Bw Manuel anasifika kwa kuimarisha vyema uchumi wa Afrika Kusini. |
Bw Zuma ameahidi kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi, umasikini uliokithiri na uhalifu unaoongezeka, lakini akasisitiza kuwa hatawapendelea wafuasi wake.
Bw Gordhan alikuwa akifanya kazi katika idara ya kodi na amesifiwa kwa kuimarisha mapato ya serikali.
Baraza la Mawaziri Makamu wa rais: Kgalema Motlanthe Tume ya Mipango: Trevor Manuel Usimamizi na Tathmini: Collins Chabane Fedha: Pravin Gordhan Sheria: Jeff Radebe Ulinzi: Lindiwe Sisulu Afya: Aaron Motsoaledi Mambo ya Nje: Maite Nkoana-Mashabane Makazi: Tokyo Sexwale |
Akiwa mkuu wa kitengo cha taifa cha mipango, Bw Manuel sasa atakuwa na majukumu ya kupanga mikakati na kusimamia uratibu wa shughuli za idara za serikali.
Bw Manuel amesifiwa kwa kuongoza vyema uchumi wa Afrika Kusini kwa miaka 13, anaondoka wakati uchumi unayumba kote duniani.
Aaron Motsoaledi amepewa jukumu la kusimamia wizara nyeti ya Afya. Atakuwa na jukumu la kuongoza mapambano dhidi ya maradhi ya HIV na UKIMWI nchini humo.
Madaraka
Bw Zuma alichaguliwa na bunge kuwa rais baada ya chama cha African National Congress kushinda uchaguzi mkuu mwezi Aprili. Aliapishwa siku ya Jumamosi kuchukua hatamu ya kuongoza taifa la Afrika Kusini kama rais mpya.
Kiongozi huyo alikula kiapo mbele ya wageni waalikwa 5,000 na wafuasi wa ANC waliokusanyika kwenye majengo ya Muungano (Union Buildings) katika sherehe hizo mjini Pretoria.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar