Sabtu, 14 November 2009

Obama ataka uchunguzi ufanyike

Rais wa Marekani Barack Obama ametoa amri ya uchunguzi kufanywa, wa jinsi mashirika ya kijasusi yalivyo shughulikia taarifa za afisa wa jeshi anayedaiwa kuua watu 13.

Hatua hiyo imekuja baada ya mamlaka za kijasusi za Marekani kuweka wazi kuwa walifahamu kwamba Meja Hasan alikuwa akiwasiliana na mtu anayeunga mkono kundi la al Qaeda.

Watu 13 walikufa katika shambulio lililotokea kwenye kambi ya jeshi ya Fort Hood, Texas.

Meja Hasan alipigwa risasi na polisi, na amelazwa hospitalini. Ameshitakiwa kwa makosa 13 ya mauaji.

Hata hivyo bado hajakutana na wachunguzi.

Imeelezwa kuwa Meja Hasan hakufurahishwa na uwezekano wa yeye kupelekwa nchini Afghanistan.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar