Selasa, 10 Februari 2009

CHINA YAENDELEA KUTAFUTA MASOKO AFRICA IKIWEPO TANZANIA

Rais Hu Jintao wa jamhuri ya Watu wa china amefunga leo safari ya siku 8 itakayomchukua Saudi Arabia na katika nchi 4 za kiafrika:Mali,Senegal ,Tanzania na Mauritius.Hii ni ziara ya kwanza ya rais Hu nchi za nje mwaka huu mpya wa 2009.

Rais Hu Jintao atawasili barani Afrika baadae wiki hii kwa ziara ambayo wachambuzi wa kisiasa wanasema inalenga kukuza heba ya nguvu za kiuichumi za China barani Afrika ambako imetia raslimali nyingi ili nayo ivune sehemu ya akiba ya mafuta na madini.

Rais wa China kwanza anawasili leo Saudi Arabia kwa ziara ya siku 3 kabla hakuwasili Mali,Senegal,Tanzania na kisiwani Mauritius, nchi am bazo hazina maliasili kubwa ambayo kiawaida huivutia China.

Biashara lakini kati ya afrika na China ilifikia kiasi cha dala bilioni 100 mwaka jana 2008 huku mafuta ya petroli na madini nyengine yanayopatikana Afrika yakisafirishwa China na china ikimimina bidhaa zake katika masoko ya Afrika.

2006,Rais Hu Jintao aliwaahidi viongozi wa kiafrika msaada zaidi ,raslimali na biashara .Hii ilikuwa wakati wa mkutano III wa mawaziri wa Jukwaa la ushirikiano baina ya Afrika na China uliofanyika Beijing.

Wac hambuzi wanadai madhumuni ya ziara hii eti ni zaidi kujenga imani kabla ya kufanyika mkutano wao 4 uliopangwa huko Sharm el-Sheikh nchini Misri mwishoni kabisa mwaka mwaka huu wa 2009 kuliko kufunga mikataba ya biashara.

Nchi zilizochaguliwa kutembelea mfano wa Tanzania zilichaguliwa makusudi ili kutoonesha usuhuba wa China na Afrika haushikamani tu na haja ya madini ya Afrika.Christopher Aden ,bingwa wa uhusiano kati ya China na Afrika katika Chuo Kikuu cha uchumi cha London School of Economics,ameliambia shirika la habari la ujerumani DPA kuwa Senegal yamkini imechaguliwa kutembelewa kwavile mwaka jana ilichukuwa wadhifa wa mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za kiislamu yenye wanachama 57 na kwamba China ina hamu ya kuendeleza mafungamano yake na ulimwengu wa kiislamu.

Kiu kikubwa cha China cha kujipatia nishati ya mafuta na madini kumepalilia wasi wasi juu ya sera za China barani afrika huku ikikosolewa kwsmaba imejitolea kushirikiana na serikali yoyote huko bila kujali inaheshimu nchi hiyo haki za binadamu au la.

China imeziungamkono dola kama Sudan na zimbabwe ambazo haziangaliwi kuheshimu utawala bora.

Rais Omar Hassan Al bashir wa Sudan anakwepa marufuku ya silaha ya kimataifa na anatumia silaha alizonunua China huko Dafur.

China pia imeupatia utawala wa rais Mugabe nchini zimbabwe silaha na mwaka jana 2008 ilifunga mkataba wa dala bilioni 9 na Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo kuijengea miundo-mbinu kama barabara,njia za reli,mahospitali ili China nayo ipatiwe haki za uchimbaji madini nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar