Wanafunzi 75 kuburuzwa mahakamani kwa kufoji vyeti. 8 kati yao ni kutoka chuo kikuu cha urafiki LUMUMBA
kwani kutoka ni lazima mtu aende chuo kikuu?
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), inatarajia kuwaburuza mahakamani wanafunzi 75 wa elimu ya juu wanaosoma nchini na nje ya nchi baada ya kugundulika kughushi vyeti na kuidanganya bodi ili wapatiwe mikopo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, George Nyatega alitoa taarifa hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliyofanyika mjini Moshi jana kwa lengo la kuelezea maoni waliyoyapokea kutoka kwa wateja wao mkoani Kilimanjaro.
Alisema wanafunzi hao ni pamoja na wanaosoma nchi za nje zikiwamo Algeria na Urusi waliofanya hivyo kwa lengo na kutaka mikopo ili waendelee na masomo. Alisema pamoja na kupandishwa kizimbani, wanafunzi hao watafutiwa mikopo.
Waliopo nje watarejeshwa nchini ili kuwawezesha wanafunzi wengine wenye sifa kupatiwa mikopo hiyo. Nyatega alisema katika uchunguzi wao wa awali umebaini wanafunzi saba walioko Algeria na wengine wanane walioko Urusi, wamefanya udanganyifu huo.
Kwa upande wa walioghushi kutoka vyuo vya ndani, wanafunzi 15 ni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Chuo cha Ushirika na Biashara cha Moshi (MUCCoBS), wamegundulika wanafunzi 45 walioghushi vyeti. Mkurugenzi huyo alisema taarifa nyingi za wanafunzi wanaodai kuwa wametoka katika familia duni siyo za kweli.
Aliwataka wanafunzi wanaoomba mkopo katika bodi hiyo kuhakikisha wanatoa taarifa za kweli ili kusaidia kufahamu wanafunzi wanaostahili kupewa mikopo. Akizungumzia mafanikio ya HESLB, Nyatega alisema wanafunzi wanaopata mikopo kutoka katika bodi hiyo wameongezeka kutoka wanafunzi 16,345 mwaka 2004/2005 hadi wanafunzi 56,071 kwa mwaka 2008/2009.
Alisema katika kipindi cha mwaka 2008/2009, kulikuwa na maombi 74,983 ya mikopo kwa wanafunzi, lakini wote hawakupewa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo wengine kutotimiza masharti yaliyowekwa. Pia Mkurugenzi huyo alisema bodi hiyo inatarajia kutoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 140.3 kwa mwaka wa fedha 2008/2009, ingawa awali bodi hiyo ilitenga kiasi cha Sh bilioni 117
Tidak ada komentar:
Posting Komentar