Rais wa Sudan afika Misri
Na Tedy Mwarabu
Rais wa Sudan Omar al-Bashir
Kiongozi wa Sudan anashtakiwa kwa makosa ya kihalifu chini ya mazingira ya kivita nchini Sudan
Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, amewasili nchini Misri.
Hii ni safari yake ya pili tangu waranti ya mahakama ya kimataifa ya ICC ya kutaka akamatwe kutolewa.
Nchi ya Misri haimo katika orodha ya mataifa ambayo yametia saini mkataba wa ICC.
Mataifa wanachama yanawajibika kumnasa yeyote yule ambaye hati ya kumkamata imetolewa dhidi yake, wanapoingia katika ardhi ya nchi hiyo.
Bw Bashir, ambaye alifanya ziara fupi siku ya Jumatatu nchini Eritrea, anatazamiwa kufanya mashauri na Rais Hosni Mubaraka wa Misri.
Kiongozi huyo wa Sudan anashtakiwa kwa makosa ya kihalifu katika mazingira ya kivita katika eneo la Darfur.
Bado haijafahamika wazi ikiwa rais Bashir ataendelea na mipango yake ya kuhudhuria mkutano wa mataifa ya Kiarabu utakaofanyika Doha, Qatar, kati ya tarehe 29-30 mwezi Machi.
Mamlaka ya juu zaidi ya kidini nchini Sudan, ambayo ni kamati ya wasomi wa Kiislamu, wiki hii ilimshauri asisafiri, kutokana na vitisho kutoka kwa maadui.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar