Imeandikwa na Mwandishi wa BBC
| | | | Mabomu yamedondoshwa Gaza | Ndege za kijeshi za Israel zimeshambulia vituo vya Hamas katika Ukanda wa Gaza. Watu walioshuhudia mjini Gaza wanasema takriban makombora ishirini yamerushwa katika mji huo. Radio ya huko pamoja na wauguzi wa Kipalestina wanakadiria watu waliouawa kufikia mia moja na arobaini, au zaidi. Mkuu wa polisi wa Gaza Tawfik Jaber anahofiwa kuwa miongozi mwa waliouawa. hakuna usalama Picha za televisheni zimekuwa zikionesha majeruhi wakipelekwa hospitali, huku kukiwa na ripoti kuwa vyumba vya kuwekea maiti vikiwa vimejaa. Mwandishi wa BBC mjini Gaza anasema watu walikuwa wakitafuta hifadhi, lakini hakuna mahala salama. Wakati huohuo, baraza la mawaziri la Israel lilikutana wiki hii kujadili jinsi ya kujibu mashambulizi wa makombora kutoka Palestina, yaliyoanza kurushwa baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas kufikia kikomo chake. mwanzo tu Msemaji wa kijeshi wa Israel Brigedia Jenerali Avi Benayahu amesema mashambulizi dhidi ya Gaza ni mwanzo tu, na kuwa jeshi litachukua hatua kulingana na hali ilivyo. Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amelaani mashambulizi ya anga ya Israel na kutoa wito wa kusitisha ghasia. |
Tidak ada komentar:
Posting Komentar