Kamis, 18 Desember 2008

JK:No kushinikiza kesi za mafisadi

Zile kesi zidi ya watuhumiwa wa rushwa zitaendelea kuendeshwa, kwa kutumia utaratibu pamoja na uangalifu kwa kukataa shinikizo la kuwapeleka watuhumiwa mahakamani.

Kauli hiyo ya kukataa shinikizo la kesi za mafisadi, ilitolewa na Rais Jakaya Kikwete, alipokuwa akizungumza na Watanzania waishio Msumbiji.

Alisema upelelezi unatakiwa kufanyika kwa umakini ili kuweza kupata ushahidi, pamoja na vielelezo sahihi kabla ya washitakiwa kufikishwa mbele ya mahakamani.

JK alisema hairuhusiwi mtu kupelekwa mahakamani kwa shinikizo la umma, kwani ni lazima ushahidi wa kutosha ukusanywe.

Alifafanua kwa kina na kusema kwamba baadhi ya watuhumiwa ni watu maarufu, ambao haitakuwa vizuri kuharibiwa sifa zao bila sababu.

Kwani baadhi ya wananchi wamepeleka orodha ya watu wanaodaiwa kuwa ni wala rushwa, na wanataka wachukuliwe hatua za haraka.

Mawaziri wawili wa zamani na Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Fedha, wameshashitakiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka.

Hao ni mawaziri wa zamani wa fedha, Basil Mramba na Daniel Yona, na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja, wanaotuhumiwa kutumia vibaya madaraka yao na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 11.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar