Selasa, 17 Februari 2009

Makazi ya rais yashambuliwa E Guinea


Sehemu ya kitongoji mji mkuu Malabo
Makazi ya Rais wa Equatorial Guinea yashambuliwa
Kundi la watu waliokuwa na silaha, wamefanya jaribio la kuyashambulia makazi ya rais katika mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo.

Msemaji wa serikali Jeronimo Osa ameliambia shirika la habari la Hispania Efe kwa njia ya simu kwamba washambuliaji hao hatimaye walifurushwa.

Wizara ya mambo ya nje ya Hispania, nchi iliyowahi kuitawala Equatorial Guinea imesema serikali ya nchi hiyo imekanusha kuwa kulikuwa na jaribio la mapinduzi na kuwashutumu washambuliaji hao kwa kufanya uhalifu.

Rais Teodoro Obiang Nguema wa Equatorial Guinea hakuwepo katika makazi yake rasmi mjini Malabo wakati wa shambulio hilo.

Kwa miongo kadha nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta imekuwa ikikabiliana na majaribio ya kuipindua.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar