Sabtu, 30 Mei 2009

Mohammed Dewji amkana Juma Kaseja

Mohammed Dewji amkana Juma Kaseja
Kocha mpya wa African Lyon Eduardo Filipe Almeida(katikati) akitambulishwa kwa waandishi wa habari na Mkurugenzi wa timu Mohamed Dewji(kulia) katika halfa fupi jijini jana.
Na Mwandishi Wetu

AFRICAN LYON imemtambulisha kocha wake mpya Mreno Eduardo Filipe Almeida ambaye atainoa timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara huku ikisema imejitoa katika suala la kumtaka Juma Kaseja.

Akimtambulisha kocha huyo kwa waandishi wa habari jana katika ofisi zake jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu, Mohamed Dewji alisema kocha huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kufundisha klabu hiyo.

Alisema Mreno huyo alishawahi kufundisha kikosi cha vijana wa umri chini ya miaka 13 na 16 katika timu kongwe za Ureno za Benfica na Porto kabla ya kupata mkataba Hongkong. Katika hatua nyingine Dewji amekanusha madai kuwa timu hiyo imemsajili kipa wa Yanga, Juma Kaseja.

Dewji alikiri kufanya mazunguzmzo na kipa huyo lakini hawaafikiana naye kwa madai kuwa dau alilotaka lilikuwa ni kubwa mno.

Dewji alisema kuwa timu yake inahitaji kipa kijana zaidi ambaye wanaweza kumtumia zaidi ya misimu mitatu ya ligi na hivyo umri wa Kaseja pia umekuwa ni kikwazo cha wao kumhihitaji.

" Tunao vijana wengi wa umri mdogo ambao walicheza vizuri wakati wa mechi za kutafuta kupanda daraja. Tulihitaji wachezaji wachahe wenye uzoefu ili kuwapa changamoto vijana wetu wachanga na ndiyo maana tukamfuata Kaseja," alisema Dewji.

Hata hivyo Dewji hakuwa tayari kueleza Kaseji alihitaji kiasi gani ili asajiliwe na klabu hiyo ya African Lyon yenye makazi yake Mbagala wilayani Temeke.

Katika hatua nyinine Dewji alisema kuwa ujenzi wa uwanja wa kisasa katika eneo la Mbagala tayari umeshaanza katika hatua za awali na utakuwa na nyasi za bandia.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar