Uhalifu wa mtandao wa internet umeigharimu Marekani dola milioni 8 |
Amesema kutoka sasa , mfumo wa kompiuta wa Marekani utathaminiwa kama chombo muhimu cha serikali.
Ametangaza kuundwa kwa ofisi ya Ikulu ya White house itakayohakikisha usalama wa internet , na akasema atateua mtu atakayeshughulika na visa vya uhalifu katika internet.
Serikali ya Marekani pamoja na taasisi za kijeshi zimeripoti kuingiliwa mara kadha na wahalifu wa internet katika miaka ya hivi karibuni.
Bwana Obama amesema kundi la al Qaeda na makundi mengine yanatatiza makabiliano dhidi ya uhalifu wa mtandao.
Amesema Marekani inategemea sana mifumo ya kompiuta na kwa hivyo uhalifu wa mtandao wa internet ni tishio kubwa nchi yake.
Katika mwaka 2007 pekee , makao makuu ya kijeshi ya Pentagon yaliripoti visa 44,000 vya kile kilichoelezewa kuwa uhalifu wa mtandao uliotekelezwa na wanajeshi wa kigeni , mashirika ya kijasusi na watu binafsi.
Ameeleza kwamba kulingana na utafiti , uhalifu wa mtandao umeigharimu Marekani zaidi ya dola bilioni 8 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Amesema ufanisi wa kiuchumi wa Marekani katika karne ya 21 utategemea usalama wa shughuli za mtandao wa internet.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar