Rabu, 10 Desember 2008

nyepesi nyepesi....

Kuna uvumi unaoenezwa na wanafunzi waliofutiwa udhamini na serikali kuwa serikali pamoja na ubalozi umewaita na kuwapa ofa ya kuendelea kusoma ili waombe msamaha na wanafunzi hao kuchomoa. Kutokana na habari zilizofikia studio zetu, serikali wala ubalozi haukuwa na mawasiliano yoyote na wanafunzi hao, wala hawatafanya mawasiliano yoyote kama hayo. Habari hii inanikumbusha methali isemayo MFA MAJI HAACHI KUTAPA.

Imeoneka wazi kuwa uvumi huo unaoenezwa na watu hao ni njama ya kuwateka kiakili na kuwaathiri kisaikolojia wanafunzi waliojiunga chuo kikuu Lumumba mwaka 2008/2009 ili wawaunge mkono kwa matakwa yao binafsi.

Kutokana na maji kuwafikia shingoni wanafunzi hao wameivamia afisi moja chuoni hapa na kuwalazimisha maafisa wa afisi hiyo kuwasiliana na ubalozi ili kuhakikisha swala hilo ikiwa ni pamoja na kuomba habari zaidi hali iliyomfanya afisa mmojawapo kuamua kuwaachia afisi. Sambamba na hilo, wanafunzi hao wameomba chuo kiwaandikie barua ya kuonesha hawajafukuzwa shule, wala hawana kosa lolote. Swala hilo bado linafikiriwa na uongozi wa chuo.

Swali kwa waliooa tuu! HIVI KUNA MWANAFUNZI YEYOTE AMBAE AMESOMA CHUO KIKUU HADI KUFIKIA MWAKA MMOJA TUU AMALIZE ahitimu shahada yake, MWANAFUNZI HUYO AKIFUKUZWA chuo THEN AKAAMBIWA AKIOMBA MSAMAA ATARUHUSIWA KUIPATA DEGREE YAKE, ANAWEZA KUKATAA?

Nikiripoti toka Shabalovskaya, mimi ni Peter Zakayo wa The THOMCOM

.............................................................................

Tidak ada komentar:

Posting Komentar