Rabu, 07 Oktober 2009

Waziri wa Somalia ashikwa Uganda


Sheikh Siad aliwahi kuwa mbabe wa kivita nchini Somalia
Jeshi la Uganda limesema naibu waziri wa ulinzi wa Somalia ametiwa kizuizini na majeshi ya usalama ya Uganda wakati akielekea mjini Kampala.
Sheikh Yusuf Mohamed Siad, aliyekuwa mbabe wa kivita wa Kiislam anayejulikana kama Inda'ade, alikamatwa wakati alipoenda kutembelea familia yake mjini hapo.
Msemaji wa jeshi la Uganda Luteni Kanali Felix Kulayigye ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa waziri huyo amekuja "kwa sababu zisizo wazi na hivyo ikabidi tumfuatilie."
Uganda imepeleka wanajeshi wake wengi katika jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika nchini Somalia.
Hapo awali maafisa wa serikali ya Somalia na ndugu zake Bw Siad walisema wanaamini alikuwa ametekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha.
Hata hivyo, balozi wa Somalia nchini Uganda baadae alithibitisha kwa Reuters kwamba anazo taarifa za waziri huyo kuzuiwa na Uganda.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar