Ndesamburo anunua helkopta mbili za kampeni Chadema | |||||||
 Boniface Meena, Moshi  MBUNGE wa Moshi Mjini,Philemon Ndesamburo(Chadema), amenunua helkopta mbili kwa ajili ya kukisaidia chama hicho katika kampeni za chaguzi mbalimbali hapa nchini.  Moja ya helkopta hizo tayari iko hapa nchini na nyingine itawasili Jumatatu (kesho) na tayari mbunge huyo ameshapata vibali vya kuziruhusu helkopta hizo kutumika hapa nchini.  Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Ndesamburo alikiri kuwa amenunua helkopta hizo, ili kukipunguzia chama chao gharama kubwa za kukodi wakati wa kampeni.  Hatua hiyo ni kubwa zaidi kwa Chadema, chama ambacho kimekuwa kikijitahidi kujiimarisha na kuongeza nguvu hasa wakati wa uchaguzi. Tangu mwaka 2005 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Freeman Mbowe alipogombea urais kwa mara ya kwanza, chama hicho kilitumia helkopta ya kukodi. Hata katika baadhi ya chaguzi ndogo za ubunge zikiwemo za jimbo la Busanda na Tarime, chama hicho kilitumia helkopta za kukodi kwa ajili ya kufanyia kampeni. Lakini safari hii, chama hicho kimeamua kumiliki helkopta yake huku Ndesamburo akisisitiza: “Vibali vyote nimeshapata kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga na vile vile vya kuitoa hiyo moja Nairobi na kuifikisha hapa Jumatatuâ€.  Alisema kuwa helkopta hizo zitaanza kufanya kazi katika kampeni za serikali za mitaa katika majimbo yote ya Mkoa wa Kilimanjaro na baadaye katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.  Kwa mujibu wa habari zilizopatikana ni kuwa Chadema imesimamisha wagombea zaidi ya robo tatu katika kila jimbo mkoani Kilimanjaro.  Katika Jimbo la Moshi Mjini, chama hicho kimesimamisha wagombea 60 na Jimbo la Rombo kimesimamisha wagombea 52.  Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo huku idadi ya wapigakura ikiwa ndogo kinyume na matarajio. Hali hiyo imesababisha baadhi ya vyama kujipanga kikamilifu ili kuhakikisha wanakwepa kile wanachoita hujuma dhidi ya CCM. Uchaguzi huo ni muhimu kwa vyama vya siasa kujipatia mtaji na kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ambao unatarajiwa kuwa na mchuano mkali. Viongozi wa serikali za mitaa wana nguvu na ushawishi mkubwa wa kimaamuzi katika uchaguzi mkuu wa wabunge na Rais, kwani wapigakura wengi wako kwenye maeneo yao. Pia ngazi ya uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu katika maamuzi ya maendeleo ya nchi kutokana na watu wengi kuishi vijijini ambako pamoja na mambo mengine kuna shughuli nyingi muhimu za uchumi hasa kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa taifa. |
Minggu, 18 Oktober 2009
Ndesamburo anunua helkopta mbili za kampeni Chadema
Langganan:
Posting Komentar (Atom)
Tidak ada komentar:
Posting Komentar