Kamis, 05 November 2009

Mgogoro zimbabwe


Mgogoro wa Zimbabwe wajadiliwa
Wapatanishi wa kusini mwa Afrika wanatarajia kuanza mazungumzo nchini Msumbiji kwa nia ya kuzuia kuporomoka kwa serikali ya muungano ya Zimbabwe.

Serikali hiyo imekuwa na mgogoro tangu waziri mkuu Morgan Tsvangirai alipoanza kugomea vikao vya bunge.

Bw Tsvangirai anapinga namna rais Robert Mugabe anavyotekeleza mpango wa kugawana madaraka.

Serikali ya Zimbabwe pia ipo katika uangalizi kwenye mkutano wa kimataifa nchini Namibia unaohusu usimamizi wa mauzo ya almasi.

Mkutano huo unajadili aidha kuitoa Zimbabwe katika mpango huo kufuatia madai kwamba polisi na jeshi walihusika kuvunja haki za binadamu kwenye mgodi wa almasi wa Marange, penye utajiri mkubwa wa madini hayo duniani.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar