Minggu, 14 Desember 2008

ANGALIA LIVE HOTUBA YA Mh. BALOZI KUHUSU WANAFUNZI WALIOKWISHA PEWA TICKET

katika kusherehekea sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika, Mh. Balozi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kaptain mstaafu Jaka Mwambi alitumia nafasi hiyo kuelezea masikitiko yake juu ya baadhi ya wanafunzi kutokana na utovu wa nidham. Katika hotuba yake iliyochukua zaidi ya dk 30, Mh. Balozi hakusahau kugusia hatua zilizochukuliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwafutia wanafunzi 5 udhamini wa serikali na kumsimamisha masoma mwanafunzi 1. wanafunzi hao 6 ambapo mmoja tayari alikwisha toroka baada ya kuchukua boom lake, walipewa ticket ikiwa ni pamoja na barua rasmi ya kuwaomba kuondoka nchini Russia hadi ifikapo tarehe 13/12/2008 muda ambao umekwisha malizika.

taarifa hii pamoja na video zimeletwa kwenu na Juma Khasim wa The THOMCOM


Tidak ada komentar:

Posting Komentar