ALIYEKUWA MSAJILI MKUU WA WANAFUNZI WATOKAO BARANI AFRICA MR. SLAVA, ANATARAJIWA KUONDOKA MAPEMA WIKI IJAYO TAYARI KWA KUANZA KAZI YAKE MPYA RASMI KAMA CONSULOR HUKO ADDIS ABABA ETHIOPIA. HABARI ZILIZOIFIKIA THE THOMCOM ZINASEMA KUWA SHAVU HILO NONO ALILIPATA MWANZONI MWA MWEZI ULIOPITA NA KWA MUJIBU WAKE YEYE MWENYEWE NI KUWA SHAVU HILO HALINA UHUSIANO NA KAZI ALIYOKUWA AKIIFANYA CHUONI HAPA WALA CHUO HAKIJAHUSIKA KWA NAMNA YOYOTE ILE KATIKA KUMPATIA SHAVU HILO. AKIZUNGUMZA NA THE THOMCOM OFISINI KWAKE MWISHONI MWA MWEZI ULIOPITA, MR. SLAVA ALISEMA ANATUMAINI KUWA ATAKAYECHUKUA NAFASI YAKE ATAKUWA KARIBU NA WANAFUNZI WATANZANIA KAMA YEYE MWENYEWE ALIVYOKUWA. ALIPOULIZWA KUHUSU MKATABA AMBAO YEYE NDIYE ALIYEFANIKISHA KUTIWA SAINI KWA MKATABA HUO, MR. SLAVA ALISISITIZA KUWA WANAFUNZI WANAOSOMA CHINI YA MKATABA HUO WASIWE NA WASIWASI WOWOTE KWANI MKATABA WAO HAPA CHUONI UNAHESHIMIWA PIA NA MAKUNDI YA KIMATAIFA. ALIPOULIZWA JUU YA KAZI ALIYOKUWA ANAFANYA NA KAMA ANGEPENDA KURUDI TENA KATIKA KAZI HIYO, MR. SLAVA ALIONESHA WASIWASI WAKE JUU YA SWALA HILO NA JINSI KAZI YAKE ILIVYOKUWA NGUMU NA ISIYO NA MAFAO YA KUTOSHA. KWA UPANDE WAKE THE THOMCOM INAMTAKIA SAFARI NJEMA, KAZI NJEMA NA KUMKARIBISHA TENA TANZANIA
imeanddikwa na THE THOMCOM
Tidak ada komentar:
Posting Komentar