Sabtu, 30 Mei 2009

What happened to Mau U?

Barcelona bingwa mpya barani Ulaya

Mabingwa wapya wa soka barani Ulaya
Barcelona mabingwa wa soka Ulaya
Jaribio la Manchester United kuweka historia ya kuwa klabu ya kwanza kutetea ubingwa wake wa Ulaya, lilikwama baada ya kuchapwa katika uwanja wa Stadio Olimpico, Rome.

Matumaini ya kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson kurudia kile alichofanya dhidi ya Chelsea mwaka jana yaliyeyuka walipofungwa na Barcelona mabao 2-0 huku mshambuliaji wa Argentinas Lionel Messi akisumbua ngome ya Manchester United.

United ilianza pambano hilo kwa kishindo kikubwa, huku dalili zikionekana za kutetea ubingwa wao, huku Cristiano Ronaldo akiisumbua ngome ya Barcelona na kuwafanya Barcelona kubabaika.

Lakini mara tu baada ya Samuel Eto'o kufunga bao la kwanza katika dakika ya 10 kipindi cha kwanza, kwa kumponyoka Nemanja Vidic, hali ya mchezo ikabadilika na Barcelona wakawa wanamiliki mchezo na kufuta matumaini ya Manchester United kuongeza kikombe kingine zaidi ya kile cha Ligi Kuu ya England.

Barcelona walionekana kumiliki kila idara na hasa sehemu ya katikati ambapo Andres Iniesta na Xavi wakitawa.

Ilikuwa ni Barcelona tena walioweza kupachika bao la pili kupitia kwa Lionel Messi kwa kichwa baada ya kuwekewa mpira wa juu na Xavi, katika dakika ya 25 ya kipindi cha pili.

Kwa ushindi huo sasa Barcelona wamejiongezea kikombe cha tatu msimu huu baada ya kushinda ligi ya Uhispania- La Liga pamoja na kombe la Hispania.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar