Rabu, 07 Oktober 2009

wapinzani wa kisiasa kisiwani humo wamefikia muafaka wa nafasi za uwaziri katika serikali mpya ya muungano.


Madagascar wakubaliana kuhusu serikali ya mpito.
Antananarivo.
Wapatanishi wa kimataifa wanasema kuwa mahasimu wa kisiasa nchini Madagascar wamekubaliana kuhusu serikali ya mpito kufuatia miezi kadha ya mvutano wa kisiasa.
Chini ya makubaliano hayo, ambayo yanapaswa kutiwa saini rasmi, Andry Rajoelina atabaki kuwa rais wa mpito na Emmanuel Rakotovahiny atakuwa makamu wa rais.
Eugene Mangalaza atachukua wadhifa wa waziri mkuu. Mjumbe maalum wa umoja wa Afrika nchini Madagascar amesema kuwa makubaliano hayo yanaashiria mwanzo wa kurejesha utaratibu wa kikatiba katika taifa hilo lililoko kisiwani katika bahari ya Hindi.
Mkutano wa jana Jumanne wa kundi la kimataifa linalofanya mashauriano ulikuwa ni juhudi za mwisho kuweza kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itatayarisha uchaguzi mpya wa rais pamoja na uchaguzi wa bunge kabla ya mwaka 2010.
Madagascar imekuwa katika mkwamo wa kisiasa tangu pale Rajoelina akiungwa mkono na jeshi alipomuondoa madarakani rais Marc Ravalomanana March 17 mwaka huu.



Maafisa waliopo katika mazungumzo ya kugawana madaraka huko Madagascar wamesema wapinzani wa kisiasa kisiwani humo wamefikia muafaka wa nafasi za uwaziri katika serikali mpya ya muungano.
Taarifa hizo zimetolewa baada ya kuwepo na majadiliano kwa wiki kadhaa yaliyokusudia kumaliza mgogoro wa kisiasa ulioanza mapema mwaka huu.
Katika makubaliano hayo, Andry Rajoelina anaendelea kuwa rais wa kisiwa hicho.
Bw Rajoelina alimwondosha aliyekuwa rais wa kisiwa hicho Marc Ravalomanana mwezi Machi akiungwa mkono na jeshi la kisiwa hicho.
Kuondoshwa kwa Bw Ravalomanan kulitokea miezi kadhaa baada ya kuwepo na maandamano ya kuipinga serikali yake.


HABARI MPYA
Waziri wa Somalia ashikwa Uganda
Wakenya wajiandaa na ghasia 2012
Serikali ya Muungano yaiva Madagascar

Tidak ada komentar:

Posting Komentar