIKA.

Taadhari hii imetufikia mapema leo kutoka katika vyanzo vyetu

Na Tedy Mwarabu

wa THE THOMCOM

Eti, kuharibu mali za wafanyabiashara wasio halali ni kukuza uchumi? Au ingekuwa ni busara kuwalazimisha watu hao kupata kibali na kuliapa fidia?

Vice-President Dr Ali Mohamed Shein destroys fishing gear seized from illegal fishermen in Lake Victoria at Kasenda village, Chato District, in Kagera Region, yesterday. A total of 23 boats and 649 fishing nets were seized during the operation that involved community embers.

(Photo by courtesy of VPO)


Aliyempiga na viatu viwili Rais wa Marekani yupo huru. Kwanini aliyemchapa kofi moja aliyekuwa rais wa Tanzania afungwe?

Mama mzazi wa Irahim Said, kijana aliyemshambulia Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Mama Rehema akitoka nje ya ofisi ya Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Simba alipokwenda kumuomba radhi kwa niaba ya mtoto wake jana.


Pia mama huyo yuko njiani kuelekea Ikulu ya Rais Kikwete kuomba msaada...


Na. Joe Mukasa

Wachina wa Bongo wataka kuandamana. Polisi wazuia maandamano

MAANDAMANO ya wachina wanaoishi jijini Dar es Salaam yaliyopangwa kufanyika jana kupinga ujambazi uliosababisha mauaji ya mwenzao yamezuliliwa na jeshi la polisi.

Wachina hao walipanga kufanya maandamano hayo jana kuanzia Uwanja wa Uhuru na kupitia Barabara ya Mandera hadi Makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambako walipanga kutoa tamko lao juu ya mauaji hayo ya Guo Chenwei (25) aliyeuwawa Kariakoo jijini Dar es Salaam kwa kupigwa risasi shingoni wiki hii.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafanyabiashara Wachina nchini, Huang Zichan, alisema licha ya kutoridhika na majibu waliyopewa kwa mdomo kutoka makao makuu ya polisi kuwa ulinzi hautakuwepo katika maandamano yao wamelazimika kusitisha hadi siku nyingine watakayoipanga upya.

“Wametueleza kwa mdomo tumewaomba watujibu kwa barua wamesema kesho (Leo) watatuita kutupa jibu kwa maandishi kuwa tusifanye maandamano hayo hadi siku nyingine kwa kuwa askari wengi wameelekezwa kwenye operesheni ya kusaka majambazi maeneo mbalimbali ya jijini,” alisema Zichan.

Zichan alisema wamesikitishwa na hatua hiyo ya kuzuiliwa kufanya maandamano yao hata hivyo, wanasubiri maelezo ya barua ya leo kisha wataandaa maandamano siku nyingine.

“Hili ni tukio la kwanza kutokea tangu tuwe hapa nchini na mauaji haya kama hayatapigiwa kelele yataendelea na kuathiri uchumi wa nchi na kuharibu uwekezaji kwa wageni, kwani tukio hili limesharipotiwa na vituo vikubwa vya habari vya kimataifa ikiwemo China na nchi za Asia, hivyo inaweza kuleta madhara ya uwekezaji hapa Tanzani,” alisema Zichan

Zichan aliongeza maandamano hayo ya amani yalikuwa na lengo la kukemea uovu wote dhidi ya wageni ambao umeonekana kuibuka eneo hilo la Kariakoo.

Awali ilidaiwa Wizara ya Mambo ya Ndani nayo ilipelekewa nakala ya barua ya maandamano hayo, lakini msemaji wa Wizara hiyo, Isaac Natanga alisema hakupokea barua yoyote kutoka kwa wachina inayohusiana na masuala ya maandamano yao.

“Sikupokea barua kuhusu maandamano na jambo hulo si la kwetu ni la polisi, hivyo waulize polisi sisi hatuhusiki na hatukupokea barua ya maandamano,’’ alisema Natanga.

Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova alipotakiwa kueleza juu ya maandamano hayo alisema suala hilo lipo juu ya uwezo wake na kwamba suala hilo limeelekezwa ngazi za juu kwa kuwa inaingilina na ushirikiano wa kimataiafa.

Hata hivyo alipoulizwa msemaji wa Jeshi la polisi, Abdalla Msika kuhusiana na maandamano hayo, alisema yupo nje ya ofisi kwa matibabu na hakuwa na taarifa kuhusiana na maandamano hayo.

Akizungumzaia mazishi na kijana huyo wa kichina, Zichan alisema hatazikwa hadi wazazi wake watakapowasili wiki ijayo kukamilisha taratibu za kusafirisha maiti.

Jumat, 20 Maret 2009

Fomu sasa zinapatikana ...rub 15 tuu

Brekin niuz...Technolojia yawasili bodi ya mikopo....fomu sasa kujazwa online...Safi sana ...

body ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu hivi karibuni imemwaga chehe baada ya kutoka makucha yake na kwa machachari sana kwa kuwezesha wanafunzi ambao huomba mikopo kwa ajili ya masomo yao ya elimu ya juu kujaza fomu za maombi online.

Maendeleo haya yamekuja wakati ambao bodi hiyo ya mikopo imepata misukosuko ya hapa na pale baada ya wanafunzi vyuo vikuu nchini kugoma kwa maandamano makubwa hivi karibuni hali iliyofanya serikali kuvifunga vyuo vikuu kwa muda (tayari vimeshafungulia).

Sasa wanafunzi wote wanashauriwa kujaza fomu za mikopo online ili kuepuka kutosomeka kwa mwandiko jambo ambalo linaweza kuchelewesha fedha za wanafunzi.

ripoti na Tedy Mwarabu


Moscow 2009

Rabu, 18 Maret 2009

Korea ya kaskazini yakataa msaada wa chakula kutoka Marekani.

Korea ya kaskazini yakataa msaada wa chakula kutoka Marekani.

Pyongyang.


Marekani imesema kuwa Korea ya kaskazini imekataa msaada zaidi wa chakula.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani na mashirika ya kutoa misaada yamesema asasi tano za Marekani zisizo za kiserikali zimeamriwa kuondoka ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, baada ya kusambaza nusu tu ya chakula walichopanga kukisambaza.

Maafisa wa mashirika ya kutoa misaada wamesema kuwa Korea ya kaskazini haikutoa sababu ya hatua hiyo.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa karibu watu milioni saba nchini Korea ya kaskazini bado wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.

Nchi hiyo imekuwa ikitegemea msaada wa chakula kutoka nje tangu njaa ya miaka ya 1990 iliyoua mamia ya maelfu ya watu nchini humo.

Kuzuiwa huko kwa misaada kunakuja wakati Korea ya kaskazini inajitayarisha kurusha satalite ambayo Marekani na washirika wake wanaiona kuwa ni kombora.

Senin, 16 Maret 2009

Israel kazi bado ipo...

ERUSALEM – Prime Minister-designate Benjamin Netanyahu's Likud Party has initialed a coalition agreement with an ultranationalist faction that brings its leader significantly closer to becoming foreign minister, a Likud party spokeswoman said Monday.

Avigdor Lieberman, who heads the right-wing Yisrael Beitenu party, has drawn accusations of racism for proposing that Israel's Arab citizens sign loyalty oaths or lose their citizenship. Although that plan is not likely to be implemented, his designation as foreign minister could harm Israel's international ties.

The appointment is not yet finalized, however. Likud spokeswoman Dina Libster said the coalition agreement included a provision that both sides were prepared to form a government that would include moderate partners, such as the Kadima Party of the current foreign minister, Tzipi Livni.

That wording leaves open the possibility that Livni might retain her current job if she were to join such an alliance. Local media reported over the weekend that Netanyahu has resumed overtures to recruit Livni.

The agreement with Yisrael Beitenu is the first Netanyahu has initialed on his way toward setting up a coalition of hawkish and Orthodox Jewish parties.

The government taking shape would take a harder line on Palestinian and Arab issues than the outgoing administration of Prime Minister Ehud Olmert.

Netanyahu has criticized last year's U.S.-sponsored peace talks between Israel and the Palestinians, aimed at partitioning the land and establishing a Palestinian state. The talks made little progress, and on Sunday Olmert blamed the weak Palestinian government for the failure. In turn, Palestinian negotiators blamed Israel, citing expansion of West Bank settlements and hundreds of roadblocks in the West Bank.

Netanyahu favors focussing on efforts to bolster the Palestinian economy, leaving issues like borders, sovereignty and Israeli settlements for a later stage. In defiance of Israeli commitments to international plans, Netanyahu favors expanding Israel's West Bank Jewish settlements to allow for "natural growth," accommodating the growing families in the communities.

Palestinians reject that approach and have the backing of the new Obama administration. In a recent visit, Secretary of State Hillary Clinton said the goal of negotiations must be the creation of a Palestinian state living next to Israel in peace.

Though Lieberman now says he supports Palestinian statehood, he also believes such a state should include territory inside Israel containing heavily populated Arab areas. Such a plan could strip hundreds of thousands of Arabs of their Israeli citizenship, regardless of their feelings on the issue.

Speaking in Brussels, Belgium, before the Likud-Yisrael Beitenu accord was signed, Palestinian Foreign Minister Riad Malki said the emerging government was "anti-peace," adding, "We have to declare that sadly there is no partner on the Israeli side to negotiate with."

Netanyahu still needs to add several other parties to reach a majority in the 120-member parliament. In the election last month, his Likud won 27 seats, and Yisrael Beitenu adds another 15.

Kadima won 28 seats, but Netanyahu was chosen to form a government because a majority of members of parliament said they favored him over Livni as premier.

Netanyahu's negotiators are set to meet later Monday with a team from Shas, an ultra-Orthodox Jewish party with 11 seats in the parliament. If Kadima stays outside, Netanyahu is expected to try to bring in smaller hard-line parties like Jewish Home, National Union and United Torah Judaism, giving him a majority of 65.

But several of the parties have conflicting claims and agendas, and getting all of them to agree is not assured.

Minggu, 15 Maret 2009

Moscow kumekucha...Ni usiku wa marahaaa, Mwana FA Live in Moscow


Bingwa wa Mitikasi Mr. Kihiga, Mzee wa starehe Bw. Biboze na Mzee wa kuspend Mr. Kapilima pamoja na THE THOMCOM wamekuandalia usiku wa kukata na shoka, siku ya kuspend, siku ya kustarehe, siku ya kurusha roho, Mademu kibao, magentlemen wakunata, Ma-Dj maarufu pamoja na show toka kwa Msanii machachari nchini Mwana FA ndani ya jiji la Moscow.

Wapi na kwa namna gani, BOFYA HAPA

Usikose uhondo huu, tonge liko mdomoni mwako, uko tayari kumwachia mpita njia alitafune badala yako?...acha hizoooooo....fika ujionee mwenyewe..Kwa maelezo zaidi BOFYA HAPA

Ahahahahaaaa...Kwa mara ya Kwanza ndani ya jiji la Maraha kabisa, МОСКВА РОССИЯ 2009

Sabtu, 14 Maret 2009

Madagascar yawaka moto....Africa tutaendeleaje?

Madagascar yanyemelewa na mapinduzi

Madagascar yanyemelewa na mapinduzi
Wafuasi wa upinzani wakiwa mkutanoni mjini Antananarivo
Kiongozi wa upinzani nchini Madagascar, ameonya ataongoza maandamano makubwa hadi katika kasri la Rais wa nchi hiyo, iwapo rais huyo hatang'atuka madarakani.

Kiongozi huyo wa upinzani Andry Rajoelina, aliyejitokeza kutoka mafichoni na kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Antananarivo, amempa muda rais hadi siku ya Jumamosi jioni ajiuzulu kwa "unyenyekevu".

Viongozi wa upinzani wanaojaribu kuunda serikali yao kwa sasa wanashikilia ofisi ya Waziri Mkuu.

Tangu upinzani dhidi ya serikali ulipoibuka mwezi wa Januari, watu takriban 100 wamekwishapoteza maisha yao.

Taifa hilo ambalo ni kisiwa katika bahari ya Hindi, kwa muda wa wiki saba sasa limekuwa katika machafuko yaliyosababisha uporaji, upinzani na wizi, kukiwa na mzozo wa madaraka baina ya Rais Ravalomanana na Bwana Rajoelina.

Kiongozi wa upinzani ambaye alifutwa kazi ya umeya wa jiji mwezi uliopita, alijificha tangu tarehe 5 mwezi huu wa Machi baada ya vyombo vya usalama vilipojaribu kumkamata.

Jumat, 13 Maret 2009

Urgently.....

Wanafunzi wote mnatakiwa kujaza fomu za mikopo hadi march 31 ziwe zimeshafika bodi ya mikopo. Pia wanafunzi waliojiunga chuo kikuu cha urafiki Lumumba mwaka 2008/2009 wanatakiwa kuambatanisha vivuli vyao vya vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita pamoja na medical checkup walizofanya wakiwa Tanzania.

Habiri hizi zimeifikia The THOMCOM na mwandishi wetu kuwa wanafunzi waliojiunga chuoni hapo mwaka 2008/2009 hawatasainiwa fomu zao hadi wawasilishe vivuli hivyo jambo ambalo lingepaswa kufanywa kabla hawajatoka Tanzania.

Akiongea na The THOMCOM, msajili mkuu wa wanafunzi wa Kiafrika amesema kuwa wanafunzi waliojiunga na chuo hicho mwaka huu wa masomo wamesajiliwa kinyume cha sheria kwa kutohakiki vyeti vyao na matokeo ya afya zao wakati wakiwa Tanzania. Msajili huyo alionesha masikitiko yake kuwa hali hiyo imechangiwa pia na ahadi ya wizara ya Elimu na Ufundi stadi kuwa vivuli hivyo vingetumwa na wiara hiyo kwenda chuoni hapo kwani kwa desturi ya wanafunzi wanaojiunga na chuo kikuu cha urafiki Lumumba kwa mkataba wa serikali hupeleka vivuli vya vyeti vyao kupitia wizara ya Elimu

EDITOR, THE THOMCOM


moscow, 2009

Rabu, 11 Maret 2009

Wema Sepetu ameathirika


Wema Sepetu ameathirika

Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Anko Hashimu Lundenga, ameelezea kusikitishwa kwake na matukio yanayomkumba Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu (20) na kudai kuwa, ni vema Mnyange huyo akapimwa ili kujua endapo ameathirika na dawa za kulevya, hivyo kurahisisha zoezi la kumrekebisha...

Rais Mwinyi achapwa vibao....

RAIS Mstaafu wa serikali ya awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi,akihutubia maelfu ya waumini wa kiislamu katika sherehe za kuzaliwa kwa mtume Muhammad (S.A.W) katika ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo tukio la kupigwa kibao lilitokea


RAIS Mstaafu wa serikali ya awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, jana alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya mtu asiyejulikana kumfuata jukwaani wakati akihutubia na kumpiga kibao shavuni.

Mwinyi, ambaye alipata umaarufu wakati serikali yake ilipolegeza masharti ya kiuchumi na kisiasa hadi kuruhusu mfumo wa vyama vingi na kusababisha apachikwe jina la Mzee Ruksa,

alishambuliwa na mtu huyo jana majira ya saa 12:20 jioni wakati alipokuwa akihutubia Baraza la Maulid kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) lililohudhuriwa na waumini wengi wa dini ya Kiislamu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Shambulizi hilo lilitokea wakati Mwinyi akizungumzia masuala ya afya na hasa malezi bora ya wazazi kwa watoto na kusisitiza matumizi ya kinga wakati wa ngono, akimaanisha kondomu na ndipo alipojitokeza mmoja wa waumini aliyekuwa amevalia kanzu.

Mtu huyo alijifanya kama anataka kumsalimia Kaimu Mufti, Sheikh Suleyman Gorogosi.

Kwa kuwa imezoeleka katika shughuli za kidini kutawaliwa na amani, watu waliokuwa karibu na mtu huyo hawakuwa na shaka naye ndipo mtu huyo akarudisha mkono ghafla na kumpiga kibao Mzee Mwinyi.

"Sisi tulishangaa kuona yule jamaa akipanda jukwaani na kujifanya kama anasalimiana na Mufti. Lakini cha kushangaza tukaona akageuka na kumpiga kibao Mzee Mwinyi... sisi tulishikwa butwaa," alisema Hussein Kauli mmoja ya watu waliohudhuria sherehe hizo.

Baada ya tukio hilo, Kaimu Mufti wa Tanzania, Alhaj Suleyman Gorogosi alimuomba radhi rais huyo wa awamu ya pili akisema kwamba kijana aliyefanya tukio hilo ni mtu mwenye upungufu wa akili.

Akaongezea kwamba kijana huyo huwa anaonekana katika shughuli mbalimbali za kidini na huwa anashiriki, lakini matukio yake yote mara nyingi yamekuwa ni ya kipunguani.

Naye sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa alitumia fursa hiyo kumuomba radhi mzee Mwinyi akisema kuwa kitendo hicho kimemsikitisha kila Muislamu na kwamba hakikutarajiwa.

"Ni fedheha kubwa imetupata kwa mtu kumkabili mtu tunayemheshimu na tena mwenye hadhi kubwa namna hii katika jamii haipendezi. Tunahisi suala hili limepangwa na kundi la watu wenye malengo yao kwa sababu kijana yule asingeweza kujiamini kiasi kile. Ana kundi kubwa linamuunga mkono," alisema Sheikh Mussa baada ya kutoka ndani ya ukumbi.

Hata hivyo, Sheikh Mussa hakueleza ni kundi gani analihisi kuwa liliandaa mpango huo wa kumshambulia rais mstaafu, ambaye amekuwa akihudhuria hafla nyingi za Kiislamu.

Alisema kuwa anamfahamu kijana huyo kwa sura lakini hatambui jina lake kwani amekuwa akishiriki katika shughuli mbalimbali za kidini na mara zote hizo amekuwa akifanya mambo ya kipunguani.

Hata hivyo muda mfupi baadaye askari polisi wakishirikiana na walinzi wa Mzee Mwinyi walimbeba mtuhumiwa huyo na kumuadhibu na baadaye kumpeleka kituo cha polisi.

Baadaye, Mzee Mwinyi aliendelea na mawaidha yake akisisitiza masuala mbalimbali, likiwemo la Waislamu kutunza afya zao na kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi ambao umeleta madhara makubwa katika jamii.

Sudan yatafuta uwezekano wa kubatilisha waranti ya kumkamata Rais Bashir

Sudan imesema,inachunguza iwapo waranti iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC kumkamata Rais Omar al-Bashir,itaweza kubatilishwa au kuahirishwa.

Hiyo ni ishara ya kwanza kuwa Sudan inashughulikia suala hilo. Hatua kama hiyo haimbatani kabisa na matamshi ya kejeli ya Rais Omar al-Bashir kupuuza waranti iliyotolewa na Mahakama ya Kiamatifa ya Uhalifu ikimtuhumu kuhusika na mauaji katika jimbo la Darfur, magharibi ya Sudan. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Ali Al-Sadig alipozungumza na shirika la habari la Reuters alisema,maafisa wa Sudan huenda wakalifikisha suala la waranti hiyo katika Mahakama ya Kimataifa ya Sheria na kuwaomba washirika wake washinikize kuiahirisha kesi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Amesema,majadiliano yanafanywa pamoja na China, Urusi na Libya-nchi wanachama katika Baraza la Usalama. Nchi hizo zimeshaeleza upinzani wake kuhusiana na waranti ya ICC.Sudan pia imearifiwa na Urusi na China kuwa mataifa ya magharibi yaliyosimama kidete kuipinga Khartoum pale waranti ya kumkamata Rais Bashir ilipokuwa ikitayarishwa,sasa huenda zikawa tayari kuijadili kesi hiyo.

Juma lililopita wanadiplomasia walisema,Uingereza,Ufaransa na Marekani, wote wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama,huenda wakaunga mkono pendekezo la kuiahirisha waranti hiyo,ikiwa maendeleo dhahiri yatapatikana huko Darfur na yatafanywa majadiliano thabiti ya amani. Kwa maoni ya baadhi ya wachambuzi, serikali ya Sudan huenda ikahisi kuwa inatengwa pole pole kwani haikuungwa mkono hivyo na nchi za Mashariki ya Kati.Kwa upande mwingine wachambuzi wanasema,waranti hiyo huenda ikachochea machafuko zaidi katika jimbo la Darfur ambako vikosi vya amani vinajikuta katikati ya mgogoro huo.

Mahakama ya Kimataifa ya Sheria ni taasisi iliyo tofauti na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu,licha ya kuwa zote mbili zipo The Hague nchini Uholanzi.Kazi mojwapo kuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Sheria ni kusuluhisha migogoro inayohusika na sheria.Migogoro hiyo hufikishwa hupelekwa huko na wanachama wa Umoja wa Mataifa.Wataalamu wa kimataifa wanasema,si chini ya watu 200,000 wameuawa huko Darfur,wakati Khartoum ikisema ni watu 10,000 waliopoteza maisha yao.Mgogoro huo ulianza mwaka 2003 baada ya waasi,hasa wale wasio na asili ya Kiarabu waliposhika silaha kupambana na serikali ya Khartoum.