Sabtu, 25 April 2009

Matokeo rasmi ANC yashinda kwa kishindo

Na mwamdishi wetu, Johannesburg

Rais Kgalema Motlanthe akimpongeza kiongozi wa ANC Jacob Zuma
ANC yashinda uchaguzi licha ya kutopata wingi wa kura wa theluthi mbili
Matokeo rasmi ya mwisho yanaonesha chama tawala cha ANC nchini Afrika Kusini, kimeshinda uchaguzi mkuu lakini kimeshindwa kupata theluthi mbili ya kura kwa ajili ya kurekebisha katiba.

Kwa mujibu wa maofisa wa tume ya uchaguzi chama cha ANC kimezoa asilimia 65.9 kutokana na kura milioni 17, upande wa chama cha Democratic Alliance kina asilimia 16.6 ya kura huku chama cha Congress of the People (Cope) 7.42 kimejipatia asilimia 7.4.

Chama cha ANC hata hivyo kimepoteza jimbo la Western Cape ambalo limenyakuliwa na chama cha upinzani cha Democratic Allience.

Theluthi mbili ya kura ni muhimu katika bunge kwa ajili ya kubadilisha katiba.

Matokeo hayo yanatoa nafasi kwa kiongozi wa ANC Jacob Zuma kuwa rais mpya wa Afrika Kusini wakati bunge litakapokutana.

Wafuasi wa ANC wamekuwa katika sherehe nchi nzima huku wakisubiri matokeo rasmi kutangazwa.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar