Katika hali isiyokubalika, isiyo ya kawaida na ambayo tunaweza kuiita Utoto, THE THOMCOM imepata taarifa kuwa kuwa baadhi ya wageni (majina tunayo) waliohudhuria sherehe za siku ya kuzaliwa kwa NEEMA MWAMBI walidiriki kuiba baadhi ya vitu vilivyokuwepo katika eneo hilo, kufungua computer za reception za eneo hilo kinyume cha utaratibu na kuvuruga utaratibu uliokuwepo awali. Kana kwamba haitoshi, watu hao walidiriki pia kuingia vyumbani na kufungua mafriji, na kuchukua vitu vilivyokuwepo humo. Wengine walihamisha sukari, vinywaji binafsi vya familia na vitu vingine vingi ambavyo vilikuwa nje ya sherehe hizo. Familia ya Mh. Mwambi imesononeka sana na hali hiyo na familia hiyo isingependa kuona matendo kama hayo yanatokea tena.
Kwa wale ndugu zetu ambao walihusika kwa namna moja au nyingune (Majina tunayo) THE THOMCOM inawashauri kubadilika, kuthibitisha kuwa mmeshakuwa wakubwa, utoto ukae pembeni, elimu tuliyo nayo itumike zaidi katika maisha yetu ya kila siku.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar