Chama cha MDC Zimbabwe chagoma | |||||
Waziri mkuu wa Zimbabwe amesema chama chake kitajiengua kutoka serikali ya muungano mpaka masuala waliyokubaliana kuhusu kugawana madaraka yatimizwe. Morgan Tsvangirai amesema si kwamba MDC inajitoa rasmi lakini haitoendelea kushirikiana na chama cha Rais Robert Mugabe cha ZANU-PF. Amesema hatua hiyo imeshinikizwa na kutiwa kizuizini kwa kiongozi mwandamizi wa MDC, Roy Bennet kwa shutuma za kuhusika na ugaidi. Shirika la habari la AFP limemnukuu Tsvangirai akisema kuwa Zanu-PF si washirika wanaoaminika. |
Jumat, 16 Oktober 2009
bora ya Mugabe
Langganan:
Posting Komentar (Atom)
Tidak ada komentar:
Posting Komentar