Rabu, 10 Desember 2008

UPEKUZI,,,,,,,,,

kama The THOMCOM ilivyoahidi, itawaletea live sakata zima la kufutiwa dhamini wanafunzi kadhaa chuo kikuu Lumumba. Habari zilizoifikia The THOMCOM zinasema kwamba tayari ticket kwa ajili ya kuwapatia wanafunzi hao zimeshaandaliwa na siku yoyote watahitajika kuripoti wizarani.

Wakati huo huo The THOMCOM imepata habari kutoka katika chanzo cha kuaminika kuwa watu hao (sio wanafunzi tena) wapo kwenye mkutano (hadi kuandikwa kwa waraka huu saa 22.30) wakipanga shambulizi kali la mwisho. Inasemekana shambulio hilo litakuwa la aina yake na la kushtukia. haikufahamika mara moja ni shambulio la aina gani.

The THOMCOM imepata habari za kuaminika na kuhakikisha taarifa iliyotolewa na The THOMCOM kuhusu ufutiwaji wa udhamini ikiwa ni pamoja na uvunjwaji wa mkataba.

The THOMCOM inawatakieni sikukuu njema ya miaka 47 ya uhuru wa Tanganyika.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar