Kamis, 30 April 2009

Mamia wajeruhiwa na mlipuko Tanzania

Zaidi ya watu 300 wangine wakiwa na majeraha makubwa, wanaendelea kutibiwa, siku moja baada ya milipuko ya mabomu kutokea nje Dar es Salaam nchini Tanzania.

Maofisa wa serikali wa nchi hiyo wanasema idadi ya watu waliokufa imeongezeka na kufikia watano na huenda ikaongezeka zaidi. Wanajeshi watatu inaarifiwa hawajulikani walipo.

Uchunguzi unaendelea wa kujua chanzo cha milipuko hiyo iliyotokea kando ya kambi ya jeshi kwenye ghala la silaha nje ya jiji la Dar es Salaam.

Mamia ya watoto ambao walikimbia kwa hofu eneo la Mbagala kwenye lenye ghala hilo la kuhifadhia silaha inaarifiwa hawajulikani walipo.

Rais Jakaya kikwete ametembelea eneo lilipotokea milipuko hiyo, siku moja baada ya kadhia hiyo iliyoleta hofu miongoni mwa wananchi wa Dar es Salaam wakifikiria kumetokea shambulio jingine la kigaidi kama lililotokea katika ubalozi wa Marekani mwaka 1998 jijini Dar es Salaam.

Mwandishi wa BBC Vicky Ntetema ametembelea kambi ya muda ya shirika la msalaba mwekundu nje ya jiji la Dar es Salaam maalum ya kuwaunganisha wazazi waliopotelewa na watoto wao.

Amesema vijana 250 walikuwepo katika kambi hiyo asubuhi ya Alhamisi na wachache bado hawajulikani.

Lakini wazazi wengi waliotembelea kambi wamesema watoto wao bado wajulikani walipo na kuna ripoti kwamba watoto 750 bado hawajaonekana.

Mashuhuda wamesema watoto kadha waliokuwa wamehamanika walizama katika mto ulifurika karibu na eneo la tukio.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar