Kamis, 22 Januari 2009

MMOJA AKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA FOREIGNERS MOSCOW RUSSIA. NI AFISA WA NGAZI YA KATI WA IDARA YA UPELELEZI YA RUSSIA. UCHUNGUZI KUENDELEA.....

mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tuhuma za mauaji ya wageni (skin head) yaliyofanyika katika maeneo ya chuo kikuu cha urafiki Lumumba juma moja lililopita. Mtu huyo anayesemekana kuwa ni afisa mwandamizi katika shirika la ujasusi la Urusi amekamatwa siku ya jumatano tarehe 21/01/2009 siku mbili baada ya kuuwawa kinyama wanafunzi watatu wa chuo kikuu cha urafiki Lumumba Moscow Russia Na kuuwawa kwa mtu mwingine toka cameroon katika maeneo ya chuo kikuu. Mtu huo na wenzake wameshukiwa na kuhusika kwao katika mauaji hayo na tayari wanashikiliwa na polisi (MILITSIA) kwa uchunguzi zaidi. hadi kuanza kwa mwezi february mwaka huu, wanafunzi wasiopungua watano wameshauwawa na wengine zadi ya ya kumi kujeruhuwa vibaya sana kutokana na UBAGUZI WA RANGI katika chuo kikuu cha Urafiki Lumumba. Hadi sasa chuoni hapo imetangazwa hali ya hatari kwa wanafunzi wote wageni kutoka nje hasa nyakati za jioni na usiku, pia wanafunzi wameshauriwa kutembea kimakundi ili kuepuka adha ya kudhalilishwa, kupigwa hata kufa.

Kutokana na taarifa zilizoifikia The THOMCOM siku ya leo ni kwamba vituo viwili vya Metro (BELYAEVO NA YUGO ZAPADNAYA) vimetekwa na wabaguzi wa rangi na hakuna uwezekano wa mgeni yeyote kukatiza maeneo hayo,. kutokana na hali hiyo kujitokeza, wanafunzi wanaosoma kozi za uandisi na ecology wamekutana leo katika kikao maalumu kilichoandaliwa na viongozi wa umoja wa wanafunzi wa Tanzaina kujadili njia za kuwasaidia wanafunzi hao kusafiri kutokana na kuwa katika kipindi cha mitihani.

hali ya wasiwasi na kutishiana maisha nchini RUSSIA imekuwa ikwavunja moyo wanafunzi wageni kiasi cha kukata Tamaa hivyo mataifa ya Dunia yanaomwa pia kusaidia kulinda usalama wa wageni hasa wanafunzi wanaoingia nchiniRussia kujipatia asomo.

Nikiripoti toka bwenini, mimi ni Osana Mafundisho wa The THOMCOM

............................................................

Tidak ada komentar:

Posting Komentar