Homa ya nguruwe yawashika karibu watu 3500
Na mwandishi wa THE THOMCOM Washington:
Maafisa wa idara ya afya wa Marekani wamethibitisha homa ya nguruwe imegharimu maisha ya mtu wa watatu katika jimbo la Washington.Mhanga huyo,bwana mmoja mwenye umri wa miaka 30,amefariki dunia wiki iliyopita kutokana na kile kinachotajwa kua" kuzidi utata virusi vya homa ya H1N1.Idadi ya watu walioambukizwa na homa ya nguruwe nchini Marekani imezidi takriban mara dufu ,wakipindukia watu 1600.Maafisa wa afya wanachungutza kesai nyengine 800 za watu walioam,bukizwa maradhi hayo.Kwa mujibu wa shirika la afya la kimataifa WHO,watu karibu 3500 kutoka nchi 29 wameambukizwa virusi vya homas ya nguruwe hadi wakati huu.Zaidi ya 50 kati yao wamefariki,na wengi wao ni kutoka Mexico.Kuna kesi nyengine iliyoripotiwa ya mtu aliyefariki dunia kutokana na homa ya nguruwe nchini Costa Rica.Wakati huo huo,nchi nne ,Japan,Australia,Panama na Argentina zimeliarifu shirika la afya la kimataifa,homa ya nguruwe imeshaingia katika nchi hizo.Barani Ulaya Norway imetangaza kwa mara ya kwanza wakaazi wake wawili wameambukizwa.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar