Ghana mabingwa wa dunia vijana | |||||
Timu ya Ghana ikiwa imesalia na wachezaji 10 uwanjani ilifanikiwa kuinyuka Brazil katika fainali ya ubingwa wa dunia wa michuano ya vijana walio chini ya umri wa miaka 20. Ghana, waliompoteza Daniel Addo aliyetolewa nje kwa kadi nyekundu, walicheza soka maridadi ya kujihami kuwanyima ubingwa Brazil waliokuwa wakipewa nafasi ya kutwaa taji hilo la dunia kwa vijana. Mechi hiyo iliyofanyika Cairo International Stadium, ilimalizika 0-0 katika muda wa nyongeza na Brazil ilikiona cha moto wakati Alex Teixeira alipokosa goli la wazi. Emmanuel Agyemang-Badu alifunga goli la ushindi kwa Ghana na kuifanya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kubeba kombe hilo. Pande zote mbili zilikosa mikwaju miwili ya penati kati ya mitano na kuongeza msisimko wa mechi hiyo, hatimaye ikaingia katika hatua ya mikwaju ya nyongeza ndipo Badu alipoipatia Ghana kile kilichokuwa kikisubiriwa na waafrika wengi. |
Sabtu, 17 Oktober 2009
Ghana mabingwa wa dunia vijana
Langganan:
Posting Komentar (Atom)
Tidak ada komentar:
Posting Komentar