Uchaguzi wa bunge nchini Niger unaendelea licha ya kususiwa na upande wa upinzani na licha ya miito ya jumuia za kimkoa na kimataifa kumsihi rais Mamadou Tandja aakharishe uchaguzi huo.
Idadi ya wapiga kura ilikua ndogo kabisa vituo vya uchaguzi vilipofunguliwa leo asubuhi.
Uchaguzi huo wa kabla ya wakati umelengwa kuimarisha madaraka ya rais Mamadou Tandja,kanali zamani aliyeingia madarakani kupitia avituo vya upigaji kura mnamo mwaka 1999.
Mhula wa pili wa madaraka ya rais Tandja unamalizika december 22 ijayo,lakini mwanajeshi huyo wa zamani amejifungulia njia ya kusalia madarakani kwa miaka mitatu zaidi baada ya kuitisha kura ya maoni Agosti nne mwaka huu.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar