Sabtu, 10 Oktober 2009

hali sii mbaya sana MOSCOW,. mshiko umewasili wa kutia matumaini japo bado haifahamiki kama unaweza kutosha kukidhi mahitaji yote ya student


asilimia kubwa ya wanafunzi Moscow Russia wameanza kupata fedha zao za kujikimu. swali linakuja kama hela hiyo itaweza kukidhi mahitaji yote ya mwanafunzi hapa Moscow. Hii ni kutokana na mfumuko mkubwa sana wa bei na uwezekano wa kuporomoka vibaya kwa dola. hali ya kuporomoka kwa dola imeanza kujitokeza tena na kutokana na wataalam na watabiri wa uchumi, ni kwamba dola inatarajiwa kuanguka ifikapo mwisho wa mwaka huu. Kinyume na matarajio ya wengi, fedha iliyo wasili ni kiasi kilekile ambacho kiliwasili mwaka jana. Ikizungumza na wanafunzi mbalimbali kwa nyakati tofauti, The THOMCOM imebaini kuwa wanafunzi wengi hawajaridhika na kiasi hicho, kutokana na ukweli wa hali ya mambo n ilivyo ikiwa ni pamoja na kupanda kwa bei za PANGO. kwa ujumla, kwa sasa hali sii mbaya, ila wasiwasi wa wengi ni kwamba, uwezekano wa kuishiwa kabla ya mwaka huu wa masomo 2009/2010 kuisha ni mkubwa (zaidi ya asilimia 60) ikizingatiwa kuwa hela zingine zijazo kwa kawaida ya bodi hutumwa kwa kuchelewa sana.

Mhariri, THE THOMCOM

Tidak ada komentar:

Posting Komentar