KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Morogoro John Simkoko ametamba kuibuka kidedea katika mchezo wao dhidi ya Simba ya jijini Dar es Salaam timu hizo ambazo zitakutana leo katika Uwanja wa Taifa jijini.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili jijini jana, Simkoko alisema kuibuka kifua mbele itakuwa ni muhimu kwao kwa kuwa watajiwekea mazingira mazuri katika msimamo wa ligi ya Vodacom
'"Uwezo wa kushinda tunao, vijana wangu wana hari ya ushindi na ninamshukuru Mungu kwa kuanza mzunguko wa pili vizuri na huo ndio msimamo wetu wa sasa tunataka kucheza kwa ushindi au suluhu" alisema kocha Simkoko.
Kocha huyo alisema timu yake ilikuwa katika maandalizi mazuri ya ligi na wachezaji waliingia kambini muda wa mwezi mmoja kabla ya mzunguko kuanza huku wakicheza michezo mbali mbali ya kujipima nguvu na wanaamini kwa mazoezi hayo yatawafanya wao kuwa timu ya kutisha katika mzunguko huu.
Akiwazunguzia Simba alisema ni timu nzuri kwani wanawaelewa kwa kupitia michezo yao mbalimbali waliyoiona lakini kwa staili yao mpya waliyoanza nayo wanaamini watafanikiwa kutika na ushindi kupitia kwa wekundu hao wa msimbazi.
Timu ya Polisi wao waliibuka na ushindi kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya Kagera Sugar walipoifunga kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Jamuhuli mjini Morogoro.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar