Kamis, 02 April 2009

waliomuua Luck Dude wafungwa maisha

Marehemu Lucky Dube
Waliomuua Lucky Dube wafungwa maisha
Jaji wa Afrika Kusini amewahukumu watu watatu kifungo cha maisha jela baada ya kuwatia hatiani kwa kumuua mwanamuziki maarufu wa reggae Lucky Dube mwaka 2007.

Lucky Dube aliyekuwa na umri wa miaka 43, alipigwa risasi na watu hao watatu katika jaribio la kumuibia gari lake katika kitongoji kimoja cha mjini Johannesburg, tukio lililoleta hofu kwa taifa hilo.

Jamaa wa Lucky Dube walitokwa machozi na baadae wakashangilia baada ya kutolewa hukumu hiyo.

Mwandishi wetu Anna Kibali akiwa nje ya mahakama kuu ya South Gauteng anasema wanamuziki pamoja na mashabiki walikusanyika nje ya mahakama hiyo kuonesha mshikamano wao.

Mahakama hiyo ilielezwa kuwa washtakiwa hao watatu, walifikiria mtu waliyekuwa wakimpora gari alikuwa raia wa Nigeria na kamwe hawakufahamu waliyemuua alikuwa Lucky Dube hadi waliposoma magazetini siku iliyofuatatu hao watatu.

Moja ya mabango nje ya mahakama hiyo kwa mujibu wa mwandishi wetu lilikuwa likisomeka "Lucky Dube hafanani na Mnigeria; bali yeye ni Mwafrika."

Mahakama hiyo pia imewahukumu Sifiso Mhlanga, Julius Gxowa, na Mbuti Mabe kifungo cha miaka 15 kila mmoja kwa kufanya jaribio la kupora gari la Lucky Dube.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar