Jumat, 26 Desember 2008

Njama zafanyika kudhoofisha vyanzo vya habari vya The THOMCOM

The THOMCOM imepata taarifa rasmi zinazoonesha kuwa kuna mtu mmoja amejitahidi kufanya kazi ya kuwatafuta maripota wetu wa The THOMCOM ili kuwapa shuluba bila mafanikio. siku chache baada ya ripota wetu ajulikanaye kama JUMA MAMBOLEO KHASIM kutubrekisha habari moja toka shabalovskaya vhalafu akatubrekisha habari nyingine toka embassy, mtu mmoja ajulikaye kama JUMA KHASIM (sio ripota wetu juma mamboleo khasim) alivamiwa na watu wachache na kupata misukosuko, watu hao wakidhania kuwa mtu huyo (Juma Khasim aishie block 8) ndiye ripota wetu. Mdau huyo alivamiwa nyumbani kwake na watu hao kwa madai kuwa yeye ndiye pekee ajulikanaye kama juma khasim, kuhisiwakuwa ndiye aliyebrekisha habari hiyo. Baada ya kupata breaking news hizo za kupigwa kwa mdau huyo ambaye sio ripota wetu, The THOMCOM iliwasiliana na maripota wake wote na kuwaomba kutoa taarifa yoyote itakayoonesha hali ya tafurani.

Kutokana na Mdau huyo kupata shuluba hizo, The THOMCOM iko tayari kumchukulia hatua za kisheria mtu huyo aliyedhubutu kumvamia jamaa huyo na kumpa kichapo. The THOMCOM itatoa ushirikiano wake wote kuhakikisha kuwa jamaa huyo anaadhibiwa, ila kama mdau aliyepigwa atatoa malalamiko yake rasmi na kama Daktari atatibitisha kupigwa kwa mdau huyo. The THOMCOM inatoa salam za pole kwa mdau huyo aliyepata misuko suko hiyo, na inathibitisha kuwa huyo sio RIPOTA wa The THOMCOM.

The THOMCOM inatoa onyo kwa mtu yeyote atakayegundulika kukiuka haki zozote za maripota au mfuasi wake kuwa baada ya kudhibitisha ukiukwaji huo, hatua kamili kabisa za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kumpeleka mtu huyo mahakamani.

Imetolewa na mamlaka husika ya TANZANIA HIGH ORIENTED MASS COMMUNICATION (THOMCOM)

Tidak ada komentar:

Posting Komentar