Jumat, 13 Maret 2009

Urgently.....

Wanafunzi wote mnatakiwa kujaza fomu za mikopo hadi march 31 ziwe zimeshafika bodi ya mikopo. Pia wanafunzi waliojiunga chuo kikuu cha urafiki Lumumba mwaka 2008/2009 wanatakiwa kuambatanisha vivuli vyao vya vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita pamoja na medical checkup walizofanya wakiwa Tanzania.

Habiri hizi zimeifikia The THOMCOM na mwandishi wetu kuwa wanafunzi waliojiunga chuoni hapo mwaka 2008/2009 hawatasainiwa fomu zao hadi wawasilishe vivuli hivyo jambo ambalo lingepaswa kufanywa kabla hawajatoka Tanzania.

Akiongea na The THOMCOM, msajili mkuu wa wanafunzi wa Kiafrika amesema kuwa wanafunzi waliojiunga na chuo hicho mwaka huu wa masomo wamesajiliwa kinyume cha sheria kwa kutohakiki vyeti vyao na matokeo ya afya zao wakati wakiwa Tanzania. Msajili huyo alionesha masikitiko yake kuwa hali hiyo imechangiwa pia na ahadi ya wizara ya Elimu na Ufundi stadi kuwa vivuli hivyo vingetumwa na wiara hiyo kwenda chuoni hapo kwani kwa desturi ya wanafunzi wanaojiunga na chuo kikuu cha urafiki Lumumba kwa mkataba wa serikali hupeleka vivuli vya vyeti vyao kupitia wizara ya Elimu

EDITOR, THE THOMCOM


moscow, 2009

Tidak ada komentar:

Posting Komentar